Umasikini Kwa lugha nyengine ni Ujinga - Maarifa ni Dawa ya Umasikini

Smart Finance

Member
Joined
Apr 10, 2025
Posts
35
Reaction score
112
Umaskini hauanzi kwenye mfukoni, unaanzia kichwani. Ni hali ya kifikra kabla haijawa hali ya maisha. Mtu maskini si yule asiye na pesa, bali ni yule anayekataa kujifunza, anayepuuza maarifa, na kuamini kuwa hali yake haiwezi kubadilika. Huu ni ujinga wa hali ya juu.

Sehemu ambapo ujinga ni mwingi mara nyingi kama si mara zote pana umaskini pia.

Tunaweza kutumia msamiati ujinga ama msamiati umaskini kuwasilisha hoja moja. Tunaishi kwenye dunia ya fursa zisizo nyingi sana – utandawazi umekua Kwa Kasi kiasi kwamba kutokujua jambo Fulani ni maamuzi Yako.

Ukisikia Taifa maskini, maana yake ni taifa lenye watu wajinga wengi. Taifa lenye watu wasioweza kuvuna na kutumia rasilimali zao kwa ufanisi.

Watu wasiopenda kukosolewa wanaweza kunishambulia lakini haitabadili ukweli.

Ukijifunza, unajikomboa. Ukiwekeza kwenye maarifa, unajiandaa kuvunja minyororo ya umaskini. Lakini ukiamua kubaki kwenye kiza cha kutojua – huo si umaskini tu, huo ni ujinga uliojificha kwa kivuli cha visingizio.

Hivyo hivyo kwenye familia.. ukisikia familia Fulani ni masikini, maana yake - wanafamilia wengi wa hiyo familia ni wajinga na walishindwa au wanashindwa kutumia rasilimali zinazowazunguka vizuri na Kwa ufanisi.

Mkiwa watu 100 na kati yenu wakawepo watu 6 waliosoma na wenye akili yenye mantiki na kujiendeleza hamuwezi kujiita watu werevu kwa ujumla wenu.

Kwanini? Kwasababu Bado asilimia 94% ni watu wajinga na asilimia 6% pekee ndio wenye akili naa hivyo tunapozungumzia taifa zima tunahitimisha kuwa ni taifa la wajinga japokuwa wapo wachache wenye uwezo mkubwa.

Kumbuka ujinga ni kutokujua kitu fulani, ujinga unaondolewa pale tu muhusika/mjinga ataamua kutafuta uelewa wa jambo Hilo. Kwa maana hio unaweza kusoma lakini bado ukawa mjinga kama Elimu Yako itakuwa limited

Rai yangu ni tuongeze kasi ya kushawishi kila mmoja wetu kujenga utamaduni wa kujisomea na kujiendeleza mfululizo ili tuwe na taifa lenye watu waerevu.

Katika kitabu cha Malcom Gladwell cha "The Tipping Point" anawasilisha dhana inayofafanua kuwa ili taifa liendelee kwa kasi na tena maendeleo yatokane na shughuli za ndani ya nchi kuna mlimbikizo kiasi fulani cha maarifa na ujuzi vinavyotakiwa kufikiwa kwenye taifa kwa ujumla.

Hiko kiasi ndicho kinachoitwa the tipping point ambapo serikali haitakuwa tena chagizo la maendeleo bali jamii ndiyo itakayokuwa chanzo kikubwa cha maendeleo na mabadiliko.

📚 Usilaumu serikali Kwa Umasikini wako, jilaumu wewe mwenyewe.
📚 Usiwalaumu Wazazi Kwa Umasikini wako, jilaumu wewe mwenyewe

Chagua kujua. Chagua kuamka. Umaskini kwa lugha nyingine ni ujinga – na ujinga unatibika kwa maarifa.

Follow the Smart Finance - SW channel on WhatsApp: Smart Finance - SW | WhatsApp Channel
 
Umaskini wa raia isialumiwe serikali? Serious? Wewe hjui kama resources zina'aloketiwa"?
 
Back
Top Bottom