Umasikini na aibu

We did it! No hard feeling at all. Kila mtu maisha yake yanaenda bila mwingine. So let keep rise and shine
Huyu kama ni kweli anachosema hali yake ni mbaya kuliko faraja ya kawaida

Tena kama ameweza kuwaza na kuwazua kuwa sasa akili yake imefikia inagombana na mwili wake anauwezo mzuri wa kufikiri ila bado haisaidii kujua hilo tu

Hii hali kwa wanaume ni nafuu kidogo ila kwa mwanamke ikichanganyika na joto la mwili anaweza akajiua ni Mtu ambaye anajikuta hafai kitu

Sisi binadamu tuna ombwe ndani yetu linalotupa umaana wa kuishi

Mbaya zaidi ni la kimchakato ili kulitosheleza litahitaji maswali magumu sana mapema maishani ili liswazwe

Wengi hawana uwezo wa kujiuliza mapema mpaka hali ngumu maisha zikihusika ndipo kwao Dunia huelewaka rangi yake halisi

Wajanja kwenye Dini huweka program ya kutune hii kitu kwa waumini wao kwa kuwaambia "amelaanika kila awekae matumaini yake kwa mwanadamu" So kwa watu wa imani maisha yake huyu dada sio challenge kabisa

Ushauri_ wangu huyu si wa kunywa Dawa

Wakati huu anapaswa kuwa na watu wakomavu wawe karibu naye sana tena sana wamfariji

Aliingia kwenye mapambano ya maisha akiwa njiti kiakili

Vizuri akili yake imeshampa jibu kuwa anahitaji kukumbatiwa ndio tiba yake kwa sasa

Hata ukimshauri 'Ooh Amka jikaze anza upya hata kama kidogo kidogo' ni sawa ila kwasasa anapaswa kuliwazwa na sio kufungwa nira sizizo na mbele wala nyuma

Ana dada mkubwa ambaye ni mjinga, kwa wakati huu yeye alipaswa alone hili na alisimamie

Kapigwa na kitu kizito kama Kuna wazee wa kanisa na mama wachungaji ndio majukumu yao haya

Wamchukue akafanye utumishi wa mikono kanisani bila malipo ila wahakikishe anakula na kuvaa mpaka ajipate mbali na hapo ni matatizo juu ya matatizo
 
Umtake radhi sister angu kumuita mjinga…..

Umesema kweli vingn…

Ni kweli sijioni kama mtu ninae faa …yaan saivi wewe ukitaka kunitukana nitukane, ukitaka kunifanya nijihisi kama zezeta kwangu ni sawa tu, siamini katika mtu kunitendea jema au heshima kwa sasa sioni kama nina hadhi iyo….yaan ni kama kipo kwny uhalisia(asili)wangu…. ni kama imprinted persona yangu…

Kingine ata mm akili yangu inaamuaga kujizingira…nakua kama nimekubali huu ndo uhalisia wangu maisha yangu ndo yameanza kupuputika,ni kama nina cancer kwa wasiolewa wataisi kama na kuza mambo ila ndo ivyo nikama naitaji tu kukubali ukweli ila nitfte namna ya kutuliza hisia zangu maana sazngn nakuaga km nimechanganyikiwa…. Nawaka moto .ila muugiza unatokeaga baada ya masaa kadha mungu ananipoza……ni vita tete inakua ndani yangu…vinatokeaga sana sazngn baada ya siku 3 nawza kuamua kutembea kma ata km zaidi ya 30…miguu inavimba na swz kutembea vzr nakua naumia visigino nikiwa narudi nymbn ikipona naweza kuendelea tena kwangu iyo ni km therapy nbdlsha njia au muonkno ila unakuta kuna wanaonkmbk.najifny km naishi karibu..au ntapata lift ikiwa ilo jambo limenitokea mchana naenda kutembea asa unakuta kurudi mda unakua umeenda sana bahati inatokea napata lift…..ivyo mungu tu anakua km na yeye ananiangalia…

Ntmn kua free km zamani ila kushakua na doa haiwzkn tena…….kumeni nyenyekeza lkn..…. sioni ntaanzia wapi kutk hapa, najua peke yangu nitafeli…naitaji niwe na mtu kila siku ya maisha yangu ananielewa sisemi mwanaume ata rfk tu wa kike…. Rfk zangu hawana mda saivi …..na mm Sina nguvu yakujiinua mwnyw..na sina watu au mtu ninae muamini kivile kumwambia hali yangu…nilmwambia dada angu mmoja kionjo tu akamwambia kaka angu akanpgia akanambia naenda kuongea nn ivyo mm ni mdada mkubwa saivi nikaona km kasirika nikajfanya naenda kula…
Binadamu ndo tulivyo…zaidi utasimangwa,utafedheheswa zaidi na unavyojskia,utahukumiwa au kuonwa kama wewe ni bogus flani ivi… sina uwezo saivi wakupambania maisha yangu…..
Uyo kaka angu ana mattzo yake ila nikikaa nae vzr anaweza kunipa ata milion 4 ivi nikaanza kitu…sjui… ila nikimkamata vzr anawz kunipa.ila naogopa ntalemewa yatanishinda…

Yaan unachosema ni kweli watu wanasema pata kazi uwe busy utasahau yote….sawa pngn sikuwai kupata ile kazi ynyw yakunipa kipato chenyw ila nimepata sehemu ya ku volunteer nilkua busy sana…lkn ule uhalisia upo ndani yangu najihisi kama mm ni mbaya, na sisahau nikiamk nawaza nikilala ndicho cha mwsho kwnye akili yangu na ndoto nikiota ni hali yangu…naona kila mtu ni bora zaidi yangu,mtu yeyote ambae sio mm naona bora yake……saivi mm kuoga nawza kuka siku nne sijaoga, kupiga mswaki tu wnyw imekua ni kazi kwangu.. sjhic vbaya kinywani ile kwamba mate mabaya kumeza utajhc kichefchefu km wengi wenu mnavyojskia mm sina na meno yangu naona ata hayachafuki sana naweza kumrza wiki sjapiga mswaki na nisinuke ila ntajivuta ile kukumbk kwamba jitaidi angalau upige mswaki….. Mwili wa binadamu ni wakuwindwa ukiwa vzr tu mdomo unanuka huwz ata kula kitu bila kupiga mswaki,mm saivi nakula vzr tuu bila kuhisi uncomfort yeyote.. zamn nilkua swz kutembea nimevaa dera au sipo vzr saivi navaa dera tuu… kuvaa suruali ni kazi nyngn ya kunichosha ..narusha zangu dera ndani sivai kitu zaidi ya chupi.. aya twende …ntatoka zangu yaan mengn sio shda zangu………na ynyw ni kwamba iyo dera ndo unakuta nililala nalo na kushinda nalo siku 3 nyuma….

Mimi ni broken …najhc kama mtu alievunjwa sio kimwili tuu hadi rohoni na kwnye nafsi…….nikama tunavyoskiaga yule jamaa aliekufa na kufufuliwa na yesu hakuwai kua sawa tena wala kucheka tena…ndo nilivyo najua sitokuaga sawa tena maishn mwangu uwa nakaaga najiurzaga tena kwa sauti ivi ipo siku na mm ntakuja tu kua mtu mwnye utulivu wa nafsi sio ata niwe na vitu nipate angalau icho au niwe kuformat ubongo nisahau yote…..au Mungu anifanye nikubali hali yangu na anipe ujasiri wakuishi vyovyote vile bila kufikira sana..

Kua kwnye mahusiano mapya… yaan ile kupata mtu sidhan kama ata naweza kua kwnye hayo mahusiano na mtu mwngn naona kama sio sawa kabsa mtu yeyote kunitman najihisi kbsa uyo mtu mwngn kua na mimi nikama anajiopolea mikosi…

Mda mwngn akili yangu ikipotezea kdg kwnye uhalisia wake.nikama nikiwa nimjhx kua nakafuraha kdg….uwa naenda kujikumbushia kua mm ni fala,(disgusting,worthless,stupid,ugly)
Najikumbushia…ila unakuta kila siku 24 hrs uwa najijua mm ni uyo mtu……
 
Daah aisee hii inaitwa dark night of the soul.
Ni hatari sana, yaani unakuwa unahisi kama mwili umekufa ganzii hivi. Pole sana,

Nimesoma story yakoo, na nimeumia Kuona mtu aliyekuwa na bright future, anaishia kuwa na tamaa za muda mfupi, Kukubali promises zisizo na uhalisia na kuishia kukosa kila kitu.

Hapo itakubidi ukubali kulala mkeka uliotengeneza, sio kwa nia mbaya ila ni lazima. Inabidi uumie na uanze upya.

Badili mazingira, futa social media, Badili Namba za simu. Toweka ukaanze upya.

Utaumia, utalala njaa, utakosa mtu wa kuku sukuma ila trust me, ndo njia pekee.

Mwili huwa na akili yake tofauti na ubongo, na kupona kwa Maumivu ya mwili(depression) ni muda pekee ndo dawa, inabidi ukubali kuwa Maumivu yatakuwepo na kuisha haijulikani ni lini,

Yote kwa yote wewe ni shupavu na bado unaweza kuanza upya, never give up.
 
Nimecheka a sana kwamba wazungu wao ni wazee wa offside?
 
Bado unakumbwa na hiyo hali?
 
Tafuta MTU akuongoze ktk meditation u will be okay.

Kinachokusumbua sio umasikini ni stress za mapenzi

Kwakuwa sifikirii ktk nchi yetu kama ukiamua kupambana utakosa pesa ya kula.

And always cheap is expensive ulipenda mambo ya bure ubongo wako ukapata shida

So you can make it , ila lazima ukubali kuanza mwanzo weka aibu pembeni , go on the streets and keep fighting

As well share ur CV maybe MTU Mmoja anaweza akakupa ajira .
 
Stori inachanganya ukiisoma hii!

Huyo mwanaume yuko Australia au bado Tz?

Hivi umri miaka 30 bado yu usichana unajiitaje bibi?

Unapogundua usaliti kwa mpenzi wako tilia shaka ukweli wa penzi lake pamoja na promisses zake zingine zote na anza kumchunguza bila kuwekeza penzi lako kwake.

Kwa ulivyofikia, unahitaji kupata ushauri nasaha kutokana na mkandamizo wa mawazo ulionao.

Kama wewe msomi unajiona maskini, je wasichana wengine ambao hawana elimu wala ajira na wanaishi mitaani kwa furaha, iweje wewe!

Mradi si kilema, kubali kujishusha na kuanza upya, kuanza upya siyo ujinga na umri wako bado unaruhusu.

Kwa taarifa yako, changamoto ya ajira na kipato hapa Tz kwa sasa ni kubwa sana kuliko unavyodhani, hili ni janga la kitaifa, tuliza akili binti ndiyo upate reheal, vinginevyo utapotea kweli.

Sielewi mazingira unayoishi ili niweza kushauri sawasawa cha kufanya kitakachokusaidia.

Hata hivyo unaonekana katika maelezo yako wewe ni wife material sana.

Una haiba ambayo ukipata mwanaume muoaji wa kweli, ni lazima utadumu naye.

Sina shaka na hili, kikubwa ondoa stress kwa kujua kuwa ufukara kwa sasa ni janga la watu wote na ukistrugle lazima utawin.

Usitishwe na pretenders wa mitandaoni wanaoishi maisha ya maigizo, lakini kwa uhalisia wao wala hawakuzidi maisha halisi unayoishi kila siku..

Pole sana binti, jitulize utapata mtu aliye sahihi kwako na mwisho wa siku utasahau tu adha hizi.
 
Hatari sana.
So many layers of trauma compounding on to themselves. Usijikatie tamaa
 
Sikuizi kuna vitu vimepungua..mikono haitetemeki,nguvu nakua nazo kawaida,miguu huisha nguvu bado ila nipale nikiamua kucheza kamchezo kama kuwasha na kuzima taa..yaan nikimfkilia tuu na nikiwa nimelala miguu yangu inakua inaanza kukufa ganzi, nikifkilia kngn dk izo izo miguu yangu inakua sawa…..na moyo wangu saivi una mifumo sazngn siku nzima unakua mzito ni km ile situation inayokua umeshtushwa na kitu afu mshutuko moyoni unaanza kupungua mm iyo inawza kukaa siku nzima… lndo ivyo tuu kwa sasa lbd na ile tuu kjhs sina hadhi ndo ipo iyo kila siku…..yaan kila siku unajihc leo upo salama ila siku zako zakupotea dunian zimekarbia, au kesho yako inaenda kua ngumu zaidi kuliko ya leo……
Bado unakumbwa na hiyo hali
 
Ratiba yake kwa sasa yupo tz.. ila uwa anaenda kwao ifikapo likizo….

Asante kwa maneno yako mazuri,na ukarimu ubarikiwe sana..
Hhhm apo kwny haiba ya kuolewa sdhn km ni kweli sjion km kuitaji kuolewa..lbd in future ila sjion kbs km kitu ambacho nina uwitaji nacho…kitu nilichogundua kuhusu mm kwamba sjui ku deal na mapigo makubwa….. yaan mtu wa karbu kufariki au kunisaliti……. Next time kitu kama icho kikitokea kitanimarza….…so naona l prefer kutokua karbu sana na mtu tena maishani mwangu……lbda tuu nipate mwanaume ambae ni rfk tu na tuwe tu na mipaka usinijue wala nisikujue sana yaan tuwe ivyo ila kwnye swala la mapenzi hhhmmm!!!!..………..yaan ata sijion kama naweza kumuamn mtu anakuja anajsemsha ananipenda naona kama ni anajarb michezo na mm hehehee…na ikitokea kweli nimempenda swala la yeye kuja kunisaliti au kufa litaniangamiza afu ile naona kama nishampenda uyo mtu……naona sina uwezo wakupenda tena…..
 
Pole dada, fanya mazoezi ya kutembea kila cku hata km5 au 8. Lala vizuri, kula chakula vizuri na usisahau maombi tubu makosa Yako. Pia tafuta kazi ya kufanya hata kama itakupa kipato kidogo ucjali.
Ucangalie zamani ulikua unapata nn ww fanya sasa upate chakula na ili usahau mapito Yako.
I wish you the best.
 
Daah just wished tungeongea ila hiyo hali nilisha wahi pitia chuoni, then tena baadae mwaka juzi for almost a month.. Ni hatari na inatisha sana. Anyways kwa muda huu mawazo ya kutaka ipotee ndo yanafanya iwepo so kubali ipo na iache iwepo. Na ukimwambia mtu ambae haelewii anakuona umeshindwa kucontrol ila hapo control haipo. Pole, just keep fighting
 
Asante na asante sana pia kwa ku share… n
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…