Ulisifika Kwa Lipi Shuleni....

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
229
Wakati tukiwa tunasoma kila mtu alikuwa na sifa zake na tabia ambazo zilifahamika sana kwa wanafunzi wenzako
.
Mfano Mimi nilipokuwa shule nilikuaga mpiga kelele sugu darasan
.Nilikuaga siandiki notes darasani wala kujibu maswali darasani lakini pia
.Nilikuaga fundi wa kujitetea pale napokutwa na kesi yaani mwalimu alikuwa akinipa fursa ya kujitetea basi hawezi niadhibu najitetea hadi ananiacha"

Je wewe ulikuwa na sifa gani Unazozikumbuka wakati ukiwa unasoma?
 
Nilikuwa kipaji cha kujieleza mbele ya umma bila woja walimu walinipenda kwa hilo tu nje ya hapo nilikuwa mkorofi ukinitibua tu nafanya kweli mpaka namaliza darasa la saba 1978 ipandikilo primary school nilimkwida mwalimu mkuu nikamchania shati lake aisee kilichofuata hapo nilipelekwa staff nilishambuliwa kama mpira wa kona nilipigwa mpaka basi wakajua sitakuja shule ila kesho tena wakaniona tena sina hata muda nao enzi hizo shuleni unachezea bakora za kutosha taarifa zikifika nyumbani na kwenyewe unachezea lakini sasa hivi piga mtoto wa watu kama hujaitwa central police
 
Wakati tukiwa tunasoma kila mtu alikuwa na sifa zake na tabia ambazo zilifahamika sana kwa wanafunzi wenzako
.
Mfano Mimi nilipokuwa shule nilikuaga mpiga kelele sugu darasan
.Nilikuaga siandiki notes darasani wala kujibu maswali darasani lakini pia
.Nilikuaga fundi wa kujitetea pale napokutwa na kesi yaani mwalimu alikuwa akinipa fursa ya kujitetea basi hawezi niadhibu najitetea hadi ananiacha"

Je wewe ulikuwa na sifa gani Unazozikumbuka wakati ukiwa unasoma?
Kufaulu Kwa Viwango vya Juu Bila Kuwa na Makundi ya Mijadala Shuleni (Discussion Groups)
 
Wakati tukiwa tunasoma kila mtu alikuwa na sifa zake na tabia ambazo zilifahamika sana kwa wanafunzi wenzako
.
Mfano Mimi nilipokuwa shule nilikuaga mpiga kelele sugu darasan
.Nilikuaga siandiki notes darasani wala kujibu maswali darasani lakini pia
.Nilikuaga fundi wa kujitetea pale napokutwa na kesi yaani mwalimu alikuwa akinipa fursa ya kujitetea basi hawezi niadhibu najitetea hadi ananiacha"

Je wewe ulikuwa na sifa gani Unazozikumbuka wakati ukiwa unasoma?

Ukimya.
 
tulikuwa wawili tukitumia dawati moja, mimi nikiingia asubuhi mwenzangu mchana.

nikapewa jina la wa asubuhi na mkuu wa shule alijua hilo,kazi ikawa kila saa 8 ananitafuta nika saini ila haikudumu.
 
1. Utoro, nimeanza utoro toka darasa la kwanza, nakumbuka hadi mtihani wa kwenda darala la pili nilikuja kushtuliwa na mshikaji huku washafanya hisabati, darasa la pili hivyo hivyo, la tatu nilisoma mwezi mmoja kisha nikatokomea kusikojulikana eti nikaibuka kufanya mtihani wa darasa la nne, mwalimu akanigomea ikabidi wanirudishe tena la tatu.

Ilipofika darasa la 6 nikarudia tabia yangu nikaja kuibuka la 7, shuleni walikua wananijua kwa sufa moja tu, utoro sugu ila siku nikiibuka kwenye mtihani namba moja hadi 3 hainikosi.

2. Utorokaji, jamani nilikua natoroka shule balaa, hadi nilipohamishiwa kwa mwalimu bado nikawa natoroka tu kwenda hom, mwalim hakunichapa aliniweka chini akanishauri nikaacha kutoroka ila nilipoenda secondari nikarudia tabia ya kutoroka na kuchelewa..

Sekondari nikasoma shule ya bweni ya serikali iko katikati ya mji, ikawa kila wiki lazima nitoroke kuanzia ijumaa narudi jumatatu alfajiri maana hapo mjini alikuwepo baba mdogo na akawa hanimind maana matokeo yangu hayakua na shida.

3. Kuna tabia nyingine nilikua nazo ingawa hazikua zinajulikana ni wizi wa madaftari na kalam, kila mhula ukianza tulikua tunapewa/kuja na madaftari mapya huko shule ya msingi, sijawahi kukunua daftari, nilikua na hom library yangu ya madaftari ya wizi mapya najaladia tu jalada zuri huwezi kujua ni yako.

Sekondari pia hivyo hivyo, wale waliokua na miandiko mizuri na mpangilio mzuri wa maandishi ilikua ikikaribia tu mtihani lazima niibe madaftari yao nikajisomee, mitihani ikiisha naweza kulirudisha hapo darasani nikalitelekeza au nikaamua kulificha kabisa.

Sure nimeyamisi sana maisha ya shule.
 
Kusomea ndani ya chumba cha generator la shule, hadi siku moja Gombera akanikamata wenzangu wakiwa kwenye misa ya asubuhi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom