kaka unashangaa hayo tu!!, nipo karibu na BULYANHULU
ni mgodi unaofahamika kama " WORLD CLASS DEPOSIT" Ktk ulimwengu wa makampuni ya UCHimbaji wa madini, Huwezi kuamini kuwa mgodi huu umekuwa kwenye uzailishaji kwa zaidi ya miaka 18 sasa...
waajiriwa wageni(expats) kutoka mataifa mbalimbali huja na kutoka na kujichumia mishahara ya kufuru, achilia mbali uzalishaji wa dhahabu yenyewe.
jambo la kushangaza, ukitoka zaidi ya km1 kutoka mgodini kuna Kitongoji cha KAKOLA ambacho hakina Reflection kabisa ya utajiri ambao Mungu ameuweka Hapo... watu wanaishi maisha Choka mbaya ile mbaya.. CHini ya MBUNGE wao MAIGE... hakuna maji, vyakula wala barabara za kueleweka, watu wanaishi kwenye vinyumba vya SLOpe..
kutoka Hapo mpka ukute barabara ya lami unahitaji kutembea kilometer zaidi ya 80..
pamoja na matatizo yoote hayo jamaa wamejitoa ufahamu, na wameirudisha CCM KWA KISHINDO.. kuanzia kura za udiwani mpaka uraisi...
potelea mbali hao wengine waliojitoa ufahamu na kuwezesha BAO la mkono!!
Hii ndio tanzania ndugu yangu!!!!
"maisha bora kwa kila mtanzania" na sasa " HAPA KAZI TU".
Sasa nimeamini kuwa umasikini wa Watanzania walio wengi ni wa kujitakia.
Nasema hivi kwa kuangalia jinsi kampeni za uchaguzi zilivyokuwa na jinsi
matokeo yanavyoendelea kutangazwa. Niliamini kuwa sisi watanzania tumetambua
chanzo cha umasikini wetu ni CCM na viongozi wake. Na hii ndio imefanya uchaguzi
wa mwaka huu kuwa wa msisimko mkubwa na hata kuwapa kazi kubwa wazee wa CCM
waliostaafu, vijana wa CCM waliobahatika kupata mrija wa kupata chochote chini
ya CCM na hata wasanii wetu waliolipwa mamilioni ya pesa ili kuwashawishi
masikini waendelee kuichagua CCM. Niliamini tunajitambua na tunaelewa haki yetu ni
nini. Lakini kwa jinsi matokeo yanavyotangazwa, nimeamini kuwa umasikini wetu ni
wa kujitakia.
Ushauri Wangu:
(1) Kama ni kweli hizi kura ni za haki. Kwa kweli mtu yeyote akija kukuomba msaada
kwa maelezo yake kuwa maisha ni magumu. Mtu kama huyu hafai kusaidiwa kabisaaaaaa!
Maana mijini unaweza kutana na mtu anakuomba nauli au pesa ale. Mtu kama huyu
unaweza mfukuza tuu akaombe ofisi za kata.
(2) Vijana wengi wakilalamika kuwa hakuna Ajira. Kwa kweli nitabaki kuwaaangalia na
kuwa support wakiwa kwenye vigenge wanacheza bao.
(3)Wanafunzi wa vyuo wakilalamika mikopo inachelewa. Watu kama hawa unatakiwa kuwaangalia
tuu.
(4)Watu wakisema hamna madawa mahospitalini watu wanalala chini. Ni kuwaangalia na kuwaambia
mmejitakiwa wenyewe kwa kurudisha utawala ambao umeshindwa kuwa support miaka 54.
Kwa ujumla ni kwamba Umasikini wetu utakaoendelea kuwepo Tanzania ni wa kujitakia.
Na nchi itaendelea kunyonywa na kuwafanya wachache kuwa mabepari na matajiri na wengine
kuendelea kuwa masikini. Inasikitishaa sanaa.
Maoni yangu::::