Uliyelelewa kijijini unakumbuka nini wakati wa sikukuu?

Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
10,317
18,524
Wakuu leo nilikua najaribu kukumbuka baadhi ya matukio ya kijijini wakati wa sikukuu kama Nane nane, mwaka mpya, Christmas, Eid, Pasaka n.k
Kuna mambo nikikumbuka nacheka sana

1. Siku ya sikukuu ndio tulikua tunakula wali mara nyingi wali maharage na nyama.
Siku hiyo watoto wote mnakua na furaha, hakuna kutumwa ukanuna.

2. Siku ya siku ya sikukuu baada ya kula lunch (Ugali nyama au wali Maharage) mnapewa shilingi mia kwenda banda la video, movies maarufu zilikua Rambo, Komandoo mlachambo, ngumi zikipigwa watu wanashangilia kwenye banda la video.
TV zilikua ni Hitach (Nyeusi) inch 24 tena kijijini kwetu alikua nayo mtu mmoja tu.

3. Siku chache kabla ya sikukuu unanunuliwa nguo, mara nyingi nilinunuliwa jeans za mtumba na mashati yenye maua maua, nilikua napenda kweli.

4. Kununua big G au buble gum au Jojo, siku ya siku sikuu ndio ilikua wakati muafaka wa kula jojo maana unapewa pesa.

5. Kunywa soda, mkiwa wengi mnanunuliwa mgawane, sasa wengine walikua wanalilia kunywea kwenye chupa hawataki soda ya kwenye vikombe

Nimeyamiss sana yale maisha

6..... Ongeza zingine
 
Muda wa kwenda kutembea lazma uwapitie wenzako wakuone uvopendza na nguo mpya then muend kutembea mitaa ya mjini kuanglia muvi au kucheza vikamali vya 50 vya kurusha ring ...
 
Back
Top Bottom