Umejifunza au ulijifunza jambo gani kipindi unapopitia au ulipopitia nyakati ngumu maishani mwako?

Habari za muda huu wapendwa.

Maisha ni safari ndefu sana yenye milima na mabonde.

Kuna nyakati unapitia Raha mpaka unajiona hapa duniani upo peke yako.

Kuna nyakati unapitia msoto mkali mpaka unajuta kuzaliwa, lakini kila nyakati tunazopitia kwenye maisha zinabeba ujumbe na mafunzo ambayo unaweza kunufaika kwayo siku za mbeleni.

Si vibaya kama uta share baadhi matukio ya nyakati hizo zilizokufanya ujifunze mambo mengine ya msingi.

NB;
Mimi binafsi nilipofukuzwa na kazi na kuishi maisha ya dhiki ndio nilijifunza kuwa thamani ya mwanamume kwenye jamii, ndoa au hata familia ipo kwenye kutoa.
One thing nilijifunza about life, you cant control everything. Nyakati ngumu huwa zinapita , but wewe utabaki if ukiwa mvumilivu
 
Nilipofukuzwa kazini 2017, nilipitia nyakati ngumu sana isitoshe naondolewa hapo kazini nina mwezi moja baada ya mimi kufunga ndoa, niliyaishi maisha ya msoto kwa takribani miaka 4,nimejifunza mengi na niliona rangi halisi ya wanaonizunguka, ila namshukuru Mungu alinipa subra na uvumilivu,kwa hakika sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa mara nyingine, wazazi wangu na MKE wangu kwa hakika walikuwa nami bega bega katika nyakati ngumu nilizopitia.

Hard times never last.
 
Mkuu yalokukuta ww nyakati kama zako yalimkuta ndgu yangu mwaka juzi hvyohvyo na yy alitoka kuoa asikwambie mtu
 
Hivi ni mimi tu au..?? Yaan kwangu nyakati ngumu ni kila siku yaan ubongo haujawahi tulia...mimi ni mtu wa kushushiwa na vitu vizito....yaan kila mafanikio nayopata ni kwa nguvu na akil nyingi...ni mara chache sana napata vichembe chembe vya starehe...mi naamin hakuna mtu anaye pitia mambo mepesi...
 
Kujua yupi ndugu na yupi ndugu kweli, yupi rafiki na yupi rafiki wa kweli,kikubwa nilipata kujua kuwa na akiba ya kutosha na nidhamu ya fedha ni muhimu sana,vile vile kuna watu tunadhani wanatupenda sisi kumbe si kweli wanapenda tulivonavo,ndo maana Kuna msemo unasema kwenye kipindi kigumu cha maisha yako ndipo huwa unapata kujua rangi halisi za wanaokuzunguka
 
Back
Top Bottom