Reina princess
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 1,322
- 1,498
Tupo kama misukule vile
Niko Ulaya kwa miaka 12 sasa. Ninafanya kazi yenye kipato kizuri sana. Mara nyingi nimekuwa nikitoa misaada kwa watu mbalimbali wanaoniomba kwa kuwa wana maisha magumu. Nasikitika kusema kuwa tangu sasa nasitisha misaada hiyo rasmi! Watanzania wanajitakia dhiki wao wenyewe.
we ni jinga sana.....
kasaidie ukoo wenu, mbona shda kbao...
uwez mlazmisha mtu kuamini unachokiamini!
wengne wanaamini serikari inajitaidi na ina sera nzuri, tatizo ni kwa watendaji.
ndo maana sasa tunachagua watendaji tunaowaamini haijalishi ni chama gani!
raia tunataka kazi ifanyike ili kuleta mabadiliko yenye tija.
Hata kama Lowasa angekua ccm na Magufuli Chadema, nna uhakika wananchi wangemchagua wanaemuamini haijalishi chama gani.
usituletee habari zako za vyama wakati nchi yetu iko nyuma kimaendeleo. kazi kwanza vyama baadae.
Ka ulikua unategemea EL akuletee msoc unajidanganya, yule jamaa hawezi endesha nchi, anaumwa sana jamaa, anasahau sahau kila kitu. Ukawa walikua na tamaa sana kumsimamisha jamaa, wangemsimamisha mtu mwingine msafi angeweza pita kirahisi mno..
Kitu nalaumu watanzania mimi ni kuwapa wabunge wengi sana CCM, ningependa kuona rais Magufuli alafu wabunge wote UKAWA ili apewe challenge ya kutosha.. Sasa wabunge majority wakiwa CCM tunabaki kulekule, watakua wanapeana support wenyewe kwa wenyewe bungeni.
Kweni mnafikili ccm ikitoka na kuingia chama kingine masikini wataisha hapa Tanzania wasipatikane wa kuomba omba?mbona mnataka kutufanya kama wote hatuna akili,kuna mtu mmoja tu kipindi hiki ndo tumlaumu kwa kubadilisha akili zetu kumsema yule waliemuita hafai kua anafaa.na waliokua wazuri na wapinzani wa kweli kuwatupilia mbali.
Kubadilisha chama mara kwa mara ndio huleta maendeleo. Cha msingi kusiwe na chama cha kudumu madarakani. Yaani inabidi chama kilicho madarakani kiwe na hofu ya kudondoka, kutokana na hofu hiyo kitafanya vema kimaendeleo, kitaogopa kufanya ufisadi maana kinajua siku kikitoka madarakani wanaweza ishia jela. Sasa ccm haina hiyo hofu kwa sababu kila uchaguzi ukija wananchi wanasema ccm hoyee. Ccm haiwezi ogopa kufanya ufisadi kwa namna hii.
Anataka kujifanya Mungu mtoa ridhiki na anafikiri asipotoa hiyo misaada yake watakufa. Ambacho hakijui ni kwamba si ajabu wana furaha kuliko yeye anayehenyeka huko Ulaya na wanamcheka tu. Watu wengine kweli hawajitambui.Unaelewa maana ya Demokrasia?. Unacholazimisha wewe ni Udikteta, eti kwavile unawasaidia watu basi wachague chama ukipendacho. Hiyo ni RUSHWA. Msaada wako usiwe sababu ya kuwashurutisha watu.
Hivyo hivyo mlisema kwa kikwete.
Nakuunga mkono, waambie na wenzako wote wafanye hivyo, tumetaka chai sasa ole wake atakayesema ni ya moto.Niko Ulaya kwa miaka 12 sasa. Ninafanya kazi yenye kipato kizuri sana. Mara nyingi nimekuwa nikitoa misaada kwa watu mbalimbali wanaoniomba kwa kuwa wana maisha magumu. Nasikitika kusema kuwa tangu sasa nasitisha misaada hiyo rasmi! Watanzania wanajitakia dhiki wao wenyewe.
Mjinga ni yule aliyekuwa anaamini Lowassa atamletea kula, Maendeleo yako yataletwa na ww mwenyewe hao viongozi kazi yao ni kukuboreshea miundombinu ya ww kutafuta pesa,