Umefichwa hili kuhusu mtandao wa Linkedin

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,333
8,251
Lengo kubwa la Application ya Linkedin ni kuwakutanisha wataalamu na wabobezi kwenye sekta mbalimbali, na kutengeneza njia zaidi kwenye uzalishaji na kukua kwa vile ambavyo wanavifanya.

Ndani ya Linkedin kuna kampuni zaidi ya Milioni 57 ambazo huonesha bidhaa, huduma na fursa za kazi duniani kote.

Watu ambao wasifu wao hutazamwa zaidi na watu kwenye mtandao huu ni wakurugenzi wa makampuni, wajasiriamali, wafanyabiashara na wagavi kwenye vitivo mbalimbali.

Kitu ambacho huwenda kimefichwa kwa walio wengi kwenye mtandao wa linkedin.
  • Ipo feature inayofahamika kama "Open Candidates" hii inakuwezesha mtumiaji wa application ya linkedin kuomba fursa nyingine ya kazi pasi na mwajiri wako kufahamu.
  • Kwenye eneo la ujuzi ulionao epuka kuweka juzi hizi Leadership, communication, project management na team work, kwani idadi kubwa ya watumiaji wa mtandao huu wamejaza hizi.
  • Linkedin inamuwezesha mtumiaji wake kusoma kozi za mtandaoni kupitia ''Linkedin Learning'' ambayo ni makhususi kwa lengo la kukuongezea ujuzi kwenye taaluma yako.
Kitu gani unatamani mwana-tech akifahamu kuhusiana na linkedin, shusha comment hapo chini..
 
Linked kila mtu yuko njema ,hakuna myonge mle ,Ma CEO ndio kila mtu.....Watu mle wanajipa sifa na lakini reality hawako ivo...unaweza kudhani mtu bonge la CEO na kampuni kubwa kumbe hamna kitu...

wengi nawajua mle nina mifano hai kibao sana,kuna mmoja sana yaani ukisoma profile yake unaweza kuona ni supply bab kubwa mwenye magari na investment kubwa kubwa, reality sasa anatembelea kagari amejeza madocumnet hata jalala safi...ujanja ujanja mwingi hana mbele wala nyuma....mwingine mdada ukiona alivovaa kasuti kaphotoshop na profile yake sasa...anavikampuni 3 havina hata tender kutwa kuomba akopeshwe elfu 50..
Watanzania wengi nilichogundua linked hawana unalisia na reality wengi wanajipa sifa na uwezo ambao hawana..
 
Acha uongo boss;
 
Back
Top Bottom