Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,530
- 217,794
Kiukweli nimepita maeneo kadhaa ya Dar es Salaam , na hakika leo hakukuwa na Sikukuu ya Pasaka , ilikuwa Jumapili tu kama Jumapili nyingine zilizopita , kwenye Majumba ya watu wengi vimepikwa vyakula vya kawaida tu , vile vya siku zote tu kama ugali , wali , spinachi , maharage , matembele , nyama na samaki .
Hakukuwa na Vyakula Maalum kwa ajili ya Pasaka , unaweza kudhani wakazi wote wa DSM Wamefunga Ramadhan.
Uchunguzi wangu umebaini kwamba dhiki ya miaka 7 mfululizo ya wananchi wa Tanzania ambao idadi yao inakadiriwa kuzidi mil 65 , huku walioajiriwa na serikali wakiwa chini ya laki 6 , na ambao pia hawakuongezwa mshahara , posho wala marupurupu kwa miaka 7 ndio Sababu kubwa iliyosababisha kudorora kwa hali za familia nyingi , kiasi cha kusababisha sikukuu ya pasaka kudorora kabisa , Hakuna Shangwe wala vigeregere , kuna taarifa kwamba hata sadaka za makanisa zimeporomoka zaidi ya nusu .
Nakulilia Tanzania .