Ulinganifu wa vita kati ya USA na Iraq dhidi ya vita kati ya Urusi na Ukraine

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,154
33,367
Vita hizi zote zinaitwa operation.

USA waliita operation desert storm.

Urusi waniita operation maalumu.

USA wakisema Iraq Ina silaha za maangamizi WMD hivyo inyang'anywe.

Urusi wanataka Ukraine isijiunge na NATO,kwa vile Ukraine kakataa ombi la Urusi la kutojiunga NATO Urusi kaona basi avunje nguvu ya uwezo wa kijeshi wa Ukraine.

USA kabla ya kuipiga Iraq alihakikisha kwanza anapata taarifa zote muhimu za maeneo ya kijeshi,silaha na nguvu ya jeshi la Iraq.
Alitumia ujanja wa kuwatumia wachunguzi wa umoja wa mataifa kupitia shirika la atomic Dunia lililokua linaongozwa Mohamed El baradei.

Kwa kuchomeka wataalamu wa atomic waliokua wanaipa taarifa USA kwa Siri. Viongozi wa timu za ukaguzi wa silaha za maangamizi walikua ni Josef Butler ambae baadae alikataliwa na Iraq kwa kushukiwa kuifanyia ujasusi USA,ndipo akaletwa mwingine bwana Hans Brix. Ukweli Hawa waliisaidia sana USA kujua Siri za jeshi la Iraq maana timu ilikua inapita Kambi zote za jeshi la Iraq kukagua WMD.

Urusi imetumia muda mwingi kuishawishi Ukraine isijiunge na NATO ili ibaki kuwa taifa lisilofungamana upande wowote. Urusi imejaribu kuishawishi USA ili NATO isizidi kuisogelea hasa kupitia Ukraine,lakini wapi. Urusi imajaribu kuzishawishi nchi za ulaya kuhusu kutanuka kwa NATO kuelekea upande wake lakini haikusikilizwa. USA ilipoona imeijua vizuri Iraq kupitia wachunguzi wa silaha za maangamizi wa UN ikaanzisha mashambulizi.

Hata hivyo USA haikuenda Iraq peke yake, ilikwenda na nchi karibu zote za NATO kasoro Ufaransa na nchi chache kwenda kuipiga Iraq iloyopelelezwa na UN na ikiwa imewekewa vikwazo.

Sio tu nchi za ulaya Bali pia kulikua na nchia za kiarabu na mataifa mengine kwenda kuipiga Iraq.Na kuhakikisha Iraq haipati msaada wowote kutoka popote Duniani.

Kinyume na USA,Urusi umeamua kuipiga Ukraine,lakini Urusi imekwenda peke yake.

Sasa Cha ajabu,
NATO wote wanampa msaada Ukraine.

West wote wamemuwekea Urusi vikwazo vingi sana tokea Dunia hii kuumbwa.

USA na west wenzake wanasema Urusi imetengwa na Dunia nzima, lakini nchi zinalazimishwa kuitenga, hata kama hazina shida na Urusi,vikwazo vyenyewe sio vya UN ni vya west.

Ugomvi wa west na Urusi wanalazimisha Dunia nzima imwekee ukwazo na imtenge. Utakuta nchi nyingine kufanya biashara na Urusi ndio uchumi wao unategemea lakini wanalazimishwa waiwekee vikwazo.

USA ailipigana na Iraq akiwa na washirika wake,wakati Iraq ikiwa peke yake, lakini iliwachukua zaidi ya mwezi kumuangusha Sadam.

Urusi inapigana na Ukraine nchi yenye Nguvu ya kijeshi mara Tano ya Iraq Ile na Huku ukipata mafunzo na silaha Bora kabisa, ushauri,mbinu, nguvu ya mawaziliano ujasusi wa kiraia na kijeshi kutoka NATO, Wakati Urusi inapigana peke yake.

NATO wote wanatangaza kupeleka misaada ya silaha na fedha Ukraine,lakini hawataki kusikia Urusi inasaidiwa na nchi yoyote.ingawa Urusi hahitaji msaada wowote.


Vyombo vya habari vyote vikubwa ni vya west,
Na lugha kubwa inayoeleweka Dunia nzima English ni ya west.

Vita ni vita wamarekani wengi walikufa Iraq na WA iraq kwa maelfu nao walikufa.

Vita ni vita,Warusi wanakufa Ukraine,na WA Ukraine wanakufa.
Wanajeshi wa Urusi wakipungukiwa kitu ktk uwanja wa mapambano hiyo ni habari,
Lakini wamarekani wakiomba kusaidiwa na mataifa rafiki zake hao ni Allies na hiyo sio habari.
 
Paragraph chache za mwanzo umegundulika kuwa pro-Putin hamna haja ya kujisumbua kusoma andiko lote, Urusi imedhihirisha udhaifu mkubwa sana kwenye huu ugomvi na inaenda kuwa ulimwengu wa tatu.
 
Paragraph chache za mwanzo umegundulika kuwa pro-Putin hamna haja ya kujisumbua kusoma andiko lote, Urusi imedhihirisha udhaifu mkubwa sana kwenye huu ugomvi na inaenda kuwa ulimwengu wa tatu.
Kwa ki paragraph chako hiki kifupi umedhibirisha wewe ni pro west.
All western European + USA = called themselves NATO wamedhihirika kuwa ni dhaifu na waoga mno dhidi ya Might Russia.
Kumbe size Yao ni akina Iraq na Libya TU,maana hata watalaban wamewashindwa.poor NATO.
 
Kwa ki paragraph chako hiki kifupi umedhibirisha wewe ni pro west.
All western European + USA = called themselves NATO wamedhihirika kuwa ni dhaifu na waoga mno dhidi ya Might Russia.
Kumbe size Yao ni akina Iraq na Libya TU,maana hata watalaban wamewashindwa.poor NATO.

Guseni kataifa kokote ka NATO ndio uje useme, sasa kataifa kama Ukraine nje ya NATO kametoa Urusi makamasi yote sembuse NATO yenyewe, ambayo humo ina baadhi ya mataifa yenye uwezo kuizidi hiyo Ukraine mara mia.
 
Vita ya kwanza ya Ghuba kumtoa Saddam Kuwait iliitwa Desert Storm chini ya George Bush Sr, Vita ya pili iliitwa Operation Iraq Freedom chini ya George Bush Jr.
 
Back
Top Bottom