Umasikini ni mbaya sana

Kama huna pesa huna thamani utamaliza wiki hukuti sms wala missed call. Hakuna jipya utapata zaidi ya msoto na kunuka jasho mda wote

Naomba niishie hapa

umaskini huondoa ujasiri,
umaskini huchochea unyonge, hofu na kutokujiamini kabsaaaa.

umaskini unafanya mtu kuona haya wakati wote, aibu na hali ya kujifichafichaficha.

Unamfanya mtu ajiskie hastahili anachostahili kua nacho. Hajui kesho itakuje, atakula nini, atavaa nini, atalala vipi, lakini atauchapa tu usingizi mnono na fofofo tena kwa amani.

Mungu ni mwema Sana. Atujalie tusilemewe na mzigo huu mzito sana wa ufukara wa kipato, fikra na elimu kwa uchache. Lakini pia Ufukara wa mwili na roho bali uhakika wa uzima wa Milele.

Ametupatia bure nasi Tutoe bure.
 
Ni kweli ukiwa maskini hata kwenye vikao vya familia unaitwa basi tu mda mwingine ukitaka kutoa maoni unakatazwa usijeanzisha vurugu wenzako wakipewa beer wine ww unapewa soda usije leta mambo mapya.

Mimi ni mmoja wa watu waliopitia hii changamoto ya kuonekana sina msaada na mbaya zaidi ndio kipindi najitafuta nilikuwa nasononeka sana ila nilishawajua ndugu zangu ni watu wa aina gani basi nikapiga moyo konde nikijua huwezi kosa siku zote za maisha yako.
 
Au sio!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom