Ulimwengu wa wanyama (Mongoose)

Ulimwengu wa wanyama (Mongoose)

Hivi hawa si ndo nguchiro?, mara ya kwanza nawaona hao wapuuzi, ilikuwa morogoro. Naendesha baiskeli, mara nikaona kundi la wadudu kama panya wanakimbia. Kidogo waka simama mbele wakasimamia miguu. Nilihisi nimeona mashetani. Ilikuwa nipo speed ila baiskeli iliweza lala chini, nikarudi nilipotoka
Kidogo waka simama mbele wakasimamia miguu. Nilihisi nimeona mashetani.😀😀😀
 
Wangekua na vidole vitano wangekua sawa na wale binadamu wanaogawa mali zao nje kila kukicha..
 
Kuna documentary moja niliona kama hawa vile kama sijasahau jinsi wanavyokula nyoka kama wanakula maembe, ni wakorofi nao kwenye mambo kama hayo, nyoka unamuonea huruma.
 
Hawa mbona kama sio herbivores
Mtoa uzi hajasema herbivores. Mbona binadamu tunakula majani? Hao ni omnivores - hula vitu mchanganyiko. Hao waheshimiwa hula majani, wadudu e.g. mchwa, funza wa kwenye mbolea esp. ya ng'ombe, nyoka na mayai ya ndege n.k n.k Mbwa hana ujanja mbele yao. lazima agute.
 
Hawa ukimuona mmoja mbele ujue wazi anasoma ramani hapo utakuta kuna ukoo mzima umejificha kwenye machaka unasubiri amri ya usalama kutoka kwa kiongozi mkuu aka Geordavie wao ili wasonge mbele
 
Hawa ukimuona mmoja mbele ujue wazi anasoma ramani hapo utakuta kuna ukoo mzima umejificha kwenye machaka unasubiri amri ya usalama kutoka kwa kiongozi mkuu aka Geordavie wao ili wasonge mbele
Wana nidhamu ya hali ya juu sana. Mbwa akijaribu kuwafuata, humchen'njia na wote pamoja humwendea kama wimbi- mbwa lazima arudi fasta huku mkia katikati ya miguu.
 
Back
Top Bottom