Ulimwengu wa roho ni timilifu

Shida kubwa inayotufanya tusiujue sana umuhimu wa ulimwengu wa roho ni kwa sababu viongozi wetu wanao simama kila jumapili kutufundisha wametokana na KOROSAI 2:8 , badala na kutokana na KUMBUKUMBU 18:18-25. MUNGU BABA ameficha sirini mambo mengi ktk biblia na huwaonyesha wale tu wanao hubiri kwa kutumia KUMBU 18:18-25_lakini wanaotokana na korosai 2:8 hawaonyeshi siri zilizomo ndani ya biblia soma Wakorintho wa kwanza 2:6-10. Kiongozi wa kiroho lazima kila siku asikilize sauti ya MUNGU BABA inatoa maagizo gani kwa siku hiyo na siyo kusema uliyojipangia wewe kwa elimu yako ya dunia na kutunga litujia yako ya mwaka mzima. Soma KUMBU 28:1
 
Kama tungekuwa tunajuwa maisha ya mbele nadhani tungeacha hata kusoma, wakati unajuwa kabisa siku ya siku unakuwa jobless
 
Soul-Connection2.jpg


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mshana hii mada hua anaifundisha sana mwakasege nmeunganisha na hii napata kuelewa but kuna njia gani hasa kama ww unaweza msaidia mtu akatambua huu ulimwengu hasa kwa yaliyopita kwa mababu au wazee wake kwa maombi tnashauriwa tusali sana lakini sometimes tuna kata tamaa au kuchukulia poa

Shida kubwa inayotufanya tusiujue sana umuhimu wa ulimwengu wa roho ni kwa sababu viongozi wetu wanao simama kila jumapili kutufundisha wametokana na KOROSAI 2:8 , badala na kutokana na KUMBUKUMBU 18:18-25. MUNGU BABA ameficha sirini mambo mengi ktk biblia na huwaonyesha wale tu wanao hubiri kwa kutumia KUMBU 18:18-25_lakini wanaotokana na korosai 2:8 hawaonyeshi siri zilizomo ndani ya biblia soma Wakorintho wa kwanza 2:6-10. Kiongozi wa kiroho lazima kila siku asikilize sauti ya MUNGU BABA inatoa maagizo gani kwa siku hiyo na siyo kusema uliyojipangia wewe kwa elimu yako ya dunia na kutunga litujia yako ya mwaka mzima. Soma KUMBU 28:1
 
Hauna makosa! Hauna mawaa kwa kizungu tunaweza kusema no errors no faults. ...najua utasema kuwa Mungu kasema hakuna mkamilifu!

Kumbuka kasema hakuna mkamilifu la hata mmoja akimaanisha mwanadamu sio roho. Makosa ya kiutendaji,makosa binafsi, makosa ya kukusudia na kutokusudia , habari za bahati mbaya na maneno kama heri ningejua....! Haya yote si ya kiroho ni ya kimwili

Ukisoma habari za jicho la tatu, machale ,ndoto taarifa ufunuo na maono unaona kwa usahihi kabisa ulimwengu wa roho ulivyotutangulia kufahamu yajayo kabla ya nafsi zetu kupata taarifa rasmi

Kila tukio liko preplanned. Hakuna bahati mbaya, ni limitations za ufahamu tu wa kibinadamu ndio umezuiwa kuona haya
Maisha yako na yangu yako kwenye mchoro kamili tangu kuzaliwa mpaka kufa...........

Utazaliwa lini na nani utapitia nini na wapi utakutana na nani! Utakuwa nani, utafanya nini, utaanguka wapi na kusimama wapi! Yote haya hayatokei kwa bahati mbaya

Jee huu ni ubaguzi?
Kwamba mmoja tangu kuzaliwa mpaka kufa yeye ni mafanikio tu?
Kwamba tangu kuzaliwa mpaka kufa ni yeye na matatizo matatizo na yeye?

Kwamba wengine husimama na kushamiri kisha huanguka na kupotea kabisa?
Kwamba wengine hukulia kwenye shida nyingi na matatizo lakini huja kutoboa na kutoka kimaisha?

Ulimwengu wa roho hauyumbishwi...formula zake ziko kama zilivyo michoro yake ni kamili na kamilifu unapojaribu kuisahihisha na ishu za waganga nyota na ngekewa unajitafutia dhahama usiyoiweza

Utafanikiwa kwa kipindi tu lakini asili itakurudisha kwenye shina lako kiroho..pale ulipotakiwa kuwa na hapo ni sawa na kujaribu kunyoosha bati lililopinda na kupondeka

Ulimwengu wa roho hauna modifications! Ishi maisha yako ukijibidiisha na ufanyayo katika mstari sahihi...usijaribu kutoka nje ya mstari kwa kuchanganya ya rohoni na ya kidunia ...hutafika mbali
Asante..Ramani ya maisha
 
Kama uyasemayo ni kweli basi mafundisho yoyote yanayo amini ktk hukumu ya mwisho si yakweli....
Kama tangu kuzaliwa ramani yako ya maisha imechorwa na huwezi badili lolote ktk ulimwengu wa roho, kwa nini kuwe na hukumu???

Najaribu kuwaza tu!
Sio mkuu! Pamoja na kwamba unapitia njia iliyochorwa, njia hiyo uliiandika/uliichora mwenyewe wakati ule roho zote zilipohudhurishwa kwa Muumba. Kwa lugha rahisi, huo mchoro uliudizaini na kuuchora mwenyewe. Sasa unatembea kwenye njia uloijenga kwa mikono yako.
 
Mwee sasa kama mimi ni kizazi cha Tatu au Nne ndio nivumilie kuishi katika laana hizo kaka yangu?

Mkuu laana vjicho hasad zote zinaondoka na wewe ukabaki salama na kizazi chako kama utakuwa mtu wa maombi na kutoa sadaka.

Sadaka zina masharti sio vitu vya kubakia au visivotosha.
Sadaka inanuiliwa wakati wa kuitoa ili ifike sehemu sahihi.

Sadaka inatengeneza mfumo mzima wa maisha yako nakizazi chako.
 
Back
Top Bottom