Penzi la Wizi: Afrodenzi anajifanya anampenda Rejao kwa sababu Rejao ana mafweza kaba Rostam...... wizi mtupu
Penzi la Huruma: Afrodenzi anamkubali Rejao kwakuwa Rejao kamtongoza yapata miaka mitano sasa......
King'ang'anizi: Rejao anampenda na kumng;ang;ania Afrodenzi kwa kuwa alipoonjeshwa mara ya kwanza, hajawahi pata mtaalam kitandani kama huyu, na tena mle ndani kuna joto la kutisha..... anan'angania mpaka kieleweke....
Kutamani: Afrodenzi anamzimikia Rejao kwakuwa Rejao ni handsome ana mwili ulojengeka kimazoezi, anapiga pamba za kufa mtu na vitu kama
hivyo
Penzi la kweli halina hiyo makitu.......... Ndo pale unamkuta mtu kaoa jimama minyama uzembe watu wakibaki kujiuliza "kampendea nini yule shankupe?" na wala wapenzi hawa wasisikie kisemwacho.
Au binti wa kitajiri anaanguka kwa sakara ODM, haambiwi wala hasikii kitu watu wakibaki kubishana "ODM lazima atakuwa mchawi"
Sijui niendelee?
Kitu nilichokisoma humu ndani ni kuwa penzi la kweli halipotei, haliibiwi, haligawanyiki hata siku moja. Likiibiwa, potea, gawanywa halikuwa penzi la kweli!. Wanaume wenye wenzi wao; wanawake wenye wenzi wao wanaowapenda kwa dhati - wanapocheat nje huwa si kuwa penzi lao la kweli limekufa la hasha bali ni matamanio tu but penzi la kweli bado liko kwa wenzi wao... ni kuwa wamechoka kula nyama tu kila siku sasa wanatafuta ladha nyingine lakini haimaanishi wamechukia nyama kimoja.
kwa wale ambao wanatekwa kabisa na nyumba ndogo/ serengeti na kuwaacha wapenzi wao basi ni kwamba kwao hawakuwa wamepata penzi la kweli. So penzi la kweli linalead the way
Reference: Babu ODM.
(Babu uniambie kama nimefaulu somo lako tafadhali; na Grade niijuie)
...dossshhhhh!
yaani baada ya kumsoma tena mzee ODM na kuirudia post ya mwanajamiione ndio nimepata mwanga sasa
mnatafsiri nini hapa....daaaahhhh....
ama kweli, mapenzi ni zaidi ninavyoyatafsiri aisee...pheewwwww!
kwa mtaji huu, afrodenzi naomba kujitoa kwenye mdahalo huu bana...
mwenzenu bado old fashioned kikwelikweli, i mean nikishapenda sitaki kusikia
hizo excuses za 'mafiga matatu'...iwe kwa mwanaume au mwanamke.
Mbu umeongeza furaha kwenye siku yangu ya leo kwa huu mtazamo wako..."kumuonyesha" sio neno sahihi kwenye mapenzi, naamini kwenye mapenzi ni kutimiza wajibu wako aka -kufanya/kumfanyia/kufanyiana-,...mpenzi/mke au mume atayapokea kwa muonekanoi wake. kumuonyesha ni kama una pretend hivi, ambayo utapochoka ndio yataanza yale ya..."mbona siku hizi umebadilika, hunifanyii hili na lile...!"
Aisee Moskwito, nrudishie Mjukuu wangu Mtiifu. Tafazali usinizeeshee akingali bado mwali.
How do you protect your love ?
Je unalinda vipi upendo(penzi)??
Je tuki linda penzi hii itasaidia ku imarisha uhusiano kati ya wapendanao au ku
punguza talaka au kutengana ??
asanteeni AD..
Kwa umri huu, jembe siwezi kamata tena, ngoja niwape wajukuu zangu hazina ya mapenzi iliyosalia......... Tatizo vijana wabishi wanasahau mapenzi hayafundishi darasani wala hayahitaji ushauri. Mapenzi yanaflow nachurale......
Yangekuwa yanafundishika, tusingesikia talaka wala kubamizana vyumbani humo. Na hapa JF Maushauri ya Mbu, AshaDii, MwanajamiiOne na wengine tusingeona kila siku masredi mapya yakifunguliwa kila siku ya watu wakiomba ushauri wa kulind ndoa zao.... wangefungua posts zao na kwenda kuyafanyia kazi.......
Mkuu naona hawa wajukuu wanachanganya mambo mawili makubwa....Umuhimu wa kunogesha/kukoleza penzi Vs kulinda penzi!!
Hilo la kwanza ni muhimu sana na kuna mbinu nyingi ambazo tumezizungumzia sana hapa JF...ikiwemo kubadili mboga na usanii mwingine
Kwa upande wa hilo suala la pili...Ni kosa kubwa (close to suicide) kufanya attemps za kulinda mapenzi...Hivi mtu utatumia silaa gani???
Mbu anachokisema Babu ODM hapo ni kuwa mwenye cheating ni hulka ya binadamu (tena kuna sehemu nimesoma kuwa kwa mwanamke ni kubwa zaidi ya kwa mwanaume!!). Wenye uwezo wa kujizuia wana utashi, aibu na staha kwa wenzi na jamii na hawa si wengi sana. lakini wanaocheat si kuwa hawana mapenzi ya kweli bali ni wale walioshindwa kuzizuia tamaa zao na hawana aibu kwa wenzi wao na wanajifanya manunda kwa kuwaumiza wenzi wao hisia!
(Babu desa ulilonipa linaishia, usipoingilia kati hapa nakugeuka narudi kwa Mbuuuu)
silaha pesa,kisu mzigo
Hahaha!!! Leo utakuwa umetokea Msasanisilaha pesa,kisu mzigo
pesa kiasi gani inayolinda penzi?
Hahaha!!! Leo utakuwa umetokea Msasani
...dossshhhhh!
yaani baada ya kumsoma tena mzee ODM na kuirudia post ya mwanajamiione ndio nimepata mwanga sasa
mnatafsiri nini hapa....daaaahhhh....
ama kweli, mapenzi ni zaidi ninavyoyatafsiri aisee...pheewwwww!
kwa mtaji huu, afrodenzi naomba kujitoa kwenye mdahalo huu bana...
mwenzenu bado old fashioned kikwelikweli, i mean nikishapenda sitaki kusikia
hizo excuses za 'mafiga matatu'...iwe kwa mwanaume au mwanamke.
Unanogesha na kukoleza ili iweje?