Umeme wa nyumba za kupanga ni janga la kitaifa na ghali sana

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Katika mambo ambayo yanaumiza maisha ya upangajini ni umeme

Asikwambie mtu umeme wa upangajini ni hatari tupu

Yaani mnanunua umeme kila mtu kwa mwezi elfu kumi kumi lakini wapi???bado unaisha tu

Wengine wanachanga elfu 5 tano lakini wapi??

Tuambie changamoto ya umeme wa upangajini unachukuliaje??

Serikali tunaiomba sana iangalie hizi units pls tanesco maana daaah walau basi uje mfumo wa kuwasaidia watu wa nyumba za kupanga walau wapunguziwe mzigo maana wanaonekana mita zao ni kama kiwanda kitu ambacho sio kweli

Kero za upangajini ni umeme wewe unakabiliana nazo vipi?
 
Kinacho niliza mimi chumba chenye umeme 50 lakini umeme (nje)yani juu yako na chumba cha giza 20 sasa izo pesa zote wanazotupiga za nini au ndio wanatulazimisha tujenge zetu
Ni hatar
 
Kujenga sio kirahisi hivyo
sio rahisi kiviile ila kama una nia unajenga..kwani hata ukijenga chumba kimoja cha kuanzia nje ya mji cha gharama za kawaida kuna ambaye atakuuliza na wakati wewe ndiye unayeishi?..ukweli ni kwamba waliojenga Tanzania wana kasumba ya kuwatisha wale ambao hawajafanikiwa kujenga kwa kuwaambia kujenga ni kazi lakini ukweli ni kwamba kujenga ni process rahisi sana
 
Upo sahihi kaka
 
Back
Top Bottom