Uswazi mara nyingi wanakosa mifumo ya maji ya bomba na vyoo bora,ndio maana utaona utupaji hovyo wa maji taka na vinyesi mitaani,miundo mbinu ya Barabara ni mibovu uswazi,hivyo uzoaji taka kwenye makazi ya masikini hua ni almost hakuna coz ya miundo mbinu ya Barabara kua mibovu,
Usafi ni gharama,unahitaji kununua vifaa vya kufanyia usafi,Sabuni,Dawa ya kuua vijidudu,kwa mtu anayeishi chini ya dola moja kwa siku,kipaumbele ni chakula zaidi,msongamano pia husababisha ugumu wa kusafisha eneo,wengi wao hawana elimu bora,hawajui madhara ya uchafu na umuhimu wa usafi wa mazingira,
Pamoja na yote hayo,
Usafi ni muhimu sana ili kuepuka,
Magonjwa yanayo sababishwa na mazingira machafu,magonjwa kama Malaria,Kipindupindu na kuhara coz gharama za matibabu nazo ni kubwa,so ni vizuri kujiepusha na maradhi kuliko kusubiri tiba,kuzuwia ni bora kuliko kuponya.