Ulipata changamoto gani katika kumtambulisha mwenza katika familia yako?

Gustavo Gaviria

JF-Expert Member
Nov 19, 2018
630
1,109
Wakuu tupo pamoja.

Mimi hapa nina mwanamke mmoja bwana ana mtoto mmoja ila sio wangu nataka kumuoa, nimeridhia kabisa na nimempenda mwanamke licha ya kuwa na mtoto, ila kipengele kinakuja kwenye familia sidhani kama watanielewa! na hata kama watanielewa sidhani kama watatoa ushirikiano ipasavyo...navyoona wataniona bwege la kutupwa kulingana na uchaguzi wangu...yaani naona uchumba hapo ndio kizingiti kilipo na utafia hapo! hapa nawaza tu nimwambie mchumba aendelee na maisha yake nisimpotezee muda au nikaushe tu, tatizo ninampenda sitaki kabisa kuachana naye.

Nikimwambia ugumu utakaokuwepo nahisi ndio itakuwa mwisho wa mahusiano na mimi bado namhitaji...haya nikisema kumwambia baadae nitakuwa nimempotezea muda, yaani ni kizunguzungu, ninachojua familia yangu haitopendezwa kabisa mimi kuoa mwanamke aliye na mtoto wa mtu mwingine, ila mimi ndio nimeshampenda.

haya endapo nikimwambia kuwa hilo suala la yeye kuwa na mtoto tulifiche, itakuwa sio rahisi maana kutakuwa na muingiliano wa familia na itajulikana tu.

Je Mwanamke au Mwanaume ni changamoto gani ulipitia katika kumtambulisha Mwenza wako katika familia yako yaani baba mama na ndugu zako?

Tiririka kisa chako tupate uzoefu, naamini sio mimi tu niliyepo katika hili.
 
Kwanza hauna msimamo yaani ni zero kabisa.naamini mwanaume Kama mwanaume hajachaguliwi mwanamke ambaye hajampenda labda awe anampenda.usimpotezee dada wa watu mda wako.
 
Acha kabisa mkuu tuliobahatika kuwa na madada wengi na mashangazi ni changamoto kubwa mno,nilimpenda fupi nyundo wangu mmoja aisee ni shida,mi binafsi nawapenda wanawake wafupi huwa naamini hata kina ya ile kitu ni fupi.

Sasa basi akaja msibani yaani alitolewa kasoro mtoto wa watu,eti ninaulizwa mfuko wa simenti na yeye kipi kirefu,kuna muda nilikua simuoni na simu haipatikani kumuulizia yuko wapi nikaambiwa nimuangalie nyuma ya jiko la gesi.

Ila nipo nadunda nae na ana akili ya maisha hadi basi ukijumlisha na anavyoifinyiaga kwa ndani basi tuuu
 
Kaka yangu alimpachika mimba kwanza akazaa mtoto kisha akampeleka nyumbani kwa wazazi akiambatana na mwanae aliyemkuta, japo ilileta maneno kiasi lakini alikubalika kwa urahisi zaidi kuliko ambavyo asingezaa nae kwanza
 
Sikiliza moyo wako kijana kama unaona anafaa basi tafuta ushawishi hili kuongea na wazee wako
 
Back
Top Bottom