Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Binafsi nimewasiliana na wanachama wengi humu ndani (ME + KE), lakini mbali na kuleteana masikhara na kudanganyana kule PM sijawahi kabisa kutaka kufahamiana na mtu humu ndani. Naamini kuna waliokuwa na nia njema na wako Genuine, lakini waovu, wauaji, watekaji, mamluki na matapeli wako wengi sana mitandaoni. Hivyo wale watu wema wanisamehe tu.........

Nashauri vijana, hata kama umependa na kuvutiwa na mwandiko wa mtu fahamu kwamba huku kwenye mitandao kila mtu huonekana ni malaika japo uhalisia hauko hivyo. Nawafahamu watu ambao wameshaumizwa na kuvurugwa kisa haya mawasiliano ya humu JF, Twitter na Instagram. Binafsi nimewahi kutumiwa links za mitego na E-Mails nyingi huko PM.

Wengine wanaanzia mbali kwa kujenga urafiki mimi nawachora tu nasema Hiiiiiiiiiiiiiiiii. Huko PM nimepewa ofa za kubwa za kufa mtu, wengine wanasema wananipenda sana (wanajaribu kunijaza Sweet-Nothing) , wengine wananiletea vitisho,wengine wanataka ushauri, wengine wananiletea umbeya na majungu, wengine wanakuja kunimwagia misifa. Sasa kama ukiwa na kichwa kibovu itakula kwako. There's No Free Lunch in the World: You Eat the Devil's Food, You Pay the Devil's Bill....

Ila kama umempenda mtu wewe jilipue at your own risk, lakini kaa ukikumbuka kwamba waliomo humu ndiyo haohao wa mtaani kwako. Tanzania ya leo imejaa watu waovu wengi mno, tumefika pabaya sana, kuwa makini (Be vigilant and don't have unrealistic expectations).....

Una nakosea ndugu Mgonga Like ???
Hapo umenena kuna kajamaa kanajiita infantry soldier kalikuwa kanakuja sana PM niliwahi kukastukia kuna Siku alifanya jaribio la udukuzi nilistukia kwenye email address fake nayotumia kuna notifications nikaacha amalize kazi yake
 
Tatizo siyo kutumiwa ujumbe au kusumbuliwa PM, tatizo ni uharamia unaofanywa na watu waovu huku mitandaoni. Tunawindana kama wanyama, hasahasa pale unapokuwa mkosoaji mkubwa mwenye mawazo ya tofauti ua ushawishi dhidi ya chama tawala. Matapeli nao hawako nyuma, wameumiza watu wengi sana humu ndani. Usipokuwa makini utaumizwa vibaya,.........
Hiyo ndiyo sababu ya Ibrahim infantry soldier kuniwinda ila nilimuwekea mtego wa kumjua na nishamjua
 
Binafsi kama kuna mtu ananifatilia kwa nia mbaya namkaribisha, kwa sababu ujinga wa watu kama hao huwa wanaamini sana kwenye uwezo wao wa kutimiza uharifu wao wasijue kama wanakoenda kufanya uharifu kukoje!! Wadau tuwe makini kulingana na wadau wengine wanavyotoa maoni hayo!!
 
Binafsi kama kuna mtu ananifatilia kwa nia mbaya namkaribisha, kwa sababu ujinga wa watu kama hao huwa wanaamini sana kwenye uwezo wao wa kutimiza uharifu wao wasijue kama wanakoenda kufanya uharifu kukoje!! Wadau tuwe makini kulingana na wadau wengine wanavyotoa maoni hayo!!

Pole .. Jihadhari sana nae
 
Tatizo lake lingine mkichat anataka umjibu hapo hapo. Yaani ushikilie simu masaa yote mkiwa mnawasiliana...ikipita robo saa hujamjibu anakasirika humjali, dah alinitesa
Deko hilo.

Tuko wapi achezee makonzi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom