Ultimatum: Serikali ina siku 14 kutangaza mahakama ya Kadhi! - Wahadhiri

Status
Not open for further replies.
[/LEFT]

Unajua CCM walidhani ni lelemama, sasa subili yanayo kuja! Yaani mungu atunusuru. Kama sasa ni amri za siku za kuhesabika, Sijui, sijui tunako enda!

Hivi Waislamu hawawezi kuanzisha Mahakama ya Kadhi mpaka serikali iseme ni lini? Mbona wakitaka kumchagua sheikh au kujenga msikiti hawasubiri tamko la serikali?
 
Huku kijijini kwetu hakuna muislamu hata mumoja:). Je tuwashawishi wapigie chama gani wasio waislamu kwetu:D
CCM kazi mnayo maana very soon tutaona ccm MYK na ccm kanisa. Kwa kosa mlilofanya lazima, narudia lazima mkatike mara mbili. Njia ya muongo ni fupi. Hata wakristo hawadanganywi tena kirahisi ili mpate kura zao:(.
 
Nyakati za kumkumbuka Mkapa zimewadia!! akisema amesema, hakuna kucheka cheka
 
Waislamu wanachotaka ni kuundwa na kutambulika kwa mahakama hii kisheria na vile vile maamuzi yake yatambuliwe kisheria. sasa ni wajibu wa serikali kulidhia na kuunda mahakama hiyo.
Kuna NGO nyingi tu zinatambulika serikalini, lakini kuundwa kwake hakukuihusisha serikali.
 
Zaidi ya watu 1000, wamechanga 1.8mil? Mmmmmhh!
Naomba kuuliza ni wahadhiri (Lecturers) wa vyuo (Universities, colleges, institutes etc) au?
 
"Bakwata ni taasisi kama taasisi nyingine za Kiislamu, haipaswi kufanya maamuzi yeyote ya Waislamu wote pasipo kushirikisha tasisi nyingine, katika kikao cha siri na waziri Mkuu wahadhiri hawakushirikishwa na hata wangeshirikishwa kulikuwa na sababu gani kuitana kwa siri bila ya kutangaza,," alihoji Rico.
Mkichunguza kwa makini kauli ya huyo bwana, mtagundua kwamba hapa kuna ugomvi wa chini chini kati ya Bakwata na hao Wahadhiri. Hapo kila upande unaangalia ajira. Mwl. Nyerere aliwahi kusema kwamba dhambi ya ubaguzi haiishi mara moja. Utabagua kundi fulani na mtajitenga, baadaye mtaanza kubaguana wenyewe. Hapo naona tayari Wahadhiri hao wameshasema Bakwata ni taasisi moja tu ya Kiislamu kama ilivyo ya kwao ya Wahadhiri. Hapo naona Wahadhiri wameshaona kwamba Bakwata watapewa "shavu" peke yao!!
 
Kikwete haitakii mema nchi hii.Kwanini ananyamazia mjadala huu wa kidini?Mbona anao uwezo wa kukataza mijadala kama hii ya kidini? Kwa nini kila dini isiendeshe mambo yake kama ilivyo sasa?Kama mahakama zilizopo za nchi hazikidhi sheria za kiislamu basi hilo ni tatizo la dini husika kwa maana nyingine dini ibadilike ifuate misingi ya sheria za nchi na sio serikali ibadilike kwa ajili ya dini.''NI HATARI SANA NDUGU ZANGU''.Sasa inabidi hata sisi tuanze kumfundisha RAIS kazi kama hii ndogo?Ana malengo ya kuivuruga nchi?Kama sio,anasubili nini?Wakati wote rais wetu hasemi chochote kwenye mijadala mingi hatari kama hii lakini mjadala huu ni wa aina yake na hapaswi kukaa kimya.Ilani ya chama kikongwe si ni ilani aliyoinadi?Kwanini alikubali vipengele vya ajabu kama hivi kama sio kucheza na imani za watu?Kwanini chama hiki kikongwe kinadiliki kuweka mambo ya dini fulani kwenye ilani yake?Hawa waislamu hawajui katiba ya nchi inavyosema? Serikali itakuwa tayari kukubali kuanzisha mahakama za dini zingine(wakristo)?Kwani katiba inasemaje? Wanataka kutuletea ya Rwanda?
Nadhani nimesomeka wandugu.............
Waislamu wampa Waziri Mkuu siku 14 kutangaza mahakama ya kadhi

Na Said Powa

JUMUIA ya Wahadhiri wa Kiislamu Tanzania imetoa tamko lake kuhusu Mahakama ya Kadhi wakimpa wiki mbili Waziri Mkuu Mizengo Pinda atangaze ni lini Waislamu watapewa mahakama hiyo.

Jumuiya hiyo imesema kama Pinda hatafanya hivyo, kazi ya kutoa elimu ya upigaji kura itafanyika kwa lengo la kukiadhibu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukinyima kura katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2010.

Akisoma tamko hilo katika kongamano lililoandaliwa na taasisi hiyo, Amiri Sheikh Jumanne Amiri, alisema wanaunga mkono kwa vitendo kauli ya awali ya Mufti Simba iliyowataka Waislam wote nchini, kuungana na kuinyima kura CCM kwa maelezo kuwa imewahadaa.

"Sisi tuna uwezo mkubwa wa kuishwishi jamii ya kiislamu na ikatuelewa kuliko hata Bakwata, kwa hiyo kazi hiyo itaanza baada ya wiki mbili kama tu waziri mkuu hatawatangazia Waislamu lini watapata Mahakama ya Kadhi," alisema Amiri.

Alifafanua kuwa kazi ya kutoa elimu ya Mahakama ya Kadhi imeshaanza na wahadhiri wa mikoa yote wamepewa taarifa juu ya umuhimu wa elimu hiyo kwa waumini wa dini ya Kiislamu.

Aliongeza kuwa mikutano hiyo itafanyika kuanzia ngazi ya kijiji, kata, wilaya, mikoa na taifa na kuwaomba Waislamu wawaunge mkono harakati hizo, kwa kuchangia kwa hali na mali ili kufanikisha lengo hilo.

Katika kongomano hilo, washiriki walichanga Sh1.8 milioni kwa njia ya papo kwa papo ili kusaidia mpango huo.
Akizungumza katika kongamano hilo, Sheikh Said Rico, ambaye pia ni mhadhiri, alisema, Mufti Simba si msemaji wa Waislamu wote na kwamba anajivika mamlaka yasiyo yake.

"Bakwata ni taasisi kama taasisi nyingine za Kiislamu, haipaswi kufanya maamuzi yeyote ya Waislamu wote pasipo kushirikisha tasisi nyingine, katika kikao cha siri na waziri Mkuu wahadhiri hawakushirikishwa na hata wangeshirikishwa kulikuwa na sababu gani kuitana kwa siri bila ya kutangaza,," alihoji Rico.
Mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya Waislamu 1000 ulifanyika katika viwanja vya Manzese Bakharesa, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Tanzania Newspaper(MCL)

Swali kwao : Ubaya wa CCM na kampeni wataipigia wakiwepewa Mahakama na uozo mwingine wote wa CCM wataufumbia macho ?Ama kweli hawa wamepoteza mwelekeo .
 
Jamani,

Mimi sielewi kitu kimoja; naomba msaada - mahakama ya kadhi itakuwa ya waislamu, na siyo ya serikali; sasa ni kwa nini waislamu wanataka serikali ndiyo iwaanzishie hiyo mahakama? Kwa nini wasianzishe wao wenyewe huko misikitini or wherever?

Kwasababu wanataka iwe na nguvu ya kiserikali na serikali iwalipie gharama za kuiendesha. Kazi kweli kweli hawa watoto wa mjakazi. Akili zimebunguliwa na madrasa hawawezi hata kufikiria mambo ya maana.
Kwa kweli MUNGU apishie mbali maana naona statement kama za akina Bull zinaonyesha tayari wanajiandaa kwa jihad. Mabomu ya Mbagala na kwingineko inabidi yahifadhiwe vizuri maana hawa jamaa hawachelewi kwenda kuyachukua na kuanza kujilipua.
 
Kikwete haitakii mema nchi hii.Kwanini ananyamazia mjadala huu wa kidini?Mbona anao uwezo wa kukataza mijadala kama hii ya kidini? Kwa nini kila dini isiendeshe mambo yake kama ilivyo sasa?Kama mahakama zilizopo za nchi hazikidhi sheria za kiislamu basi hilo ni tatizo la dini husika kwa maana nyingine dini ibadilike ifuate misingi ya sheria za nchi na sio serikali ibadilike kwa ajili ya dini.''NI HATARI SANA NDUGU ZANGU''.Sasa inabidi hata sisi tuanze kumfundisha RAIS kazi kama hii ndogo?Ana malengo ya kuivuruga nchi?Kama sio,anasubili nini?Wakati wote rais wetu hasemi chochote kwenye mijadala mingi hatari kama hii lakini mjadala huu ni wa aina yake na hapaswi kukaa kimya.Ilani ya chama kikongwe si ni ilani aliyoinadi?Kwanini alikubali vipengele vya ajabu kama hivi kama sio kucheza na imani za watu?Kwanini chama hiki kikongwe kinadiliki kuweka mambo ya dini fulani kwenye ilani yake?Hawa waislamu hawajui katiba ya nchi inavyosema? Serikali itakuwa tayari kukubali kuanzisha mahakama za dini zingine(wakristo)?Kwani katiba inasemaje? Wanataka kutuletea ya Rwanda?
Nadhani nimesomeka wandugu.............

Kwakweli hata mimi sielewi kwanini bwana mkubwa yuko kimya kwenye issue sensitive kama hii. It is so dangerous kwa kweli.
 
Hivi Waislamu hawawezi kuanzisha Mahakama ya Kadhi mpaka serikali iseme ni lini? Mbona wakitaka kumchagua sheikh au kujenga msikiti hawasubiri tamko la serikali?
Mahakama ya Kadhi ni suala la KIKATIBA. Ikianzishwa haitakuwa NGO. Itakuwa na hadhi sawa na hizi mahakama tulizonazo ili HUKUMU na MAAMUZI yake yatambulike kisheria.
Tujifunze tu kutoka nchi jirani jinsi walivyoziunda mahakama hizi ili kuepusha SHARI zisizo za lazima. Tumekubali awepo MUFTI, kwa nini sio KADHI wakati BIBLIA na QURAN vipo IKULU na vinatumika!
 
Inferiority complex, Vyuo vikuu wapewe majengo ya serikali, Hapa wanataka serikali iji-comit ili kuwe na ruzuku ya kuendesha hizo mahakama.

una uhakika na unachosema? unajua sheria zinazotawala katika kuanzisha taasisi kama hizi au mawazo yako umeyaelekeza kwenye ruzuku tu, ni taasisi ngapi za kidini zinapata ruzuku toka serikalini iweje hili lliwe geni au jipya? ingekuwa rahisi kuanzisha bila kuhitaji baraka za serikali wala msingejua imeanza lini lakini haya ni masuala ya kisheria zaidi waachieni wenyewe waislam wapambane, wanajua wanachokifanya!
 
Mkuu nchi huru hii hamna mambo ya kulazimishana watu. Wewe toa hoja tu kwa nini watu waikubali OIC. Kama hoja zako zina nguvu natumai ujumbe utafika ila hii simply kusema tu tukubali kitu kisa bontowar kasema haipo. Wewe kama nani? Toa hoja mkuu.

Hoja ya nini? mengi yamezungumzwa na kuandikwa juu ya hili, kama wapo ambao hawajaelewa hawataelewa hata wapigiwe ngoma, wanaoihitaji wanafahamu umuhimu wake, kinachotakiwa ni serikali kuwapa haki zao, kwanini taasisi za kimataifa za kiislam zikitaka kuingia lazima kuwe na kelele, ina maana waislam hawana haki ya kufaidika na taasisi zinazoweza kuwasaidia, tazama jinsi viongozi wa alharamain foundation walivyotolewa nchini, na pia taasisi nyingine zipo lakini misaada yake ni highly controlled na govt, why? ni kufuata propaganda zisizo na maana, kubwa mtasingizia ugaidi etc, huku ni kuogopa vivuli!

Tueleze ukweli wewe maana najua unafahamu sababu wala haikuwa uonevu, hata mimi ningeweza kuwafukuza.
 
sasa kamauelewi kajifunze kwenza acha kuleta blablaa, kwanza takasha kiswahili chako? Alfu ndo ujekuuliza maswali ako> vibalagashia ndio walioleta uhuru na pia julius aliva kibalagashia wakati huo pork eater wanafubaishwa akili na wakoloni. Jufunze history ya nchii hii.

Sasa hivi umeletwa mjini na serikali ya ccm vitabu vingi tu vya kiswahili na vya historia ya nchi. Nyerere kavalishwa balaghasia hakuvaa msalaba wakati tunagombania uhuru na swaumu pia tulimfungisha! Kelbu we!!

goose..!!
 
Hivi kweli kulishughulikia suala la kadhi na mahakama yake ni kukubaliwa liwepo? Kwani mliahidiwakuwa itakuwepo au litashughulikiwa? Sasa serikali imelishughukia kwa kukataa mahakama ya kadhi na Kadhi mwenyewe. sasa mnataka shughuli gani tena mnataka?

Si unajua tena wazee wa "shughuli" hao, wakipewa ubwabwa tu kimyaaa!!
 
Hoja ya nini? mengi yamezungumzwa na kuandikwa juu ya hili, kama wapo ambao hawajaelewa hawataelewa hata wapigiwe ngoma, wanaoihitaji wanafahamu umuhimu wake, kinachotakiwa ni serikali kuwapa haki zao, kwanini taasisi za kimataifa za kiislam zikitaka kuingia lazima kuwe na kelele, ina maana waislam hawana haki ya kufaidika na taasisi zinazoweza kuwasaidia, tazama jinsi viongozi wa alharamain foundation walivyotolewa nchini, na pia taasisi nyingine zipo lakini misaada yake ni highly controlled na govt, why? ni kufuata propaganda zisizo na maana, kubwa mtasingizia ugaidi etc, huku ni kuogopa vivuli!
hakuna haki bila wajibu!! wanaoomba kadhi au kujiunga oic wana wajibu wa kutii na kufuata sheria na taratibu tulizojiwekea wote, kudai kadhi kwa njia wanayofanya ni kutaka kuleta fujo!! kwani dini zingine hawana mambo yao ya kiibada? kila dini ifanye yale wanayoona ni ya kwao bila kuomba ridhaa ya serikali!! serikali ni ya watu wa dini zote!
 
halafu dhana hii ya utegemezi ni mbovu kabisa!!! jifunze kujitegemea!!!kama unataka kusaidiwa kwa masharti hayo,si lazima wakusaidie ukiwa huku,unaweza kwenda huko kwao ukafaidike vzr na hiyo misaada unayofdhani huwezi ipata ukiwa huku!!
 
CCM ni kupigwa buti tu ,wakiikubali wasiikubali ,wengi wechachoka nayo ,zinatafutwa sababu za kuzidi kuibana ili itoe wakimbizi wa kisiasa kutoka CCM kwenda upinzani ,njia ni hii hii wanayokwenda nayo waislamu ,mambo ni kugandamiza tu .
 
hakuna haki bila wajibu!! wanaoomba kadhi au kujiunga oic wana wajibu wa kutii na kufuata sheria na taratibu tulizojiwekea wote, kudai kadhi kwa njia wanayofanya ni kutaka kuleta fujo!! kwani dini zingine hawana mambo yao ya kiibada? kila dini ifanye yale wanayoona ni ya kwao bila kuomba ridhaa ya serikali!! serikali ni ya watu wa dini zote!

kutii bila haki ni utumwa! suala hili sio la leo wala jana ni la muda mrefu, kama ni utii sasa umegeuka utumwa,

kumbuka serikali ipo kwa ajili ya wananci, kama kila mmoja ana uwezo wa kufanya analolifikiria basi hakuna umuhimu wa kuwepo kwa serikali,

narejea kila jambo lina taratibu zake, ingekuwa kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi lipo ndani ya maamuzi ya waislam nadhani lingefanyika muda mrefu, lakini hili suala ni la kisheria na ndio maana tamko la serikali linahitajika, kwahiyo waislam wavunje sheria kwa kuanzisha mahakama ya kadhi bila idhini ya serikali? huo ndio utii wa sheria?

achilia mbali gharama za kuendesha ebu serikali iseme waislam anzisheni mahakama ya kadhi na hatutawagharamia kwa maana hatuwezi kutumia kodi za watanzania kwa manufaa ya waislam, ili wailam washindwe wenyewe kwa umaskini wao!

suala la misaada mkuu truev, you are wrong, taasisi zote za dini zinaendeshwa kwa misaada, mpaka kodi za nyumba za watendaji wa taasisi zinalipwa na misaada, hili sio geni, na kama kujikomboa basi ianze kujikomboa serikali kwa kujitegemea, then taasisi nyingine zifuatie, pana madhehebu ikiondolewa misaada in one day tu hapatakuwa na mfuasi hata mmoja!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom