Nakereka sana kwa hili jambo

Pettymagambo

JF-Expert Member
Aug 21, 2017
1,423
7,911
Yaani ile unahustle kiume, mchana kutwa jasho linakutiririka, mwanaume wa shoka unapambana na kazi ngumu ambayo inaweza hata kukuibulia vichomi vya mbavu, mgongo hata kiuno.

Yote hayo unajikaza maana kuna watu nyuma wanakutegemea.

Inafika mda wa kusign out, unaiendea simu yako kwa pupa huku ukijiambia nitakuta missed calls lundo na sms ya kumwaga kutoka kwa wife, Dah! unakuta cm inakuita tu wala hakuna cha sms wala chochote kutoka kwa wife ambae unapambana kwa ajili yake, unaishiwa nguvu na unaona umefanya kazi bure.

unamtumia sms eti na mimi najihesabia nina mke, dah!
Ndoa sitaki tena, utapeli huu.
 
Mjomba, kama ni hivo kwanin upare mastress?
Kazi si umesema unafanya wewe? Ukitoka kwenye vichomi, pita kwa Ashura mwenye grocery, pata zako bia 3 baridi, potion ya mbuzi na kaugali ka ngumi, rudi nyumba ni toothpick mdomoni na ka mluzi ka kuzugia.
Haya maisha yapo tu, dont die trying to please others
 
Hapana kwakweli.
 
20231130_085028.jpg
 
Umewahi kuongea naye? Pengine anajua upo kazini , you are supposed to be working.
Sawa, natakiwa kufanya kazi, lakini simu yake tu, ama sms ya kunijilia hali na kunitakia kazi njema ingeniongezea morali nakunifanya niwahi nyumbani, ila sasa ndo hvyo tena.
 
Sawa, natakiwa kufanya kazi, lakini simu yake tu, ama sms ya kunijilia hali na kunitakia kazi njema ingeniongezea morali nakunifanya niwahi nyumbani, ila sasa ndo hvyo tena.
Unatakiwa uongee naye kuhusu hilo afahamu kwamba ana nafasi ya kukutumia sms ukiwa kazi. Wengine hawapendi usumbufu.
 
Back
Top Bottom