Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,718
- 6,979
YESU KRISTO alikuja duniani kwa ajili ya wale waliopotea na siyo kwa ajili ya wenye haki.We umekuja kufanya nini huku kwenye huu uzi
Na mimi nimeingia kwenye huu uzi kwa ajili ya kuwahubiria ninyi "wazinzi" na "waasherati" habari Njema ya Ufalme wa MUNGU.
BABA MUNGU anawapenda sana na ndiyo maana alimtoa Mwanae YESU KRISTO afe kifo cha aibu na mateso kwa ajili yenu ninyi. MUNGU anawapenda sana, wala hawachukii. Mnachotakiwa kufanya ni kubadilisha tu mitazamo yenu na kuacha uchafu huu na kuwa WATIIFU kwake.
MUNGU anataka kuwapa ninyi wazinzi na waasherati ufalme wake wa mbinguni lakini hawezi kuwapa ikiwa hamtaacha tabia zenu chafu.
Jamani, ikimbieni zinaa maana wazinzi na waasherati hawatauona kamwe ufalme wa MUNGU. Lakini mkitubu na kuacha hakika mtasamehewa kabisa na kukaribishwa kwenye ufalme wa MUNGU.

