Elections 2010 Umati wa Songea ni tishio kwa Slaa

Huwezi kuamini bado kuna watu nchi hii wanampenda JK kwa sababu anapendeza na suti zake!!!

Nasema kazi bado ni ngumu!!
 
Mikoa ya kusini ilikuwa ni karata yake ya mwisho ya Mh Slaa katika kujigamba kuwa REDET NA SYNOVATE walipiga mahesabu vibaya. Lakini Rais mtarajiwa baada ya 31.10, JK ALIPOINGIA Songea hata wagonjwa waliolazwa hospitali walijikongoja kwenda kumuona na kumsikiliza.

Sasa Mh Slaa anajiandaa kuzikubali tafiti zote zijazo za wataalamu hao, huku washabiki wake baada ya kuzungumzia yale waliyoyashuhudia Songea baada yake wanavilaumu vyombo vya habari eti kwa yale wanayoyaita 'ya Mbinga'.

Ni ni kwa sababu kama hiyo iliyomfanya Mh Slaa aghairishe safari yake ya kampeni huko Mtwara na Lindi siku za nyuma. Mpaka sasa wananchi wachache ambao ni wapenzi wa CHADEMA wa Mtwara NA Lindi hawajaelezwa na wala hawaelewi kwanini kwaangusha.

Wanachadema ni wazuri sana wa kuweka YOU TUBE hapa uwanjani, basi tuwekeeni na yale ya jk kule SONGEA.

Unashangaa wingi wa watu badala ya kuwahurumia hawa maskini wasiojua A wala B ya thamani ya kula yao kwao na vizazi vijavyo

Hawa hawakuonesha nje mabasi yaliyobeba watu kwenda kuhudhuria mkutano ule.

Hawa wanaSongea ni sawa kabisa na abiria wanaoshabikia mwendo kasi wasijue nini kitatokea baada ya sekunde chache baadae.

Kwa nini serikali imegoma kufungua vyuo hadi uchaguzi upite, Ujinga na Umaskini wa Mtanzania ndio mtaji kwa CCM
 
Mikoa ya kusini ilikuwa ni karata yake ya mwisho ya Mh Slaa katika kujigamba kuwa REDET NA SYNOVATE walipiga mahesabu vibaya. Lakini Rais mtarajiwa baada ya 31.10, JK ALIPOINGIA Songea hata wagonjwa waliolazwa hospitali walijikongoja kwenda kumuona na kumsikiliza.

Sasa Mh Slaa anajiandaa kuzikubali tafiti zote zijazo za wataalamu hao, huku washabiki wake baada ya kuzungumzia yale waliyoyashuhudia Songea baada yake wanavilaumu vyombo vya habari eti kwa yale wanayoyaita 'ya Mbinga'.

Ni ni kwa sababu kama hiyo iliyomfanya Mh Slaa aghairishe safari yake ya kampeni huko Mtwara na Lindi siku za nyuma. Mpaka sasa wananchi wachache ambao ni wapenzi wa CHADEMA wa Mtwara NA Lindi hawajaelezwa na wala hawaelewi kwanini kwaangusha.

Wanachadema ni wazuri sana wa kuweka YOU TUBE hapa uwanjani, basi tuwekeeni na yale ya jk kule SONGEA.

Soma nyakati vizuri. inasemekana walihudhuria wengi wao ni watoto wenye umri chini ya miaka 18!!! Kwani umesahau maagizo ya dodoma kwa walimu wakuu kuhakikisha kwamba watoto wote wa darasa la tano na sita walitakiwa kuhudhuria pale uwanja wa jamhuri? ukiachilia mbali watu kuja kusikiliza kiduku hakuna jipya lililojitokeza. pima hizi dondoo tatu halafu ujipime upo kwenye kundi gani:
1. Watu wanaozungumza masuala = Hawa ni watu wenye fikra pevu
2. Watu wanazungumza matukio = Hawa wana fikra za kawaida
3. Watu wanazungumza watu = Hawa wana fikra finyu mno
 
Kubali msikubali kikwete yuko juu na anasela sio kama slaa akisimama jukwaani yeye n kuongelea majina ya watu na matusi na kshfa tunahitaji sera na si hayo.kikwete kafanya mengi japo mnamacho hamuoni huwzi kulinganisha miaka ya nyuma na sasa
 
Na ukiwauliza wakenya swali hilo hilo jibu litakuaje? Wakongo Waganda? Waethiopia? wazambia? wamalawi? Kama majibu yao yatafanana basi tatizo laweza kuwa sio utawala.

Man, unacheza wewe!! Hivi unaambiwa au unajua kuhusu Kenya? Ndani ya miaka mitatu tu ya utawala wa Raila na Kibaki, kuna mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi Kenya, tena wala usiseme. Wala huwezi pia kulinganisha maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania na Malawi katika muda wa miaka mitano. Labda ulinganishe na Ethiopia. Wakati mwingine usiseme kama huna data. Nenda internet utafuta progressive change in economy and human life katika hizo nchi unazozitaja, halafu uone kama unaweza kuzilinganisha na Tz. Hapo ya kulinganisha ni Ethiopia tu, lakini na yenyewe ni kwa kuwa ina raia zaidi ya milioni 80
 
Mikoa ya kusini ilikuwa ni karata yake ya mwisho ya Mh Slaa katika kujigamba kuwa REDET NA SYNOVATE walipiga mahesabu vibaya. Lakini Rais mtarajiwa baada ya 31.10, JK ALIPOINGIA Songea hata wagonjwa waliolazwa hospitali walijikongoja kwenda kumuona na kumsikiliza.

Sasa Mh Slaa anajiandaa kuzikubali tafiti zote zijazo za wataalamu hao, huku washabiki wake baada ya kuzungumzia yale waliyoyashuhudia Songea baada yake wanavilaumu vyombo vya habari eti kwa yale wanayoyaita 'ya Mbinga'.

Ni ni kwa sababu kama hiyo iliyomfanya Mh Slaa aghairishe safari yake ya kampeni huko Mtwara na Lindi siku za nyuma. Mpaka sasa wananchi wachache ambao ni wapenzi wa CHADEMA wa Mtwara NA Lindi hawajaelezwa na wala hawaelewi kwanini kwaangusha.

Wanachadema ni wazuri sana wa kuweka YOU TUBE hapa uwanjani, basi tuwekeeni na yale ya jk kule SONGEA.

Duh sasa manachukua na wagonjwa? Na wao walipanda mafuso au ambulance?..........maana huo umati unaousema uliletwa haukuja wenyewe...besides mafuriko hayo bandia hubakia kwenye mikutano kuangalia fiesta free of charge
 
Zawadi Ngoda, acha kuwaongopea watanzania, bahati mbaya kabisa mimi nilikuwepo na bado nipo songea mpaka sasa! Unaongea na watu au unaangalia kijani, unaongelea wale wamama wa kijiji cha mtanguimbole walokuwa mamevaa vitambaa vya kijani? Unajua kata yenye watu wengi kuliko zote songea..uliona kilichotokea barabarani wakati "mhesimiwa" anapita?
Barabara ya Songea Makambako alikop[ita Mh, katika eneo maarufu la bombambili, bila kusahau uswahilini lizaboni kwa wenye maisha magumu- Katika kila bendera moja ya ccm, kulikuwa na bendera mbili pembeni za chadema!!!!
Huwezi kuelewa maudhui kwa kusoma muonekano! Mimi nilikuwa kwenye huo msafara...! karaghabaho!!!:tonguez:
 
tehe teh teh teh teh me yangu macho.mm mwanakijiji tuwekee you tube ya jk songea jamani,au wana chadema tuwekeeni muwe fair jamani.
 
Zawadi Ngoda-nina wasiwasi na ubongo wako kuna uwezekano mkubwa ukawa na utindio wa ubongo to the extent huwezi kabisa kufikiri, thinking capacity is low, shallow, na kubwa zaidi wewe unaweza ukawa ni mtoto wa pembeni wa fisadi moja, ama kweli moto umewawakia sasa maji shingoni mnahaha kutafuta jinsi ya kuiba kura mnajihami sana ila tunasema 2010 hatudanganyiki-kazi pevu mnayo mitandao yenu yote tunayo tutawafuatilia kwa ukaribu sana. BIG UP SLAA
 
Mikoa ya kusini ilikuwa ni karata yake ya mwisho ya Mh Slaa katika kujigamba kuwa REDET NA SYNOVATE walipiga mahesabu vibaya. Lakini Rais mtarajiwa baada ya 31.10, JK ALIPOINGIA Songea hata wagonjwa waliolazwa hospitali walijikongoja kwenda kumuona na kumsikiliza.
Hatma ya uchaguzi huu haiko huko hata kidogo na kama ni mfuatiliaji mzuri JK sana sana anachofanya ni kutwanga maji kwenye kinu.

Dr. Slaa huenda huko hata asifike kwa sababu wenye turufu ya chaguzi hii wako aliko Dr. Slaa na ndiko anakokubalika sana. JK na Prof. Lipumba watagawana kura za huko kusini
 
Mikoa ya kusini ilikuwa ni karata yake ya mwisho ya Mh Slaa katika kujigamba kuwa REDET NA SYNOVATE walipiga mahesabu vibaya. Lakini Rais mtarajiwa baada ya 31.10, JK ALIPOINGIA Songea hata wagonjwa waliolazwa hospitali walijikongoja kwenda kumuona na kumsikiliza.

Sasa Mh Slaa anajiandaa kuzikubali tafiti zote zijazo za wataalamu hao, huku washabiki wake baada ya kuzungumzia yale waliyoyashuhudia Songea baada yake wanavilaumu vyombo vya habari eti kwa yale wanayoyaita 'ya Mbinga'.

Ni ni kwa sababu kama hiyo iliyomfanya Mh Slaa aghairishe safari yake ya kampeni huko Mtwara na Lindi siku za nyuma. Mpaka sasa wananchi wachache ambao ni wapenzi wa CHADEMA wa Mtwara NA Lindi hawajaelezwa na wala hawaelewi kwanini kwaangusha.

Wanachadema ni wazuri sana wa kuweka YOU TUBE hapa uwanjani, basi tuwekeeni na yale ya jk kule SONGEA.

Wewe ndio walewale tu, Msio na uchungu na nchi hii, Matatizo ya Watanzania wewe kwako sawa? Kwasababu unakula na kushiba? Je unajua watu huko vijijini wanaishi katika maisha ya Namna gani? Unajua Mapesa yaliyomwaga kwenye kampeni ya CCM yangeweza kufanya mambo MANGAPI YA MAENDELEO? Hapa si suala la Chama bali mustakabali wa nchi kwanza, halafu vyama baadaye. Tunataka mtu ambaye anaweza kutuletea maendeleo ya ukweli, naye ni DR SLAA (Wa ukweli).
 
Kubali msikubali kikwete yuko juu na anasela sio kama slaa akisimama jukwaani yeye n kuongelea majina ya watu na matusi na kshfa tunahitaji sera na si hayo.kikwete kafanya mengi japo mnamacho hamuoni huwzi kulinganisha miaka ya nyuma na sasa

Wewe ndio zilipendwa kwelikweli! Sasa kikwete kafanya mengi hayo mengi mengi gani zaidi ya kuendelea kufanya mambo ya bwana Ben!! yalipoisha ya Ben, Kikwete hana tena dira, hajui afanye nini mara baada ya kumaliza aliyoanza bwana Ben. Ahadi million moja zisizo na mpango, ukiwauliza wanasema hivyo ndivyo wananchi wanavyopenda kusikia!! Yaani kusikia na sio kutekelezewa!!! Anashindwa kuitegemeza nchi na anaishia kuombaomba kila leo. kama kuombaomba kusiko na mpango ndio kufanya mengi basi kweli kafanya mengi.
 
kubali msikubali kikwete yuko juu na anasela sio kama slaa akisimama jukwaani yeye n kuongelea majina ya watu na matusi na kshfa tunahitaji sera na si hayo.kikwete kafanya mengi japo mnamacho hamuoni huwzi kulinganisha miaka ya nyuma na sasa

sera si zipo kwenye vitabu tu, na kila wakati wa uchaguzi ukifika tunatunga mpya za kwenda kuwadanganyia wapiga kura, hizi ni ngonjera na nyimbo tu za kuombea kura, angalia utekelezaji wake, au umesahahu muheshimiwa aliyesema kuwa sera zao hazitekelezeki? Slaa anaongelea facts, na sasa anauza sana na sera ya huduma za jamii bure, afya na elimu.
 
Nasema hiviii.. kama kweli mnataka kujua watu wanafata nini kwenye mikutano ya CCM, ACHENI KUANDAMANA NA WASANII, watu wanafuata akina Diamond na wasanii wengine ambao wako kazini TU SI UPENZI. Mwambie Rais anayeondoka madarakani hivi karibuni ( oct 31, 2010) aachane na hilo kundi la watafutaji (wasanii) aone kama hajahutubia vumbi linalotimuliwa na helkopta yake akitua na majani uwanjani..

Thubutu!!!!!!! mtaumbuka nyieeeee.. ohooo... siku hiyo badala ya kucheka-cheka mtalia-lia:preggers:
 
Mikoa ya kusini ilikuwa ni karata yake ya mwisho ya Mh Slaa katika kujigamba kuwa REDET NA SYNOVATE walipiga mahesabu vibaya. Lakini Rais mtarajiwa baada ya 31.10, JK ALIPOINGIA Songea hata wagonjwa waliolazwa hospitali walijikongoja kwenda kumuona na kumsikiliza.

Sasa Mh Slaa anajiandaa kuzikubali tafiti zote zijazo za wataalamu hao, huku washabiki wake baada ya kuzungumzia yale waliyoyashuhudia Songea baada yake wanavilaumu vyombo vya habari eti kwa yale wanayoyaita 'ya Mbinga'.

Ni ni kwa sababu kama hiyo iliyomfanya Mh Slaa aghairishe safari yake ya kampeni huko Mtwara na Lindi siku za nyuma. Mpaka sasa wananchi wachache ambao ni wapenzi wa CHADEMA wa Mtwara NA Lindi hawajaelezwa na wala hawaelewi kwanini kwaangusha.

Wanachadema ni wazuri sana wa kuweka YOU TUBE hapa uwanjani, basi tuwekeeni na yale ya jk kule SONGEA.

Huko Songea ndio wapo nyuuuma kabisa kimaendeleao. Serikali imewasahau kabisaaaa!! Miundombinu bado duuuni kabisa. barabara za mijini tangu zijengwe enzi za mwalimu. Wamshukuru mwalimu kwa kuwajengea ile barabara miaka ya 80 na ule uwanja wa majimaji ambavyo havifanyiwa maintenance yoyote. Waliojaa pale ni wale walioenda kumshangaa raisi yupoje kwani viongozi huwa hawaendi kule mpaka vipindi vya uchaguzi. Na most of them walibebwa kwenye malori toka kwenye vitongoji mbalimbali, na wengi walilalamika kwani walipelekwa tu na kurudi walijiju wenyewe.
 
Zawadi Ngoda-nina wasiwasi na ubongo wako kuna uwezekano mkubwa ukawa na utindio wa ubongo to the extent huwezi kabisa kufikiri, thinking capacity is low, shallow, na kubwa zaidi wewe unaweza ukawa ni mtoto wa pembeni wa fisadi moja, ama kweli moto umewawakia sasa maji shingoni mnahaha kutafuta jinsi ya kuiba kura mnajihami sana ila tunasema 2010 hatudanganyiki-kazi pevu mnayo mitandao yenu yote tunayo tutawafuatilia kwa ukaribu sana. BIG UP SLAA

Maneno mengi mimi sitaki, tuwekeeni YOU TUBE ya huko Songea kama mnataka tumalize mjadala. Hivi ni vigumu sana kufanya hivyo?

Mimi ningeiweka hapa, lakini mlivyowabishi mtasema nimeitengeneza kwa hiyo sioni haja ya kupoteza muda. Na kwa maana hiyo ndio Ningefurahi kweli kama MKEREKETWA WA CHADEMA 'AMOEBA' # 29 ANGETUWEKEA Y. TUBE. Hebu msikilize alivyoandika hapa chini, ukweli hata simuelewi anachoandika.

"Zawadi Ngoda, acha kuwaongopea watanzania, bahati mbaya kabisa mimi nilikuwepo na bado nipo songea mpaka sasa! Unaongea na watu au unaangalia kijani, unaongelea wale wamama wa kijiji cha mtanguimbole walokuwa mamevaa vitambaa vya kijani? Unajua kata yenye watu wengi kuliko zote songea..uliona kilichotokea barabarani wakati "mhesimiwa" anapita? "

Chuki pembeni, angalieni hali halisi kwani siku zilizobaki ni chache na ndio kwanza Mh Slaa kapanda mpaka 12%. Je aneweza hata kuzikusanya angalau 12% zaidi ili afike 24 mpaka 31.10?
 
Nasema hiviii.. kama kweli mnataka kujua watu wanafata nini kwenye mikutano ya CCM, ACHENI KUANDAMANA NA WASANII, watu wanafuata akina Diamond na wasanii wengine ambao wako kazini TU SI UPENZI. Mwambie Rais anayeondoka madarakani hivi karibuni ( oct 31, 2010) aachane na hilo kundi la watafutaji (wasanii) aone kama hajahutubia vumbi linalotimuliwa na helkopta yake akitua na majani uwanjani..

Thubutu!!!!!!! mtaumbuka nyieeeee.. ohooo... siku hiyo badala ya kucheka-cheka mtalia-lia:preggers:

kwanini aachane na wasanii na wakati na yeye pia ni msanii na anataka ajiunge nao baada ya Oct. 31!! Akiachana nao atajishughulisha na nini hapo atakapomaliza muda wake?
 
Back
Top Bottom