Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 22,854
- 32,657
DadeqqqOperesheni Ivanka....
Hodi kwenye huu uzi wa kimasihara, leo na mimi naomba kutoa mchango wangu kwenye uzi huu kwani nimekuwa msomaji sana wa uzi huu miaka mingi sasa na sitatenda haki kama sitoweka hapa kisa hata kimoja cha tunda kimasihara.
Awali kabla sijaanza kuandika niseme sijawahi kutongoza mwanamke, mara nyingi wanawake ninaokula huwa wanakuwa tayari wenyewe ni wachache sana ambao nilijikuta naanza kuwaomba mapenzi mimi ila wengi walinichokoza wao.
Andiko hili litakuwa na CODE za maeneo na vitu vingine ambavyo vinaweza kubainika kwa uwazi, hivyo nitajaribu kuweka code kwenye maeneo hatarishi kwa sababu naamini huyo mwenzangu niliyemla kimasihara anapenda sana mitandao licha ya kuwa hayupo hapa nchini.
"Tusamehewe kwa tamaa zetu za kimwili"
Ni jioni moja nipo kwenye gari natoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine baada ya kupewa mwaliko wa birthday, huwa sina kasumba ya kuhudhuria sherehe hizi na wala siabudu sherehe aina yoyote. Mwaliko wa kwenda kwenye birthday niliupata kutoka kwa mpenzi wangu Nancy.
"Brighton naomba kaniwakilishe kwenye sherehe ya rafiki yangu Ivanka, mimi kwa sasa siwezi kwenda kwa hali yangu hii" yalikuwa ni maneno ambayo yalikuwa yanasikika kutoka kwenye simu ya Nancy (mpenzi wangu) Hata yeye anajua wazi mimi siyo mtu wa kujichanganya na sipendi kuwa katikati ya kundi kubwa la watu bila sababu yoyote ya msingi na nzito.
Nilitafakari sana na kuamua kwenda mkoa jirani na pale tulipokuwa tunakaa, ilikuwa ni wastani wa kilomita 90 kutoka nilipo hadi kwenye sherehe hiyo (birthday ya Ivanka)
Ivanka nilikutana naye mara mbili kama sikosei ila mara zote hatukuwahi kuingia kwenye maongezi ambayo yangetuweka karibu zaidi, nilikuwa nasalimiana naye pale ambapo Nancy anawasiliana naye kwa njia ya simu.
Majira ya saa 9 alasiri nafika na kupiga simu kwa mwenyeji wangu kuwa nimefika na akanipa maelekezo njia ipi nipite hadi nyumbani. Baada ya muda mfupi nikawa nimefika kwao Ivanka ambaye alikuwa anakaa na Baba yake na Bibi yake mzaa Baba. Ivanka alifurahi sana kufika pale siku ile nami nikafurahi mno kuwepo pale, story na baba yake Ivanka zikanichukua na ghafla ni jioni na maandalizi ya sherehe yakaanza. Sherehe hii ilikuwa inaenda kufanyika kwenye ukumbi mmoja jirani na kwao Ivanka.
Basi baada ya muda nikaitwa ndani na kupewa chakula cha nguvu kisha nikaambiwa nijiandae tunaondoka muda si mrefu, japo sipendi kutoka usiku ila nilijikokota hivyohivyo na tukapanda gari na kuelekea ukumbini. Tumefika nikakutanishwa na waalikwa wengine na wengi wao walikuwa ni wanafunzi wa vyuo.
Sherehe ikaanza Ivanka alipendeza jamani, mpaka uone namsifia ujue alipendeza huwa sina kasumba ya kusifia kila aliyevaa nguo kuwa kapendeza. Kifupi huyu ni mwanamke mrefu, rangi ya kung'aa siyo mweusi wala mweupe, ana umbo jembamba ila lenye kupendekeza machoni kwa kila mwanaume mwenye uwezo wa kupenda.
Ivanka naomba ulaumu gauni lako ulilovaa ile siku kuwa ndilo lilikuponza, mimi siyo wa kuachiwa mapaja nje na kuoneshwa nusu ya matiti (kifua) yaliyosimama na kujaa vyema.
Ndugu wasomaji, Ivanka wakati anafanya sherehe hii alikuwa tayari kachumbiwa na jamaa mmoja kutoka Sweden na alikuwa na pete ya uchumba, hisia zangu zikaanza kusafiri hadi zikafika Sweden nikajiuliza kwahiyo Ivanka akaenda kukazwa Sweden na mzungu? Wanabeba vivutio vya taifa na kupeleka kwao huku wakiacha Taifa likibaki na wakina Chiku, Mwajuma na Mamu!
Sherehe ikaisha na tukapanda gari kurudi nyumbani, wakati tupo kwenye gari nikaendelea kuwa karibu na raia huyu mtarajiwa wa Sweden, tulikaa karibu yeye akiwa tayari kalewa, tumefika nyumbani anajifunga kanga na kuja chumba ambacho nilipaswa kulala na kuanza kunitandikia. "Brighton hiki ni chumba cha ndugu yangu, siyo mtu wa kujali kuhusu usafi naomba ulale na nisamehe kama hujapenda"
Sikuchukulia kama ni suala kubwa sana kwangu maana mimi naweza kulala popote hata juu ya moto ili mradi ufunikwe tu vizuri na shuka. Basi nikalala na asubuhi ikafika, hatimaye mchana na jioni nikarudi kwenye makazi yangu.
Baada ya mwezi nikawa naendelea kuwasiliana naye na nilijisikia furaha sana kukutana na mwanamke ambaye unaweza kuchat naye na usiboreke (kama wewe ni mwanamke wa hivyo basi mimi ni shabiki wako)
Siku moja jioni nikamuuliza unafanya nini? Akanijibu nipo tu shemeji yangu sina chochote nachofanya zaidi ya kuimba na kucheza muziki. Nikapigilia msumari wa inchi 5 kwenye kucheza muziki, nikamuuliza kumbe unajua kucheza na muziki na mbona ile siku hukucheza ama ulikuwa unaogopa watu? Akasema anapenda kucheza ila si mazingira yote anaweza kucheza muziki. Mwanaume nikatumia mbinu za kivita kama ambazo natumia kule Ukraine (angalia avatar) nikaomba kutumiwa kipande kidogo cha video chenye kuonesha akicheza muziki.
Kweli baada ya maridhiano ya amani video ikatumwa na nikaona kwa macho yangu kiuno kikikatwa kwa ustadi mkubwa sana (alikuwa amevaa taiti na kitop) nilipata nafasi ya kuona kitovu na herufi V iliyobanwa vyema zaidi na ile taiti. V ni nzuri acheni tu itumike huko Ukraine kwenye operesheni ya Urusi ila V ni nzuri sana.
Video ile ilikuwa na masharti kuwa isionekane popote kwani Nancy ni rafiki yake wa damu na nisije nikaacha kwenye simu bila kuifuta. Nilivyomaliza kuitazama nikaipeleka kwenye makumbusho yangu (email) hiyo email imetunza siri nyingi na nzito zaidi ya nyaraka za uhuru na muungano zilizopo pale Magogoni.
Baadae nilijikuta nami namtumia kombora langu la hypersonic lililokuwa limesimama wima tayari kwa oparesheni yoyote ile. Kombora hili lisilozuilika kwa namna yoyote lilienda kuharibu mfumo wake mzima wa kiulinzi na akaomba tukutane ili kumaliza huu mzozo kabla hajapata hasara kwenye miundombinu yake ambayo ilikuwa inapelekwa Sweden muda si mrefu.
Basi tukaendelea kuwasiliana kwa ahadi kuwa siku moja tutaonana. Siku moja Nancy ananiambia anataka kwenda kumsalimia Ivanka na kama naweza twende wote kwake. Kutokana na uchokozi wa wanajeshi wake kwangu nikaona lazima niende kwa Ivanka nikiwa na Nancy na tutajua huko huko mbele ya safari nini kifanyike.
Ivanka amemchokoza Putin na sasa Putin anaenda kumpiga kwake (Kiev) mbele ya Nato (Nancy) na washirika wake wa karibu.
Usikose sehemu ya pili ya Operesheni Ivanka.
.................... Itaendeleza...................




