Umefanya nini toka Januari 2015 hadi Disemba?

Umefanya nini toka Januari 2015 hadi Disemba?

Nimefanya mengi sana mpaka nashangaa ukuu wa Mungu........siwezi pendelewa hivi.......ila ni kwa Neema tu......
 
Namshukuru Allah nimehamia kwangu, nimeanza masomo ya jioni (degree), nimepata mkataba wa kudumu kazini na nimefanikiwa kutembelea nchi kadhaa. Vile vile nimeuza gari langu kuu kuu na kununua la maana. Malengo ya mwakani ni kufufua biashara zangu, kununua shamba na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima...... Namwomba Allah anipe uzima na uwezo inshallah.
 
Namshukuru ALLAH niko salama.Kubwa lililo niharibia Mwaka ni wahesabu kura kuto kumtangaza Mgombea wa chama changu kuwa mshindi japokuwa wapiga kura tulimpigia.
 
namshukuru mungu nimejenga nyumba yangu na nimeezeka kidogo na kuhamia mimi na mwanangu pia nimenunua gari la kuzugia,pia nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji na mbuzi,japo nilipunguzwa kazi baada ya kufanya kwa miaka miwili inshallah life goes on.natumain 2016 ntapata kazi ili nilimalizie nyumba yangu
 
uweza wa Mungu ni mkuu, amenitendea mengi hadi nashangaa, nategemea makubwa zaidi kwa uweza wa Mungu, nipo tayari kuingia 2016, God bless me
 
Nimefanya mengi sana ndani ya 2015, ni kwa Neema ya Mungu nimefanikiwa haya yote. Ila kuna moja bado, naomba Mungu anisaidie niweze kufanikisha hilo na mengi zaidi.
 
Namshukuru Mungu kwa kunifanyia kicheko kwa kila siku. Jambo kubwa nililofanya ni kujifunza kuvumilia na kujaribu bila kukata tamaa. Ila napenda kuwashukuru members wa jf wrote but Malila, Biashara2000 wametisha
 
Last edited by a moderator:
Mie nimetukanwa sana hapa kwa kuweka mtizamo tofauti wa uchaguzi na baadhi ya wana jamii wakati admins wako kimya. Nimejifunza kuwa jamvi hili ni kama kikao cha mazishi : tuko sawa wote kwa kilio ila baadae naingia ktk VW CC yangu na kwenda kwenye geti na wewe unayenitukana unapinga mbuga mpaka Tabata kwa mguu. Ila tukikutana ktk net, tunasahau hata utu wetu wa kuheshimu watu we nye age kama baba mkubwa.
 
Mwaka huu haukuwa productive kihivyo kwangu
Kwa mwakani na hii mipango mikakati niliyoweka,nisipotusua angalau kidogo,naachana na maisha nafanya vitu vingine.


Pia Bi mkubwa anataka kuona kamjuukuu so inabidi kavu ziwe nyingi.
 
Mm nimetimiza malengo yangu kwa kusimamisha vyumba viwili na kuachana na kupanga mjini
 
Nimenunua kiwanja nimefungua Duka kubwa la jumla ,nimeachana na boyfriend wangu namwomba mungu aniwezeshe 2016 nijenge nyumba kubwa .
 
Nimenunua kiwanja nimefungua Duka kubwa la jumla ,nimeachana na boyfriend wangu namwomba mungu aniwezeshe 2016 nijenge nyumba kubwa .

Hongera. Nisaidie kidogo kama umefungua duka la matumizi ya kila siku mtaji ni km sh ngapi? Na mimi nipo najichanga walau kufika April mwakani nilifungue. Nisaidie kujua kianzio nione kama na mm nina uelekeo. Asante.
 
Nashukuru kwa kuhonga sana bila ya kutetereka wala kufilisika. 2016 naingia kwa kishindo.
 
Hongera. Nisaidie kidogo kama umefungua duka la matumizi ya kila siku mtaji ni km sh ngapi? Na mimi nipo najichanga walau kufika April mwakani nilifungue. Nisaidie kujua kianzio nione kama na mm nina uelekeo. Asante.

Ok tuingie pm au wazwaz? Tatizo sio mtaji Unatakiwa upate Duka sehemu kwenye mzunguko wa watu mm langu kwa barazan nimeweka soda , maji ,bia kwa ndan nimeweka Nikaweka vitu vya matumiz Ya kawaida Ya Kila cku
Unatakiwa uangalie je kunamzunguko wa watu?
 
Back
Top Bottom