Ultimatum: Serikali ina siku 14 kutangaza mahakama ya Kadhi! - Wahadhiri

Status
Not open for further replies.
Turudi kwenye Hoja PM amepewa siku 14 atoe jibu? Je PM anaweza kujibu bila kupata baraka za Bunge??
 
Sidhani Lazima wakae tena kushauriana

Kwasababu PM anachoweza kuahidi ni lini serikali itapeleka Mswada bungeni nadhani hawezi kugurantee lini mahakama inaweza kuanzishwa. Maana kama sheria haitapitishwa bungeni then Hakuna Mahakama, ingawa kwa mwendo wa sasa CCM wakidhamiria ianze wataanzisha tu!
 
Sasa kamauelewi kajifunze kwenza acha kuleta blablaa, kwanza takasha kiswahili chako? alfu ndo ujekuuliza maswali ako> vibalagashia ndio walioleta UHuru na pia Julius aliva kibalagashia wakati huo Pork eater wanafubaishwa akili na wakoloni. Jufunze history ya nchii hii.

Sasa hivi umeletwa mjini na serikali ya CCM vitabu vingi tu vya kiswahili na vya Historia ya nchi. Nyerere kavalishwa balaghasia hakuvaa msalaba wakati tunagombania uhuru na Swaumu pia tulimfungisha! Kelbu we!!

Balaghasia siyo vazi la waislamu pekee yao. Ile ni kofia tu kama kofia zingine, hivyo yeyote anaweza kuvaa. Mimi ninamvalisha mbwa wangu hapa nyumbani.
 
Kweli amewekwa kwenye kona. Akijibu kwanza ataonesha weakness ya serikali ya kukubali kupokea altimatum ya kikundi fulani cha watu. Leo "wahadhiri" mara kesho "walokole" na kesho kutwa mafisadi, kila kikunid kitatoa altimatum. Pili Mh KPinda ni mkristo kujibu isshe kama hii si muafaka. Angejibu JK mwenyewe, au waziri mwislamu.
Lakini all in all inaonekana kuwa hii ni weakness nyingine ya serikali ya sasa, kuacha hali ifikie hapo.
Na Kibaya zaidi ni kuwa kama hao "wahadhiri" wakishindwa, sheikh Mkuu na wao wataonekana hawafai mbele ya macho ya waislamu.Tusiburi tuone
 
Siasa za JF bwana. Kama hisia za humu ndizo zingekua general feelings za watu.....Kuna watu hapa washaanza kuongea kwa jazba na kutishia kumbe kelele za bure tu. Tuombee amani siyo kushindana nani mwenye nguvu zaidi.
 
sawa mzee wangu, hawajamaa hawaijui nchi hii wameebuka from no where? hawakuwepo wakati ule.

Wewe unaongea nini wewe? Mafumbo ya nini? Wameibuka from no where wakina nani? Wakati ule wakati gani? Au unaogopa kutoa hoja direct ili baadae hoja yako ikiwa scrutinized upange cha kusema?
 
Mkuki kwa ngurue

Hakuna haja ya ruzuku meefurahi kusamehewa kupitisha biashara zenu bure na mme nuna kunyimwa ile ruzuku ya na MKUU.. ndio sasa mnasema tena SIO CHAGUO LA MUNGU pia mkubali OIC
Mkuu nchi huru hii hamna mambo ya kulazimishana watu. Wewe toa hoja tu kwa nini watu waikubali OIC. Kama hoja zako zina nguvu natumai ujumbe utafika ila hii simply kusema tu tukubali kitu kisa bontowar kasema haipo. Wewe kama nani? Toa hoja mkuu.
 
Jamani,

Mimi sielewi kitu kimoja; naomba msaada - mahakama ya kadhi itakuwa ya waislamu, na siyo ya serikali; sasa ni kwa nini waislamu wanataka serikali ndiyo iwaanzishie hiyo mahakama? Kwa nini wasianzishe wao wenyewe huko misikitini or wherever?

Suala ni mshiko baba, tukianzisha sisi nani atamlipa. Ni vizuri serikali iji commit ili iwe responsible kumlipa pamoja na wafanyakazi wote. Lakini pia tunataka iwe na meno kwasababu baadhi ya shaeria zake zinakinzana na sheria za kikatiba.
 
Hivi kweli kulishughulikia suala la kadhi na mahakama yake ni kukubaliwa liwepo? Kwani mliahidiwakuwa itakuwepo au litashughulikiwa? Sasa serikali imelishughukia kwa kukataa mahakama ya kadhi na Kadhi mwenyewe. sasa mnataka shughuli gani tena mnataka?
 
Akizungumza katika kongamano hilo, Sheikh Said Rico, ambaye pia ni mhadhiri, alisema, Mufti Simba si msemaji wa Waislamu wote na kwamba anajivika mamlaka yasiyo yake.

Nashindwa elewa kitu kimoja, hawa Waislam vipi? Mbona inaonekana hawana umoja(Unity). Inamaana hakuna chombo kinachounganisha waislamu wote? Mimi nilidhani BAKWATA ndicho chombo lakini kama hawa nao wanapingana na Mufti kweli wataweza kujoin nguvu kutekeleza matakwa yao. Wenyewe hawaeleweki wamejipanga vipi sasa nani atakaye heshimu matamko yao ambayo yamegawanyika? Je mtu akiuliza tamko la waislamu ni lipi achukue la BAKWATA au la hawa wajamaa?

Mimi nashauri Waislam mkae kwanza mjipange vizuri halafu ndo muwe na msimamo mmoja otherwise serikali itachukua this advantage kuendelea kuwa-puuza. Angalieni jinsi zanzibar wanavyofanya, ingawa kuna utofauti mkubwa sana wa vyama (CUF na CCM) linapokuja swala la muungano wote wanakuwa kitu kimoja na wanasikilizwa. So waislam ondoeni kwanza tofauti zenu mengine baadae.
 
CCM na hadaa , tamaa za kura ndiyo madhara haya .Walidhani ni wajanja kuliko Mrema na sasa kesha waingiza kwenye mkenge watatoka vipi ? Mrema alisema hoja ya Kadhi ilikuwa yake yeye na Chama chake CCM wakaichukua na kusema ni yao .Madhara haya ya kuiba sera .Kuna bwana mapesa siku hizi kupe mapesa ya JK , slowly tunasema CCM dira haina na inaiba sera za vyama vingine wakubali.Sasa wajue si kila kitu huibwa ili kjupata kura hapana .Kadhi huyo sasa .Pinda hana la kujibu kwanza hakuwepo wakati akina Ngasongwa wana andika haya .Leo yeye anatumwa tu .Best and the right person is JK mwenyewe aje ama Makamba wasemee hili .

Na hawa wa siku 14 wanatufanya sasa tuandae ile sheria yetu ya anti terror maana baada ya hapo wamesema wataamua .Maamuzi yao mengi huwa ni kuvaa mabomu.Wanashusha hadhi ya Waislam wastaarabu wachache .
 
MoU ya Serikali ya JMT
na
THE CHRISTIAN COUNCIL OF TANZANIA &
TANZANIA EPISCOPAL CONFERENCES

Versus

MAHAKAMA YA KADHI

TATHMINI KWA MAKINI tu unafiki na undumilakuwili wa wabunge na mawaziri
wetu kuhusu uamuzi waliochukua kwa
kuwakatia wakiristo sekta ya elimu na afya (jambo la kijamii na kiuchumi)
na kunyimwa haki ya Waislamu haki ya kuwa na Mahakama ya Kadhi (jambo la ibada na imani):

1. Haki ya Elimu na Afya ni kwa kila Mtanzania na sio jambo la dini
moja ila kama tunataka kuigawa nchi na jamii husika. Serikali yetu imeingia katika MoU inayopendelea upande
mmoja kwa hasara ya upande mwingine katika jamii inayostahili kuwa kitu kimoja,
****** ****** ******

2. Mahakama ya Kadhi sio mahakama ya kiserikali bali ni suala la ibada na
imani kwa Waislamu sio Tanzania tu bali dunia nzima, na haiwezekani kuwaachia watu wa dini nyingine kuja kusimamia masuala yetu ya ibada labda kama sote tunataka kwenda motoni,

****** ****** ******
3. MoU hiyo ina mtazamo kama vile Tanzania ni ya Wakiristo tu na Waislamu
hawakuwepo,hawapo na hawatakuwepo ili hali kila mmoja wetu anajua nani alipigania uhuru na ni nani alikaa pembeni au kumuunga mkono mkoloni wakati ule,

****** ****** ******
4. Waislamu wengi wanaamini katika hili kuwa nchi sasa inaongozwa na
Wakatoliki wakisindikizwa na
manasara wenzao na serikali tunayoichagua ni kofia tu,
****** ****** ******
4. Eti wanaoweza kuokoa masuala ya elimu, afya na tiba nchini ni
Wakatoliki na wenzao (of kozi kwa misaada
toka Ujerumani) lakini Waislamu hawawezi kwa kuwa haohao Wakatoliki na
Wamarekani wamewafungia Waislamu fursa ya kupata fedha toka nchi za Kiislamu kwa kisingizio cha ugaidi na
udobi wa fedha haramu. Je, Mahakama ya
Kadhi isingelichangia nayo kuinua sekta ya elimu na afya kwa kuwadhibiti
viongozi wabovu na mafisadi miongoni mwa Waislamu ? Vijana wa Kiislamu watakuwa na adabu, nidhamu na tabia njema bila kulelewa katika maadili na sheria za Kiislamu ? Au serikali na Wakatoliki wana njama za kutaka kuona ni vijana wa Kiislamu ndio wanaostahili kujaza magereza na kuwa mateja barabarani ?
****** ****** ******

5. MoU hiyo inaelekea imetungwa na kufikishwa serikalini bila serikali
kushirikishwa na litakuwa jambo la
kushangaza kama imekubalika na kusainiwa kama ilivyoandikwa na maaskofu
hao.
Je, ili haki hapa itendeke si na Waislamu nao chini ya mwamvuli mmoja
wangeliandika MoU yao kwa serikali juu ya Mahakama ya Kadhi na OIC na kuipeleka isaniwe na sio kuzungumzwa na
yeyote yule sembuse wasiohusika na imani
na ibada za Kiislamu na madhehebu yake,

****** ****** ******
6. Je, serikali inayopigiwa kura na watu wote hivi kweli inaweza kukubali
kutengwa kwa sababu yoyote ile
iwayo zaidi ya nusu ya wapiga kura wake kwa sababu yoyote ile ?
****** ****** ******

7. Serikali inafanya maamuzi kama vile haijui na haielewi jinsi suala la
elimu na afya lilivyo zito na linalogusa
maisha ya kila mtu na kwamba likichiwa na watu wenye tabia kama zile za
Wahutu wa Rwanda linaweza kuipeleka nchi pabaya. Au kama sivyo basi inaamini kwamba Waislamu wamechoka mno kiasi
ambacho wanahitajiwa kusaidiwa na
watu wenye imani tofauti na yao na wao watakubali na wataliona hili ni
sawa tu kwao ?
****** ****** ******
8. Waislamu walitaka Mahakama ya Kadhi na kwa kuwa hukumu za kesi
ambazo awali zingelipelekwa
kuhukumiwa kwenye mahakama isiyo na dini basi gharama zake huko zipewe
Waislamu kwa kuendesha mahakama
yao ya kiimani na kiibada bila utata wowote. Hili likakataliwa. Je,
inakuwaje sasa serikali hiyo hiyo kuwapa FEDHA
KWA MLANGO WA NYUMA wale ambao watazitumia fedha hizo ili kuchagua
madiwani wao, wabunge wao,
watumishi wao, wakuu wa wilaya wao, wakuu wa mikoa wao, mawaziri wao,
waziri mkuu wao na rais wao maana
hakuna tena chaguo la Mungu leo!!! Au serikali katika MoU hii ilichanganywa, kuchanganyikiwa au kujichanganya ?
****** ****** ******
9. Ni serikali gani yenye kujali haki na usawa inayoruhusu wakiristo
wapewe fedha na Ujerumani, Marekani,
Wakorea na Wazungu wengine halafu jamaa hao waziharamishe fedha
wanazopewa Waislamu na waislamu wenzao
kutoka sehemu nyingine duniani na hivyo kung'oa kabisa mizizi ya kuota na
kuendelea kwa Uislamu sehemu nyingi
hapa Tanzania ambazo zina watu wengi ambao wangelipenda kuwa Waislamu? Kwa uono wake serikali inadhani jambo hili linajenga udugu na umoja au linavibomoa ?
****** ****** ******
10. Je, haitatokea kuwa hadithi ya ngamia na Mwarabu jangwani kwa masuala
ya Wakiristo kuwa na Bodi za
Elimu na Afya?
****** ****** ******
11. Je, Tanzania inataka kuwa kama Belgium na magomvi yasiyokwisha kwa
kujenga tabaka mbili za jamii, yaani, jamii ya Wakiristo walionacho, na jamii ya Waislamu wasio nacho? Na hao
maaskofu wetu ndicho hicho
wanachokitaka kweli na masheikh nao wanalikubali hili ? Ni nini itakuwa
ya hatima ya msimamo na mtazamo kama huu
kwa muktadha wetu wa umoja na mshikamano wa kitaifa?
****** ****** ******
12. Nini kitatokea wakati Wakiristo ndio watakaokuwa wakimiliki viwanda
vyote vya uchapishaji vitabu na vifaa vya elimu hapa nchini na Waislamu hawana lao ? Au serikali haijui hii ndiyo nia ya wachapishaji vitabu wa Ujerumani na Marekani ili kukuza soko lao kupitia dini fulani ?
****** ****** ******
13. Nini kitatokea wakati Wakiristo watamiliki njia zote za usafiri (kama
ilivyoua biashara ya Muislamu wa
Scandinavia ili wakiristo watambe katika biashara hiyo hapa Tanzania)
achilia uwezo waliopewa TRA kuziadhibu
biashara za Waislamu na kuzipa ahueni biashara za Wakiristo ni nani
asiyejua hili.
Na juu ya hapo waweze kudhibiti kampuni za intaneti, simu za kawaida na
simu za mikononi huku Waislamu kama
wale wa Zantel wakiwekewa ngumu kila hatua ?
****** ****** ******
14. Nini kitakachotokea katika nchi endapo kama shule na vyuo vitakuwa
katika mpangilio huu:

SHULE NA VYUO BORA KABISA- ZOTE ZA WAKIRISTO

SHULE NA VYUO WASTANI-
ZOTE ZA SERIKALI

SHULE NA VYUO DUNI KABISA- ZOTE ZA WAISLAMU
****** ****** ******
15. Nini kitakachotokea dini mojawapo nchini itakapopora kazi ya 'Human
Resource Development' ambalo ni
jukumu la serikali na linalostahili kuwa katika sera mama ya chama chochote tawala kinachojua wajibu wake katika uongozi wa nchi na sio mtu mwingine ? Hatujui maana ya hili kama vile
hatukwenda shule jamani?
****** ****** ******
16. Inavyoelekea ni kwamba serikali imeshindwa kubainisha na kuonesha
waziwazi MIPAKA KATI YA
SHUGHULI ZA SERIKALI NA ZILE ZA MASHIRIKA YA KIDINI na hili sasa
linaifanya kufanya kazi kwa namna
ambayo inatia mashaka na tuhuma kubwa-ndani na nje ya nchi! Na MoU ya kiranja Wakatoliki ni tusi kwa serikali. MoU hiyo inawaambia viongozi kwamba wao maaskofu wana akili, uwezo, rasilimali, visheni, kompetensii na kapasitee kubwa zaidi ya kuongoza nchi kuliko wao na kuwa wamewaachia tu kwa sababu Katiba nawafungafunga lakini wanaamini wanaweza kuwapika watu wao, wao wenyewe, nao wakawa na uwezo mkubwa kuliko madiwani, wabunge, mawaziri, waziri mkuu na rais waliopo madarakani sasa,
****** ****** ******
17. Hivi kuna shirika la kidini litakalotamalaki katika kuwa na shule,
vyuo na hospitali litakaloajiri kwa urahisi
watu wa dini nyingine. Na hata likiwaajiri, je, litawathamini kama watu
wa dini yao ?
****** ****** ******
18. Je, ni busara na hekima kutoa ruzuku kwa SHULE, VYUO NA HOSPITALI za
WATU BINAFSI AMBAZO
HAZINA UDINI au kutoa hilohilo kwa MASHIRIKA YA KIDINI YENYE UDINI WA
KUPINDUKIA ?
****** ****** ******
19. Je, kwanini tunavumilia nchi kama UJERUMANI na zingine
zinazotanguliza UDINI kwanza wakati zikisaidia
nchi yetu. Je, nchi kama hii ina nia njema na hatima yetu ?
****** ****** ******
20. Je, SHIRIKA LA KIDINI KAMA WAKATOLIKI ambao wameanza kuonesha roho
mbaya kwa WAISLAMU
wakiachiwa kuagiza madawa ya binadamu na mifugo Waislamu watakuwa na
uhakika na usalama wa afya na maisha
yao? Na hasa katika miaka hii ambayo wenzetu wanatengeneza sio binadamu
tu bali hata manii kwenye maabara
achilia mbali 'genes' ambazo zinaamua mtu awe mbwia unga, ****** au
kafiri au mwenye kuabudu Mungu mmoja!! Na vijana wa Kiislamu wanaosoma shule za Kikatoliki watakuwa salama kweli au watafanyiwa yale Wajerumani hao hao ambao ndio marafiki zao leo waliyowafanyia watoto na vijana wa Kiyahudi kwenye miaka ya 1930 hadi 1945 ?
****** ****** ******
21. Huduma ya bima ya taifa ni kwa Waislamu tu kiasi cha Wakatoliki
kushadidia kuwa na Bima ya Afya ya
Kikatoliki? {Wengine kwangu ni mabogi tu na itafika mahala jamaa
watayaacha mabogi hayo bila wasiwasi!}. Huduma hii inaanzishwa kwa ajili ya mapadri au wafuasi wao au Watanzania wote ? Sheria ya nchi inasemaje kuhusu mifuko ya akiba ya uzeeni na afya na tiba ?
****** ****** ******
22. Kwanini serikali isitoe nafasi za masomo ya Ualimu kwa walimu wa
shule na vyuo vya dini zote na sio kwa
shule na vyuo vya Kikiristo tu ? Mbona viongozi wa zamani wa makanisa hayo waliweza kufanya mambo mengi bila msaada wa serikali. Hela siku hizi zinakwenda wapi ? Vatican au kuna ukata huo kiasi cha kulilia kugawana hela serikali inayofadhiliwa na wazungu ?
****** ****** ******
23. Serikali ikianza kugawa mapato yake kwa Wakatoliki basi kiuadilifu na
kwa haki na usawa isiache kufanya
vivyo hivyo kwa dini nyinginezo na hata kwa wale wasiokuwa na dini pia !
****** ****** ******
24. Je, serikali iliyoko madarakani inajua UZITO WA DHAMBI YA UJIVUNI NA
UBAGUZI WA KIDINI katika jamii yoyote na madhara yake kwa jamii inayojisahau na kujikuta katika
dhambi hiyo?
****** ****** ******
25. Je, wanasheria Waislamu wanaweza kutueleza ni kwa kiasi gani katiba, sheria na sera za CCM zimefuatwa au kuvunjwa katika masuala ya Mahakama ya Kadhi ulinganisha na Bodi ya Elimu ya Wakiristo na Bodi ya Afya ya Wakiristo ?
****** ****** ******
26. Wakoloni wa Kijerumani na Kiingereza hawakuupenda kabisa Uislamu lakini wao waliiachia Mahakama ya Kadhi kuendelea kuwepo kwa kutambua kwamba wanaweza kuitumia kama 'an arm of administrative law yao,' sasa angalia wenzetu wa CCM na serikali yao walivyo na akili. Pamoja na kushindwa kuwatekelezea wananchi wao mambo mengi na wengine huko Zanzibar kuanza ujuha wa kugombania shilingi milioni moja ya mafuta watakayoikota kesho, tena bila inshallah, wameshindwa kutambua fursa ambayo Mahakama ya Kadhi imewaachia nje nje, nayo sio nyingine, ila kupunguza mzigo wao ambao kama sio kwa udhaifu na kushindwa kuungana kwa vyama vya upinzani njoo 2010 chama hicho kingelikuwa almanusra kubakia madarakani.
****** ****** ******
27. Hawa jamaa sio kwamba wanaendelea kuwepo madarakani kwa sababu ya 'ujinga' wa wananchi vijijini ni kina nani wanaoweza kujitolea kubadili hali ilivyo na kuwafungua macho wananchi vijijini kwamba Chama kimoja kuwa na viti vingi bungeni ndiko kunakochangia rushwa, ufisadi, wizi wa kura, njaa, kukosa maji vijijini, shule duni, kipato duni, barabara duni na yote yanayowakabili sasa. Na kwamba kwa Waislamu vijijini kukosa Mahakama ya Kadhi watakuja ishia wote kuritadishwa wao na watoto wao watakaokujakusomeshwa na manasara ? Na katu umasikini wao hautaondoka bila Mahakama ya Kadhi kusimama kidete kwenye masuala ya ZAKAT inayotkiwa iwaondoe wao kutoka kwenye umasikini. Watambue hakuna nasara atakayewatajirisha bali ni Zakat kutoka Bait ul Mali itakayosimamiwa na Mahakama ya Kadhi kwa haki, bila rushwa na bila ufisadi na longolongo nyingi.
****** ****** ******
28. Zaidi ya asilimia 68 ya viongozi serikalini ni Wakiristo, wengi wao wakiwa Wakatoliki je wanaharibu mipango na mikakati ya kuendeleza shule, vyuo, hospitali na taasisi nyingine kama hizo ili serikali ionekane kushindwa na kuwa ni kanisa tu ndilo linaloweza kufanikisha masuala ya elimu, afya na tiba nchini ?
****** ****** ******
29. Tabia ya viongozi wetu wa juu kutaka kuendelea kuwa karibu na nchi za Kikiristo kama vile Ujerumani, Uingereza, Marekani na nyingine kama hizo halionekani kama ndio chanzo cha matatizo mengi ya kidini hapa nchini. Maana hawa ndio wanaowapa vichwa viongozi wa makanisa. KWANINI TUSIKURUBIANE KABISA NA NCHI KAMA CHINA, JAPANI, KOREA, VIETNAM NA INDIA ili kuondokana na tatizo hili la kuwa na WAFADHILI WANAOTAKA KUIFANYA NCHI YETU YOTE IWE YA KIKIRISTO ?????
****** ****** ******
30. Vinginevyo kwa kila shilingi 1 inayotolewa kwa madhehebu za KIkiristo toka nchi za Wakiristo na Waislamu nao waruhusiwe kuchukua shilingi 1 toka nchi za Kiislamu. Nchi hizo zina nia, sababu na uwezo wa kuwasadia Waislamu lakinti tatizo ni serikali na CHAMA CHA MAPINDUZI!!!!!!!!

****** ****** ******
ian_jua
 
Jamani,

Mimi sielewi kitu kimoja; naomba msaada - mahakama ya kadhi itakuwa ya waislamu, na siyo ya serikali; sasa ni kwa nini waislamu wanataka serikali ndiyo iwaanzishie hiyo mahakama? Kwa nini wasianzishe wao wenyewe huko misikitini or wherever?

Waislamu wanachotaka ni kuundwa na kutambulika kwa mahakama hii kisheria na vile vile maamuzi yake yatambuliwe kisheria. sasa ni wajibu wa serikali kulidhia na kuunda mahakama hiyo.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom