Uliona wapi mwanaume anajipeleka gerezani?

Hii ishu ya chadema Jana na leo! Kuna Memba wapya zaidi ya 100 Wamejiunga kuongea pumba kuhusu chadema. sijui, VGL, KUZOU etc
 
Natumaini wewe mleta hii mada huo mgahawa uliokwenda ni pale msikiti mkuu wa hapa Arusha kuna wale wanaume wanofugwa na wake zao mchana kutwa ni kushiNdia kahawa na kutaka kujua fulani kala nini au fulani kavaa nini ndio hapa ulipopata huo umbea! NENDA KAMUULIZE ALIYEKUTUMA ULIONA WAPI MWANAMUME MTU MZIMA TENA BABA WA NYUMBANI LAKINI HAJUA KWANINI FAMILIA YAKE NI MASIKINI!
 
Eti niliingia kwenye mgahawa mmoja mjini,eti nikawakuta watu wanajadili kuhusu Lema,eti watu wanaojipeleka gerezani,eti mzee mmoja akasema,anachezea serikali legelege ya jk,eti wanasema alitaka akadake posho za bunge eti eti! Wewe unafikiria nn?acheni majungu na umbea
Hao walikuwa wanatoa maoni yao, si ndiyo inayoitwa people's power hiyo?
 
Hao walikuwa wanatoa maoni yao, si ndiyo inayoitwa people's power hiyo?

Muandika post hajui hata Historia ya "Wanaume Halisi" huko kusini mwa Africa wakiongozwa na Rholilala Madikizela Madiba (Nelson Mandela), Govan Mbeki, Walter Sisulu, Ahmed kathrada na vijana wa ANC youth league walipoongoza kampeni iliyoitwa "Defiance Campain" mwaka 1953, ambapo walikuwa wanajipeleka kwa makusudi ktk vituo vya polisi bila "pass" katika kupinga pass law kwa watu weusi nchini humo....
 
Jamani hata Yesu alijipeleka mwenyewe kwa wayahudi wakamkamata na kumhukumu hivyo ndivyo ilivyo, tumechoka na viongozi wanafiki kwa wananchi wao, sasa hivi sukari imepanda sana bei hao wabunge wetu wako wapi? shilingi imeshuka mpaka 1800 kwa dola moja hao wabunge wako wapi kama sio wanafiki? Ili kukomboa watu ni lazima ujitoe kisawasawa, bila kujitoa huwezi kuleta mabadiliko ktk nchi hii na ndo maana CCM haitaweza kwa sababu wabunge na viongozi wao wameshindwa kujikana na kujitoa muhanga kututetea sasa si unaona bei za vitu zinapanda wao wako kimya na matokeo sisi wananchi ndo tunaumia hapa, wao wanakamua posho tu na kugonga meza na kupiga makofi na vigelegele.
 
Alienda kuonana na vijana wenzake waliop gerezani, mwache akae kidogo, ajuwe kuwa kuna Serikali na ina mkono mrefu, natamani angejipeleka Dar ningekwenda kumtembelea.
 
Back
Top Bottom