Umaskini ni laana; nimeamini pia maskini ana roho mbaya sana

Wewe ni mwongo. Au unadhani watu humu ni wajinga wajinga hawajui mifumo? 3m kwa siku ni ngumu na kama ni upigaji iwe serikalini au nje ya serikalini jua ni suala la muda tu kabla ya kudakwa.
Acha wivu. Maneno yako yana mlengo wa wivu na husuda kwa 100%.
 
Hiki niandikacho ni kisa cha kweli na ndicho ninachopitia.

Nikiri kwamba nimezaliwa kwenye umaskini na nimesomeshwa kwenye umaskini mpaka namaliza elimu yangu

Nilisota kidogo tu kitaa baada ya kumaliza elimu nikapata kazi sehemu nikaajiriwa, baada ya mda kutokana na Tabia yangu ya ukimya na usiri mkuu wangu wa kazi akanihamishia idara ambayo baadae nilikuja kujua ni sehemu yenye michongo mingi ya pesa.

Nikafundishwa kazi, nikaiva. Hela zipo idara hii bwana, kwa Siku nilikuwa nikitoka kazini mfukoni kuna 3+m kama hamna hamna sana nina 1+m.

Ndani ya miezi 3 nikiwa pale nikawa niko vizuri nikanunua uwanja sehemu yenye hadhi kidogo heka 3 nikaweka mansion yangu ikiwa na uwanja wa basebal na netbal ikiwemo sehemu za kucheza watoto na mabwawa ya kuogelea.

Mpaka huu mjengo unakamilika nilitumia zaidi ya 400+m, siku nawapeleka wazazi na ndugu hawakuamini kutokana na mazingira niliyotoka na namna nilivo mkimya. Sikuishia hapo wadogo zangu tumbo moja wote nilianza mchakato wa kuwajengea nyumba kila mmoja yake na nikafanikisha nyumba nzuri za kisasa ambazo wastani nilitumia 120+m

Ndugu zangu wote nilitoa msaada kwao bila kubagua, watoto ambao walikuwa wamefeli shule niliwapa uchaguzi wanachotaka wanawafanyia, nimetoa mitaji nimepeleka vyuo vya ufundi natimiza mahitaji yao kila kitu maana hela ninayo na sioni fahari ya kuabudiwa.

Sasa baada ya miaka 6 kuona nazidi kuwekeza kwa kasi ileile tu, mashangazi wakaanza za chinichini huyu jamaa ni Freemason mimi nikiwa sijui chochote. Kuna kipindi msiba ulitokea, Mke wa mtoto wa shangazi alifariki kulingana na majukumu yangu ule msiba sikufika ila nilibeba gharama zote za msiba.

Bwana kama miezi 6 hivi za msiba kupita, napata habari k kumbe watu wanachukuzwa na mafanikio, mashangazi wanapanga mipango ya kunidhuru kwa mda mrefu na mmoja aliyepewa majukumu ya kuchukua baadhi ya vitu kwenye mwili ikawa mlopokaji akanipa mchongo wote, wala sikuvumilia nikawawashia Moto mashangazi kufatilia kumbe baba zangu baadhi wanazo habari za hii mipango na wakanyamaza. Imenitia hasira sana.

Wanasema nimemuua yule mke wa binamu yangu na moja ya masharti niliyopewa ni kuwa na roho nzuri ya kuwasadia kwa hiyo nao wanataka kulipa kisasi kwa kunidhuru. Nina hasira na hawa watu Moto niliowawashia nimejikuta nawatukana mpaka matusi ya nguoni.

Natamani siku zirudi nyuma nisingefanya huu ujinga wa kusaidia hawa wanaoitwa ndugu, huku tunakoelekea naona kabisa kuna dalili mbaya kisa mafanikio yangu

Nimeongeza nguvu zaidi upande wa mama, huko nawajengea majumba ya maana.. Sasa naona wivu waziwazi mpaka watoto wao niliowasaidia kwa hali na mali.
Pole sana mpambanaji. Nita kuinbox
 
Back
Top Bottom