Ulimwengu wa roho ni timilifu

Mkuu laana vjicho hasad zote zinaondoka na wewe ukabaki salama na kizazi chako kama utakuwa mtu wa maombi na kutoa sadaka.

Sadaka zina masharti sio vitu vya kubakia au visivotosha.
Sadaka inanuiliwa wakati wa kuitoa ili ifike sehemu sahihi.

Sadaka inatengeneza mfumo mzima wa maisha yako nakizazi chako.
 
Nielewavyo mimi, injini ya uhai ni Roho na injini ya matendo, hisia, kumbukumbu, tabia na kadhalika ni NAFSI, mwili ni sehemu ambayo Roho na NAFSI ndo makao yake, MOYO ni utashi

Nipo tayari kukosolewa, nimeeleza navyoelewa mimi
Hapo kwenye Moyo Ni utashi sikubaliani.moyo Ni kiungo tu Kama viongo mwili kazi yake Ni ku-supply damu mwilini kupitia auricle na ventricle,Mambo ya cjui utashi Wala hauhusiani
 
Maisha yetu huwa yanasimamiwa na mikataba ya kiroho(maagano) ambayo either ilifanywa kati mababu, wazazi wetu au sisi wenyewe na miungu.
Viwango vya maisha vinafungwa kwenye mikataba hiyo na ndo maana level ya hali ya maisha inafanana sana kwenye familia au ukoo au hata kabila.
Mikataba hii inadumu hadi kizazi cha nne otherwise ujue jinsi ya kuifunja na kuingia mkataba mpya na Mungu Mwenye nguvu (Creator of universe)
Imani tu hizi hazina ukweli wowote
 
Asante mshana jr kwa kututoa tongotongo. Niukweli kabisa usiopingika kwa ulichoandika, na nimaswali ambayo wanatheologia huyakwepa sana kwan mm nilishawai kuuliza swali hilo kasisi mmoja ila sikuambulia kitu zaid ya kuniambia yakua mambo mengine ni dogma.

Ila mshana ninaomba unieleweshe zaid juu ya hili je tufanye nn sasa kama mchoro wako upo tiyari. Je kulsla makanisani kushinda misikitin, kwenda kwa waganga, na mizimu ni utupu kama mtume paulo alivosema??? Nisaidie tafadhali
 
Naomba utafute hili andiko... Liao Fan's four lessons.. YOU CAN CHANGE YOUR DESTINE
Asante mshana jr kwa kututoa tongotongo. Niukweli kabisa usiopingika kwa ulichoandika, na nimaswali ambayo wanatheologia huyakwepa sana kwan mm nilishawai kuuliza swali hilo kasisi mmoja ila sikuambulia kitu zaid ya kuniambia yakua mambo mengine ni dogma.

Ila mshana ninaomba unieleweshe zaid juu ya hili je tufanye nn sasa kama mchoro wako upo tiyari. Je kulsla makanisani kushinda misikitin, kwenda kwa waganga, na mizimu ni utupu kama mtume paulo alivosema??? Nisaidie tafadhali
 
Kuna watu wanaamini ukifa unazaliwa mara nyingine tena..unaweza kuzaliwa mtu yuleyule na sura ileile au kiumbe kingine. Wanadai maisha uliyoishi ndo yana-determine next life utazaliwa katika mazingira gani. Hili nimelisikia siku nyingi ila sijawahi kulitilia maanani maana mimi kwa imani yangu mtu akifa ndo mwisho wake anasubiria hukumu ni either uzima wa milele au moto wa milele lakini naona kadri siku zinavyoenda natamani kujua zaidi kuhusu hili..hii imekaaje mshana jr
Hii kitu kwa iman za wenzetu huko wao huamin.
Hawaamin uumbaji sijui wa majini n. K wao huamin aina ya maisha unayoish ndio yatakufanya huwe kwa mtindo flan wa maisha. Usipo shika sawa sawa imani yako, watu huweza na facts na proof kidgo ukayumba.
Sasa tuseme kidgo hili.

Nakumbuka kuna scenario za mizim inayoweza kuitwa na kuvaaa mwili, kisha muhsika akawa ana behave kila kitu kama marehemu, au unaweza summon roho ya mtu, kama ilivyo kwa roho ya samweli ilvyoitwa. Lakini pia kuna kitu kinaitwa ALTER EGO, fatilia hiii utakuta inaweza link na hayo uwazayo
 
Usiende kwa waganga! Usitafute ufumbuzi wa matatizo yako nje ya utaratibu wa kusahihisha uumbaji kama kusafisha nyota na kufanya kafara na matambiko
Laana za ukoo zinatokana na kutaka kusahihisha michoro yetu
Mshana kuoga chumvi ya mabonge sio kusafisha/kuinua nyota??
 
Hapo kwenye Moyo Ni utashi sikubaliani.moyo Ni kiungo tu Kama viongo mwili kazi yake Ni ku-supply damu mwilini kupitia auricle na ventricle,Mambo ya cjui utashi Wala hauhusiani
siyo auricle yaani una maana ni moja, usahihi ni auricles yaani ziko mbili! Unajua hizi; Sinu Atria Node, na Purkinje fibres kazi zake kunako moyo? hizo ndo roho yenyewe inapokaa! inatoka nje na kurudi inavotaka.

Ukiota ndoto. sometimes hata uko mahali au watu ambao hujawahi kuwajua, au hata hujawahi kufika mahali hapo ulipoota ndotoni, kifupi hii ni roho yako ile inavinjali Duniani, haijawahi kupumzika toka uzaliwe hata vitoto vinaota sana, wakati mwingine inakwenda mpaka Mbinguni, lkn ukiamka tu, kumbukumbu inapotea.
 
Hauna makosa! Hauna mawaa kwa kizungu tunaweza kusema no errors no faults. ...najua utasema kuwa Mungu kasema hakuna mkamilifu!

Kumbuka kasema hakuna mkamilifu la hata mmoja akimaanisha mwanadamu sio roho. Makosa ya kiutendaji,makosa binafsi, makosa ya kukusudia na kutokusudia , habari za bahati mbaya na maneno kama heri ningejua....! Haya yote si ya kiroho ni ya kimwili

Ukisoma habari za jicho la tatu, machale ,ndoto taarifa ufunuo na maono unaona kwa usahihi kabisa ulimwengu wa roho ulivyotutangulia kufahamu yajayo kabla ya nafsi zetu kupata taarifa rasmi

Kila tukio liko preplanned. Hakuna bahati mbaya, ni limitations za ufahamu tu wa kibinadamu ndio umezuiwa kuona haya
Maisha yako na yangu yako kwenye mchoro kamili tangu kuzaliwa mpaka kufa...........

Utazaliwa lini na nani utapitia nini na wapi utakutana na nani! Utakuwa nani, utafanya nini, utaanguka wapi na kusimama wapi! Yote haya hayatokei kwa bahati mbaya

Jee huu ni ubaguzi?
Kwamba mmoja tangu kuzaliwa mpaka kufa yeye ni mafanikio tu?
Kwamba tangu kuzaliwa mpaka kufa ni yeye na matatizo matatizo na yeye?

Kwamba wengine husimama na kushamiri kisha huanguka na kupotea kabisa?
Kwamba wengine hukulia kwenye shida nyingi na matatizo lakini huja kutoboa na kutoka kimaisha?

Ulimwengu wa roho hauyumbishwi...formula zake ziko kama zilivyo michoro yake ni kamili na kamilifu unapojaribu kuisahihisha na ishu za waganga nyota na ngekewa unajitafutia dhahama usiyoiweza

Utafanikiwa kwa kipindi tu lakini asili itakurudisha kwenye shina lako kiroho..pale ulipotakiwa kuwa na hapo ni sawa na kujaribu kunyoosha bati lililopinda na kupondeka

Ulimwengu wa roho hauna modifications! Ishi maisha yako ukijibidiisha na ufanyayo katika mstari sahihi...usijaribu kutoka nje ya mstari kwa kuchanganya ya rohoni na ya kidunia ...hutafika mbali
Hekima ya pekee sana iliyopo kwenye maneno haya. Natamani sana walio wengi waweze kuiona. Mtu hahitaji kuji-modify mwenyewe, anatakiwa aiache nature ifanye kazi yake, akijibidisha kutenda yaliyo mapenzi ya Mungu tu, basi!
 
Mh kaka Mshana leo umeniacha gizai. Sasa nifanyeje ili niuishi mchoro wangu?
Usiyaumbe maisha kwa kutumia njia ambazo ziko nje ya akili yako uliyopewa na Mungu, na logic yako. Kwa mfano, kinachosababisha Profesa msomi aende kwa mganga wa kienyeji ni pale anapoona elimu yake kubwa aliyonayo inakumbana na kitu ambacho hakina logic, lakini kinafanya kazi, tofauti na uelewa wake ulivyo na elimu yake. Ni pale kwa mfano anaposhuhudia jiwe kubwa la tani zaidi ya 100 ambalo grader haiwezi kulisogeza hata nchi moja, linachezeshwa kwa kidole cha binadamu baada ya kuwa limetamkiwa maneno. Sasa Profesa hapa lazima ajiulize, tangu lini jiwe likasikia maneno ya mtu!
 
"Utafanikiwa kwa kipindi tu lakini asili itakurudisha kwenye shina lako kiroho..pale ulipotakiwa kuwa na hapo ni sawa na kujaribu kunyoosha bati lililopinda na kupondeka" Haya maneno mkuu yana ukweli mtupu lakini ndio hivyo,ngoja twende tu mpaka tufike mwisho,ina maana hata Wake /Wapenzi wetu tunapata nao mshike mshike inawezekana kiroho hawakutakiwa kuwa wetu ila tumelazimaisha tu kwakuwa ni warembo na tumetumia vipesa vyetu au ufundi wa kuwatongoza tukafanikiwa kuwapata...!
 
Hekima ya pekee sana iliyopo kwenye maneno haya. Natamani sana walio wengi waweze kuiona. Mtu hahitaji kuji-modify mwenyewe, anatakiwa aiache nature ifanye kazi yake, akijibidisha kutenda yaliyo mapenzi ya Mungu tu, basi!


Jr
 
Back
Top Bottom