sun wu umeongelea vizuri kwenye System ya KERS na hasa lengo langu hapo halikuwa Battery ila flywheel. Siku ya kwanza niliposikia KERS na kufahamu inavyofanya kazi nilicheka sana maana nilikumbuka ile mashine ya kusaga ya kijijini kwetu ambayo ilikuwa inatumia hilo flywheel.
Sasa hapo kwenye video, bahati mbaya huwezi kuangalia, ni mchezo huo huo wamefanya na zaidi hapa inatakiwa kitu kinaitwa TIMING. Motor inawashwa kwanza na kwa umeme na inaanza kuizungusha Generator. Generator inaanza kuzalisha umeme ambao unarudi tena kwenye motor ambayo inaendelea kuzunguka na kuizungusha Generator.
Hii inaenda kwa sekunde kadhaa na ndipo wanauzima umeme kutoka ukutani na umeme unaotoka kwenye Generator,
Mkuu nimekuelewa ila ili twende sawa inabidi tufahamu kwanza hii flywheel, je inatengeneza umeme au inastore umeme ambao otherwise ungepotea.., mfano nikitaka kusaga mahindi nanaweka energy 3x (kutoka kwenye umeme) ambao unafanya kazi load 2x na nyingine inapotea kama friction na heat 1x; Hivyo basi 3x = 2x + 1x (yaani ile work load na energy waste)
Hivyo basi kama hii efficient flywheel ambayo inachukua hii energy ambayo otherwise ingekuwa lost (1x) na kuirudisha mwanzo ili itumike tena ni kwamba after itabidi tuweke 2x zaidi ili ikijumlishwa na ile 1x tupate 3x kama mwanzo.., sababu hatuwezi kuli-cover ile 2x iliyotumika kusaga mahindi sababu that is work done (na hapa nimeongelea theoretically sababu ni vigumu kabisa kuondoa heat na friction waste).., kwahio hapa mkuu utaona kwamba machine yetu itakuwa efficient zaidi (ila bado tutakuwa tunahitaji some addition of energy na hii must come from somewhere, ambapo itabidi labda kuwa unaongezea mara kwa mara ingawa sio sana kama ungekuwa hauna hii energy recovery system)
unachukua nafasi ya kuizungusha motor. Motor ikizungushwa inaizungusha Generator na mchezo unaendelea.
Hii theoretically its possible and wonderfully lakini hii kitu ikifanya kazi yaani ukiongeza load (workdone) utajikuta kwamba there is some energy ambayo imekuwa used kufanya kazi, can not be recovered sasa hapo ndio unahitaji ku-tap energy from somewhere (external source) maybe wawe wanawasha umeme na kuzima in steps ili kuongezea energy mara kwa mara
Hapo wanachofanya ni kama kuitumia Energy ya KERS kabla haijaanza kupungua, kuzungusha Generator na generator inaizungusha motor. Vyombo wanavyoficha ni vile vinavyosaidia kuifanya hiyo timing na kusawazisha mambo kipindi umeme unakatwa na Motor & Generator zinaanza kujitegemea zenyewe.
Ndio hapo nasema kwa hii technology wangeweza kuweka patent na kutoa a working model ya mashine na kuuzia watu, they could have been rich beyond their wildest dreams (ila kuna watu huwa wanataka tu kuuza plans zao bila kuuza a working model.., because its not easy to such as thing as kutengeneza such machine)
Kwenye mambo ya Energy, kumbuka kuwa MAJI ni energy inayoweza kuendesha magari kwa sana tu.
Mkuu ni kweli kabisa kuna energy kubwa kwenye maji (yaani ukiweza kutenganisha hydrogen na oxygen kwenye H2O, hapo utapata energy ya kutosha ambayo haina mazara yaani recycled ila sasa issue ipo kwenye kutengenisha efficiently na mpaka sasa kuna watu wanapata challenge how to do this cheaply and efficiently (using less energy). Sababu mpaka sasa wengi wanatumia same amount of energy kutenganisha hydrogen na oxygen na ile usable energy inayopatikana
Ila WAKUBWA wa dunia hii hawawezi kuruhusu duniani waache kutumia mafuta. Dunia ikisimama kutumia Mafuta na Gas, basi kutatokea mwisho wa dunia na hali mbaya sana ya uchumi duniani maana hata nchi kama Tanzania, wanapata hela nyingi sana kwa kutumia kodi.
Mkuu believe me when I say this kwa sasa nchi nyingi kubwa na wanasayansi na makampuni makubwa wanatafuta hii (holy grail) sababu itakuwa sifa na a license to make money kwa nchi au mtu atakayekuja na such workable device wa kwanza.., people now are looking for efficient clean energy.., na sasa makampuni na nchi wana-pump millions of money kutafuta hii kitu (sio wao tu hata sisi wadau huku tukilala usiku tunaota labda tutapata a eureka moment, sababu ukifanikiwa mkuu
Sikonge Amini nakwambia umasikini utakuwa umeupiga chenga, sio wewe tu bali na vitukuu vyako)
Nimewaona jamaa the question is kwanini wasitengeneze hizi na kutoa mainstream ?, baada ya ku-google nimegundua hawa jamaa hata kuuliza tu maswali inabidi kulipia,