Ulimwengu wa roho ni timilifu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
157,730
2,000
Hauna makosa! Hauna mawaa kwa kizungu tunaweza kusema no errors no faults. ...najua utasema kuwa Mungu kasema hakuna mkamilifu!

Kumbuka kasema hakuna mkamilifu la hata mmoja akimaanisha mwanadamu sio roho. Makosa ya kiutendaji,makosa binafsi, makosa ya kukusudia na kutokusudia , habari za bahati mbaya na maneno kama heri ningejua....! Haya yote si ya kiroho ni ya kimwili

Ukisoma habari za jicho la tatu, machale ,ndoto taarifa ufunuo na maono unaona kwa usahihi kabisa ulimwengu wa roho ulivyotutangulia kufahamu yajayo kabla ya nafsi zetu kupata taarifa rasmi

Kila tukio liko preplanned. Hakuna bahati mbaya, ni limitations za ufahamu tu wa kibinadamu ndio umezuiwa kuona haya
Maisha yako na yangu yako kwenye mchoro kamili tangu kuzaliwa mpaka kufa...........

Utazaliwa lini na nani utapitia nini na wapi utakutana na nani! Utakuwa nani, utafanya nini, utaanguka wapi na kusimama wapi! Yote haya hayatokei kwa bahati mbaya

Jee huu ni ubaguzi?
Kwamba mmoja tangu kuzaliwa mpaka kufa yeye ni mafanikio tu?
Kwamba tangu kuzaliwa mpaka kufa ni yeye na matatizo matatizo na yeye?

Kwamba wengine husimama na kushamiri kisha huanguka na kupotea kabisa?
Kwamba wengine hukulia kwenye shida nyingi na matatizo lakini huja kutoboa na kutoka kimaisha?

Ulimwengu wa roho hauyumbishwi...formula zake ziko kama zilivyo michoro yake ni kamili na kamilifu unapojaribu kuisahihisha na ishu za waganga nyota na ngekewa unajitafutia dhahama usiyoiweza

Utafanikiwa kwa kipindi tu lakini asili itakurudisha kwenye shina lako kiroho..pale ulipotakiwa kuwa na hapo ni sawa na kujaribu kunyoosha bati lililopinda na kupondeka

Ulimwengu wa roho hauna modifications! Ishi maisha yako ukijibidiisha na ufanyayo katika mstari sahihi...usijaribu kutoka nje ya mstari kwa kuchanganya ya rohoni na ya kidunia ...hutafika mbali
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
53,876
2,000
Kuna watu wanaamini ukifa unazaliwa mara nyingine tena..unaweza kuzaliwa mtu yuleyule na sura ileile au kiumbe kingine. Wanadai maisha uliyoishi ndo yana-determine next life utazaliwa katika mazingira gani. Hili nimelisikia siku nyingi ila sijawahi kulitilia maanani maana mimi kwa imani yangu mtu akifa ndo mwisho wake anasubiria hukumu ni either uzima wa milele au moto wa milele lakini naona kadri siku zinavyoenda natamani kujua zaidi kuhusu hili..hii imekaaje mshana jr
 
mzee wa mazabe

JF-Expert Member
May 10, 2016
839
1,000

Utakuwa uliona kwenye Tamthilia ya second chance!!
 
Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
3,676
2,000
Roho,mwili,moyo na nafsi.Hivi vitu vinatofautiana vipi mkuu?Je ni ipi hasa injini halisi ya mwanadamu katika maisha ya kila siku?
Nielewavyo mimi, injini ya uhai ni Roho na injini ya matendo, hisia, kumbukumbu, tabia na kadhalika ni NAFSI, mwili ni sehemu ambayo Roho na NAFSI ndo makao yake, MOYO ni utashi

Nipo tayari kukosolewa, nimeeleza navyoelewa mimi
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,214

Umenena vema mkuu japo bado sijakupata hivi
 
gambagumu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
996
1,000
Maisha yetu huwa yanasimamiwa na mikataba ya kiroho(maagano) ambayo either ilifanywa kati mababu, wazazi wetu au sisi wenyewe na miungu.
Viwango vya maisha vinafungwa kwenye mikataba hiyo na ndo maana level ya hali ya maisha inafanana sana kwenye familia au ukoo au hata kabila.
Mikataba hii inadumu hadi kizazi cha nne otherwise ujue jinsi ya kuifunja na kuingia mkataba mpya na Mungu Mwenye nguvu (Creator of universe)
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,214
2,000
Ningependa kujua nafsi ni nini na roho ni nini?Je baada ya kifo kipi kinakufa na kipi kinabaki?Je kinachobaki kinakwenda wapi??
 
Mr Miller

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
11,193
2,000
Maisha yetu huwa yanasimamiwa na mikataba ya kiroho(maagano) ambayo either ilifanywa kati mababu, wazazi wetu au sisi wenyewe na miungu.
Viwango vya maisha vinafungwa kwenye mikataba hiyo na ndo maana level ya hali ya maisha inafanana sana kwenye familia au ukoo au hata kabila.
Mikataba hii inadumu hadi kizazi cha nne otherwise ujue jinsi ya kuifunja na kuingia mkataba mpya na Mungu Mwenye nguvu (Creator of universe)
YESU pekee anaweza vunja hiyo mikataba
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom