Wapendanao ni binadamu kama ambavyo wasiopendana walivyo......nao pia wana mioyo ya nyama na hawawezi kuwa perfect 100%. Kama ambavyo baba huweza kumkosea mwanae, mpenzi pia aweza kumkosea mwenzie.... Kwa mantiki hii walio katika mapenzi nao pia huanguka na kujikuta wanacheat........... Sasa ODM akimmega Eliza, haimaanishi mapenzi yake kwa mama Matesha ndo yameisha. Na ndio maana kama yakitokea haya hufanyika kwa siri kubwa sasa, si hadharani au kumwonyesha mwenzi wake kama ulivyotaka kutuchakachua hapo juu.....Ukisema walitamaniana unakosea Babu sema huyu alimtamani kwa sababu anayefanya unyama huu ni mwenzi mmoja dhidi ya mwingine.
Swali langu sasa kabla hujaondoka na ninaomba jibu la mwisho sitakuuliza tena; ODM anapocheat na Amanda muhudumu wa Bar, au Sophia Secretari wake tunawezasema nakuna penzi la dhati hapo kwa Mama ODM au?
Na unaposema kuwa mwenye kufanya hayo hakuwa na mapenzi ya kweli ina maana inakuwa imekula kwake yeye aliyeolewa/oa mtu wa aina hii lakini akawa na penzi la dhati au haiwezekani mwenye penzi la dhati akakutana na aso penzi la dhati? na je ndoa yenye penzi la aina hii utaiitaje??
Wapendanao ni binadamu kama ambavyo wasiopendana walivyo......nao pia wana mioyo ya nyama na hawawezi kuwa perfect 100%. Kama ambavyo baba huweza kumkosea mwanae, mpenzi pia aweza kumkosea mwenzie.... Kwa mantiki hii walio katika mapenzi nao pia huanguka na kujikuta wanacheat........... Sasa ODM akimmega Eliza, haimaanishi mapenzi yake kwa mama Matesha ndo yameisha. Na ndio maana kama yakitokea haya hufanyika kwa siri kubwa sasa, si hadharani au kumwonyesha mwenzi wake kama ulivyotaka kutuchakachua hapo juu.....
Yes, kuna uwezekano mkubwa wa mwenye penzi la kweli akaolewa/oa na aliyemtamani. Hii ni mateso kwa mwenye mapenzi ya kweli. Ukisikia mmoja katika ndoa anataabika kwa manyanyaso na bado anang'ang'ania japokuwa ana uwezo wa kuanza mbele na maisha yake ujue mapenzi hayo ni ya dhati kwa upande mmoja.......... Lakini ukasikia "babue, usinletee za kuleta kama vipi nigaie talaka yangu niende kwetu" afu hata kabla hajamaliza sentensi talaka tatu zishachomekwa kwenye sidiria, ujue hapo hakukuwa na mapenzi ya kweli..... kutamaniana tu.....
Ndoa zenye aina hii ya mmoja mwenye mapenzi ya kweli na mwingine msanii naweza kuziita "ndoa za kifo"..... "mguu ndani mguu nje"
Bado niko hapa kama bado una swali nyoosha kidole juu.
Hahahahh njoo bwana usiondoke. Sasa ndio mdahalo unaanza hebu njoo bana amah!! wengi tunavitamanis ana vionjo hivyo vya kizamani Mbu na ni wengi kama si wote tungetamani kuishi maisha hayo ya kizamani kwani ndio ya ukweli zaidi. Ila sasa anachoongelea ODM hapa ni hali halisi ya maisha ya ndani ha hii Global village ya sasa hivi! Ambayo unawezalinda na kulinda kama unavyoweza kulinda na bado mwishowe ukaangukia pua vile vile (unless mkutane wote ni wa enzi hizo za old fashion penzi). Lakini kwa maisha ya ulimwengu wa sasa ambao Mbu unakutana na ODM kwenye viti virefu kila mara akikucheka kwa kukazania penzi la MwanajamiiOne kama vile umelishwa limbwata ni wazi kuwa ni wachache watakaokuwa na uwezo wa kuruka vihunzi vya ODM. Maana siku hizi mwanaume mwaminifu kwa mwenzi wake anaonekana ni Old fashioned, mshamba, dhaifu, kakolezwa, kawekwa kiganjani and all the bad images ambazo zinawezaua ego yake mbele ya wenzake................changanya na vishawishi vya watotot wazuri wanaozaliwa kila siku tena wenye stadi kali za maisha ikiwemo kutongoza mwanaume mtu mzima.............................utajikuta tu unacheat huku ukijiliwaza kuwa mara moja tu haiumiza unasahau kuwa kuna kunogewa. So kwa staili hii hata mwanajamiione mie nikikaa mlangoni na panga, upinde au bunduki kulilinda penzi letu bado itakula kwangu hahahahahah
(nirudishieni password yangu wapenzi kabla sijapewa talaka humu)
Hahahahhahah Babu bwana, nimesema hawana aibu kwa wenzi wao loh.... wanajua kuwa mwenzi anajua kuwa anacheat na bado anacheat si hana aibu wala haoni vibaya??
Hilo ningeomba upate ushahidi humu humu ndani, wapo wanaowaletea wenzi wao mahawara, wakawashusha kwenye matrimonial beds na kuwalaza sakafuni au kwenye vyumba vya watoto! Hujawahisikia? kuna wanaume washenzi babu! Usiri unaouzungumzia nao pia unategemea unatafsiri vipi maana kama ni siri kwa mke/mume wakati rafiki yako ambaye ni shemeji wa mwenzi wako anajua hii si siri Babu yangu.
kulinda utalinda lakini hautafanikiwa.....!
hata hivyo sijawahi kuona watu wakifanikiwa ''kuyalinda'' haya mapenzi....!mifano tunayo wajameni.tuwe realistic kidogo au vipi mazee?!
tunaona wake za watu wakishughulishwa mahoteli makubwa hapo dar nyakati za asubuhi na mchana...wakirudi makwao wanasoma biblia....
tunajiona sisi wenyewe wanaume tunavyoshindwa kuheshimu ndoa zetu kwa kuwa na vimada huko nje....na jioni tunarudi kuwakumbatia wake zetu as if ''nothing happened''
mimi nadhani kuna vitu ''basics'' vya kufanya ili:
-tuziheshimu ndoa zetu
-tuheshimu miili yetu
-tuheshimu afya za wenzi wetu
-tuwaonee huruma tuliowaleta duniani
sasa hayo mambo tajwa hapo juu yakifanyika utajikuta ''automatically'' unalinda hilo penzi!...sasa hayo mambo unayafanyeje hiyo ni topic kubwa sana basing on perceptions za ''imani''
kinyume na hilo my friends tutakuwa tunachangamsha jamvi!
Aksante Teamo hapa umemaliza kila kitu...............unajua mnachokichanganya wewe na ODM ni nini? hapo kwenye nyekundu hapo, mwenyewe unasema ukizifanya hizo basics utajikuta UNALINDA hilo penzi aotomatically...........na ndicho tunachokisema pia sisi. so kwa maelezo yako hapa unakubali kuwa kwa kufuata hizo basics, autonmatically unalilinda penzi si ndio? au leo magugu maji yametanda kichwani mwangu
....lol....umenirudisha kwa post hii,
...ama kwa style hii, acha tu mie old fashioned niendelee kuonekana zumbukuu ulimwengu upo huku,
nijibanze na old fashioned mwenzangu iwapo tu naye atakuwa anapuuzia kasi ya mabadilikoyamapenzi.com
hivi afrodenzi hili swali lake angeuliza; unajilinda vipi kwenye mapenzi
ili kuepukana na kuachana/talaka, majibu yangekuwa haya haya?
Teamo kwa kusema hayo na hayo uliyoyaorodhesha ninaomba kufunguliwa mlango upande wako na kuingia kwenu. Mimi wakati najadili hapa sikuwa nimeyafikiria hayo engine, na ndi maana kama utasoma vizuri posts zangu nasisitiza kwenye yale yanayokubalika ambayo wewe na babu ODM mnayaita "Basics".mimi nashindana na wewe emjeiwani kwenye kulinda hilo penzi kwakuwa naamini kuna vitu wanawake wanafanya wakiamini ndo wanalinda penzi....!WAO WANADHANI WANALINDA KUMBE WANAHARIBU KABISA...!kwa mfano:
-kupekua pekua inbox (mails na simu)ya mwanaume.
-kumtambulisha tambulisha mwanaume kwa videmdem sijui vinani (kwamba wataogopa)
-kuacha viatu kwenye gari
-kuacha vipodozi
-kumkagua kagua mwanaume kila akirudi home (wengine wanamkamua hata 'paipu' kuona kama kuna masalia ya tui)
-kumpigia pigia simu za kumwahisha kurudi hm mwanaume wakati anajua yupo baaa...
-na upuuzi mwingine wote
hivi vitu ndo wakinamama wanadhani wakifanya wanalinda penzi.....!
tuwe wakweli wajameni......!huko ni kudanganyana
Uchune bana! kuna kadada nataka kukaimpress hapa JF , ndo maana nimeandika hako kapost.Klorokwini ukiwa hujalewa unaongea points. Safi sana.

Uchune bana! kuna kadada nataka kukaimpress hapa JF , ndo maana nimeandika hako kapost.

wewe si umenipiga kibuti.

am off!
shemeji bwana!! Mikwara mingi kama mcheza mieleka! Aksante kwa ufafanuzi huu, naungana nawe kichwa, mabega na mikono!Naomba nipingane na wote mlochangia kwenye hii sredi. Mkiona nimekuvunjieni heshima kashtakini kwa Invizibo.

Huu mjadala una mitazamo miwili tofauti kwa maoni yangu na katu hauwezi kuwa sahihi kwa kuuangalia kwa mtazamo mmoja, Penzi linalindwa at the same time Penzi halilindwi (kiswahili kigumu lakini mtanielewa mbele ya safari)

1) PENZI LINALINDWA:

Kumbukeni sisi ni binadamu na tuna madhaifu yetu ambayo kama tukiyapa nafasi kututawala au kuwatawala wenza wetu basi tutakuwa tunalizembea penzi hata kama liwe madhubuti vipi.

Ufafanuzi: Mfano mwanaume ana udhaifu wa tamaa na mwanamke ana udhaifu wa kupenda attention au kupenda kwa mazowea, ni vyema ukamlinda mwenzio ili asiteleze kwa kumwelewesha kukaa mbali na vishawishi ambavyo vinaweza vikapenya kwenye udhaifu wake na kuharibu penzi, haiwezekani mwanamme amruhusu mke wake akalale na marafiki wa kiume eti tu kwasababu anamuamini au mwanamke kumuacha mume wake ajiexpose kwenye vishawishi au mitego ya starehe eti kwasababu tu penzi halilindwi. (Hapa unalinda ili mwenza au wewe mwenyewe usije ukateleza na ukaliathiri pendo na mtiririko wake)

Conclusion: Penzi linalindwa ili lisiingie doa kwa kuzingatia weakness ya mtu/jinsia, mazingira na kwenye wajibu (hapa inaingia kunogesha/kukoleza penzi)

2)PENZI HALILINDWI: hii inabase zaidi kwenye hisia, hisia za mapenzi hazilindwi na wala hazifuatiliwi wala kubadilishwa kirahisi. Yoyote mwenye hisia za mapenzi za kweli anaweza akatawaliwa na tamaa tu lakini moyo utabaki kwa anaempenda na hili halina ubishi. Lakini kumbuka kwamba mtu huyu inabidi alindwe ili asiteleze na akalitia doa pendo, kwa vile mtendwa siku zote hajui moyo wa mtenda kama umebeba penzi la dhati au la usanii, hivyo hata penzi la dhati lina nafasi kubwa ya kuparaganyika kama halijalindwa (refer to Penzi linalindwa, above).

Nimeandika haraka haraka kwavile hapa Igunga internet cafe hawaruhusu ukae zaidi ya dakika 10, hivyo kama hamjanielewe nitakuja kufafanua sku jirani yangu mwenye laptop akilejea holidei.

Nisiulizwe masuali kwa vile sitokuwa hewani.

Kwaherini!
Naomba nipingane na wote mlochangia kwenye hii sredi. Mkiona nimekuvunjieni heshima kashtakini kwa Invizibo.

mimi ninajitahidi ucku na mchana kutafuta hela za kulipia bill za maisha,...mimi ni mwanaume na najua for sure ukiwa huna hela hakuna mapenzi siku hizi,..na hili ni kwa upande wangu

asanteeni...Igwe

mkuu Igwe hapo umenena kama mwanaume haswaaaaaa,ndo maana wahenga walisema 'penye udhia tia rupia' ukimuuzi mama we mtwange upande wa khanga then ugomvi kushne!