Ultimatum: Serikali ina siku 14 kutangaza mahakama ya Kadhi! - Wahadhiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ultimatum: Serikali ina siku 14 kutangaza mahakama ya Kadhi! - Wahadhiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Jul 9, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Waislamu wampa Waziri Mkuu siku 14 kutangaza mahakama ya kadhi

  Na Said Powa

  JUMUIA ya Wahadhiri wa Kiislamu Tanzania imetoa tamko lake kuhusu Mahakama ya Kadhi wakimpa wiki mbili Waziri Mkuu Mizengo Pinda atangaze ni lini Waislamu watapewa mahakama hiyo.

  Jumuiya hiyo imesema kama Pinda hatafanya hivyo, kazi ya kutoa elimu ya upigaji kura itafanyika kwa lengo la kukiadhibu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukinyima kura katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2010.

  Akisoma tamko hilo katika kongamano lililoandaliwa na taasisi hiyo, Amiri Sheikh Jumanne Amiri, alisema wanaunga mkono kwa vitendo kauli ya awali ya Mufti Simba iliyowataka Waislam wote nchini, kuungana na kuinyima kura CCM kwa maelezo kuwa imewahadaa.

  "Sisi tuna uwezo mkubwa wa kuishwishi jamii ya kiislamu na ikatuelewa kuliko hata Bakwata, kwa hiyo kazi hiyo itaanza baada ya wiki mbili kama tu waziri mkuu hatawatangazia Waislamu lini watapata Mahakama ya Kadhi," alisema Amiri.

  Alifafanua kuwa kazi ya kutoa elimu ya Mahakama ya Kadhi imeshaanza na wahadhiri wa mikoa yote wamepewa taarifa juu ya umuhimu wa elimu hiyo kwa waumini wa dini ya Kiislamu.

  Aliongeza kuwa mikutano hiyo itafanyika kuanzia ngazi ya kijiji, kata, wilaya, mikoa na taifa na kuwaomba Waislamu wawaunge mkono harakati hizo, kwa kuchangia kwa hali na mali ili kufanikisha lengo hilo.

  Katika kongomano hilo, washiriki walichanga Sh1.8 milioni kwa njia ya papo kwa papo ili kusaidia mpango huo.

  Akizungumza katika kongamano hilo, Sheikh Said Rico, ambaye pia ni mhadhiri, alisema, Mufti Simba si msemaji wa Waislamu wote na kwamba anajivika mamlaka yasiyo yake.

  "Bakwata ni taasisi kama taasisi nyingine za Kiislamu, haipaswi kufanya maamuzi yeyote ya Waislamu wote pasipo kushirikisha tasisi nyingine, katika kikao cha siri na waziri Mkuu wahadhiri hawakushirikishwa na hata wangeshirikishwa kulikuwa na sababu gani kuitana kwa siri bila ya kutangaza,," alihoji Rico.

  Mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya Waislamu 1000 ulifanyika katika viwanja vya Manzese Bakharesa, jijini Dar es Salaam.

  Source: Mwananchi Tanzania Newspaper (MCL)

  Swali kwao : Ubaya wa CCM na kampeni wataipigia wakiwepewa Mahakama na uozo mwingine wote wa CCM wataufumbia macho ?Ama kweli hawa wamepoteza mwelekeo .
   
  Last edited by a moderator: Jul 10, 2009
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Unajua CCM walidhani ni lelemama, sasa subili yanayo kuja! Yaani mungu atunusuru. Kama sasa ni amri za siku za kuhesabika, Sijui, sijui tunako enda!
   
 3. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #3
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kupitia 'chama chetu' hiki wananchi wamepumbazwa sana. MIMI sitetei uwepo wa mahakama ya kadhi, ila nasema Chama cha Masela kimezidi kudanganya, sasa kimeanza kucheza na imani za watu.Hatari sana tena sana.
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vikianza mi nitawanza hawa CCM popote walipo
   
 5. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mungu Atasaidi mambo yakae sawa

  Nimeusikiliza vizuri sanna huo muhadhara kwa wasio elewa watakuwa wanavichwa vigumu saaana

  Mungu yu pamoja nasi
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Haya Mambo huwa yatagemei sana MUngu ni sisi wenyewe tunavyopanga.
  Unadhani wale wa Rwanda walitenda dhambi sana kuliko TZ, Unadhani Kosovo Mungu hakusikia kusaidia?? (sikiliza Mungu anakupenda wa Kijitonyama)

  Ebu tupakulie uliyosikiliza kwenye huo Mhadhara
   
 7. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mungu Atasaidi mambo yakae sawa

  Halafu mie sio mpakuaji

  Huo ndio mwanzo mungu ataleta kheri
   
 8. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #8
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani,

  Mimi sielewi kitu kimoja; naomba msaada - mahakama ya kadhi itakuwa ya waislamu, na siyo ya serikali; sasa ni kwa nini waislamu wanataka serikali ndiyo iwaanzishie hiyo mahakama? Kwa nini wasianzishe wao wenyewe huko misikitini or wherever?
   
 9. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wavivu wa kuchukua hatua na kushiriki katika kutafuta muafaka wanakimbilia sababu rahisi ya Mungu atasaidia, where is this Mungu??? by the way who is this MUNGU??? La Pili umeshema umeelewa vizuri kilichojiri kwenye huo mhadhara sasa unakata kusema basi hukusikiliza au hukuelewa then.
   
 10. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
 11. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
 12. m

  mtemi Member

  #12
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hao vibaragashia wasitusumbue waende huko misikitini wachague huyo nani vile.....kazi aka kadhi(au nimekosea??),harafu kama kuna anaelewa atueleweshe kwann wanataka serikali iwaanzishie hiyo mahakam badala ya kuanzisha wenyewe??
   
 13. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Inferiority complex, Vyuo vikuu wapewe majengo ya serikali, Hapa wanataka serikali iji-comit ili kuwe na ruzuku ya kuendesha hizo mahakama.
   
 14. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mkuki kwa ngurue

  Hakuna haja ya ruzuku meefurahi kusamehewa kupitisha biashara zenu bure na mme nuna kunyimwa ile ruzuku ya na MKUU.. ndio sasa mnasema tena SIO CHAGUO LA MUNGU pia mkubali OIC
   
 15. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Sio Ruzuku wala OIC itakayoifanya jumuiya ya waislam kuwa na nguvu Tanzania na duniani, Unadhani wamarekani (Wakristo) na Saudi Arabia (Waislam) wametofautiana katika nguvu walizo nazo duniani kwa sababu ya Misaada na ruzuku au kujiunga na OIC au Vatican??? There is more than That, na hicho ndicho Waislam hawajajua, walipaswa to learn what makes the other segment of the society (christian) more dominant and influencial than their muslim counterpart
   
 16. B

  Bull JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sasa kamauelewi kajifunze kwenza acha kuleta blablaa, kwanza takasha kiswahili chako? alfu ndo ujekuuliza maswali ako> vibalagashia ndio walioleta UHuru na pia Julius aliva kibalagashia wakati huo Pork eater wanafubaishwa akili na wakoloni. Jufunze history ya nchii hii.

  Sasa hivi umeletwa mjini na serikali ya CCM vitabu vingi tu vya kiswahili na vya Historia ya nchi. Nyerere kavalishwa balaghasia hakuvaa msalaba wakati tunagombania uhuru na Swaumu pia tulimfungisha! Kelbu we!!
   
 17. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  POLe pOle mzee! Mrema naye amevalishwa, wengi bado watavaa,

  Tusiishi kwa ahistoria jamani,


  [​IMG]
   
 18. B

  Bull JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa mzee wangu, hawajamaa hawaijui nchi hii wameebuka from no where? hawakuwepo wakati ule.
   
 19. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Bull

  Ilisoma HKL achana na mambo ya uhuru huo ni mwanzo pia anawe ikasadia kuwanshua CCM kuacha Udhalimu wao
   
 20. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Wewe unaye ijua saana umebadilika au unazidi kizeeka umri huo

  Mabadiliko gani ulileta au kusaidia kwa chochote
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...