Ulimwengu wa 3D na 4D

Ulimwengu wa 3D na 4D

...nilijua tu nyie wavaa visuruali vifupi ni short sight mno...mnachojua na kuamini ni jua kuzama matopeni tu
....hamko tayari kabisa kupokea elimu mpya vichwani mwenu..hopeless kabisa nyie
teh teh teh.
yaani Mimi kuvaa suruali fupi wewe tayari umenuna.
Vipi IGWE mumeo ana wake wawili au?
acha wivu wa kitoto.
suruali fupi nivae mimi jazba upate wewe, halafu unaniita hopeless.

halafu elimu gani iliopo hapa ambayo ungependa na sisi wavaa suruali fupi tujifunze? kuona kwa jicho la tatu au?
 
Kitu gani unachokijua zaidi ya ulivyofundishwa?
Nilivyofundishwa na nani?kuhusu nini? Hicho unachokijua wewe hukufundishwa? Ulikijuaje? Na ni nini kingine unachokijua tofauti na hicho unachokijua/ulichofundishwa?
 
teh teh teh.
yaani Mimi kuvaa suruali fupi wewe tayari umenuna.
Vipi IGWE mumeo ana wake wawili au?
acha wivu wa kitoto.
suruali fupi nivae mimi jazba upate wewe, halafu unaniita hopeless.

halafu elimu gani iliopo hapa ambayo ungependa na sisi wavaa suruali fupi tujifunze? kuona kwa jicho la tatu au?
...jamaa katumia muda mwingi kuandaa hii thread halafu unakuja pinga kwa hoja mfu....inakera sana kupinga jambo kwa research feki
 
mkuu naona kama aujamuelewa mtoa mada vizuri kutokana na yeye kajichanganya kidogo alivyoanza na mambo ya 3D na 4D za kisayansi zaidi lakini mwisho wa uzii ameenda kwenye point yake mambo ya kumeditate na mjicho wa tatu sijui

Dunia ina mambo mkuu kwa habari ya jicho la tatu alilo lizungumzia mtoa mada ni kweli kabisa inawezekana na ukiwa na nia ya kulifungua ilo jicho litafunguka tu na utaona madudu ya ajabu ajabu
Hivi hilo jicho la tatu haliwezi funguka mpaka ukae sehemu iliyotulivu na kufumba macho....au hakuna njia nyingine zaidi ya hii.
Niliwahi kusoma kitabu kimoja kinaitwa 'The witch of Potobelo' walikuwa wanaingia kwenye hall flani wanawasha mziki na kuanza kucheza kwa hisia Kali mpaka wanajikuta wapo kwenye ulimwengu mwingine nadhani nayo hii ni Meditation
 
Nilivyofundishwa na nani?kuhusu nini? Hicho unachokijua wewe hukufundishwa? Ulikijuaje? Na ni nini kingine unachokijua tofauti na hicho unachokijua/ulichofundishwa?
Hujajibu swali langu mkuu. Ni kitu gani unachokijua tofauti na ulivyofundishwa?
 
Mbona upo nje ya Mada
hujajibu lolote ila umemkashifu kuwa jamaa hajui lolotwe kuhusu 4D
mwenzako kasema ACHENI KUTULETEA UONGO
na ni kweli hamjagusia 3D wala 4D
mnatuletea YOGA mara sinema
kwanini usiingie Google au Wikipedia
kupata maana ya 3Dimension au 4Dimension
ni tofauti kabisa na hizo YOGA
View attachment 884944
kuna binaadamu wengine Mungu kawaumba kuwa sababu ya kuchafua mazingira tu na mfano mzuri ni huyu anaejiita LUCKDUBE as if he is one of Lucky one..

Watu wanajadili Pilau yeye analeta habari ya Oil na Grease.
kaazi kweli kweli.
 
...jamaa katumia muda mwingi kuandaa hii thread halafu unakuja pinga kwa hoja mfu....inakera sana kupinga jambo kwa research feki
hio research feki umeiona wapi IGWE?
au umeianza weekend mapema?
manake ukishakuwa ktk Influence of alcohol inakuwa shida sana ku reason na waungwana.
hebu tulia kidogo watu wajadili mada husika.
mambo ya Yoga yatafutie uzi wake.
hapa sio mahala pake
 
Hivi hilo jicho la tatu haliwezi funguka mpaka ukae sehemu iliyotulivu na kufumba macho....au hakuna njia nyingine zaidi ya hii.
Niliwahi kusoma kitabu kimoja kinaitwa 'The witch of Potobelo' walikuwa wanaingia kwenye hall flani wanawasha mziki na kuanza kucheza kwa hisia Kali mpaka wanajikuta wapo kwenye ulimwengu mwingine nadhani nayo hii ni Meditation
Hio ni Hallucination Bro.
tabia hizi wanazo hata watu wa Ethiopia.

wanacheza mziki huku wanakunywa mitishamba mpk wanaanza kuona mambo wanayotaka wao
 
Mi naogopa hapo tu kushindwa kurudi na kuanza maisha mapya na viumbe vya ajabu

ngoja mtoa mada aje na part two, atuambie jinsi ya kurudi ,ila nadhani ukisema tena Meyi,Meyi utarudi duniani kama ulivyoenda lol..
 
hakuna kitu kama hii Bro. hizi ni ndoto ambazo Holywood wamezipandikiza ktk vichwa vya watu.
asilimia 99 ya maneno ya watabiri wote na waganga wote NI UONGO.
Nimefanya Research miaka chungu mbovu.

Usipoteze muda wako kuzigeuza hizi fictions kuwa Reality. Hizi habari za 4 Dimension ziwache kwenye movie's tu. kinyume cha hapo utapoteza muda wako huenda ukadhurika kwa kulishwa UCHAFU na sumu na waganga wa kienyeji.
Nakataa mkuu, hii kitu ni kweli na haiusishwi na imani potofu hata kidogo, binafsi ni shaidi nimefanya sana meditation kipindi tunajifunza shoulin kung fu mkuu, hakuna uchawi katika hili nasisitiza, kama hujawahi jaribu na haijawai kutokea utaamini hivyo ila ukiielewa vizuri kiukweli iko poa sana, inaongeza nguvu za akili mwili na roho!! Siyo kila unayemwona mnaishi naye katika ulimwengu mmoja wapo watu wanaoishi katika maeneo mengine tofauti ila kimwili ndo wamuona bongo!! Usipotoshwe kuna mengi katika dunia fungua kichwa kuwa tayari kujifunza, kizuri chukua kibaya tia kando!!!
 
Nimekwambia hii kitu ya Kuhama ulimwengu Physically HAIPO ndugu.

nakubali bila kipingamizi chochote kuwa Meditation zipo na Mimi ni mmoja wa watu wenye ku practice meditation on daily basis lkn usinambie wewe au yyt ktk wanaadamu anaweza kuishi ulimwengu mwingine .

Kuhamisha fikra kutoka hapa kwenda Mars au chini ya bahari hakumaanishi nguvu yyt ya ziada.
akili ya binaadamu inaweza kusafiri all over the place lkn utakacho kiona huko ni aidha imaginations au kile ambacho umeshakiona aidha kwenye movies au fantasy zako binafsi.

ni sawa na Ndoto.

wewe unaweza kuota chochote na mpk mwili wako uka respond na Ndoto ile mpk ukajikuta unatoka jasho au unapiga kelele kutokana na ile Ndoto lkn ndani ya ndoto ile Hakuna UHALISIA WWT zaidi ya imaginations.

Na suala la kuongeza nguvu through meditation hilo pia nalikubali lkn sivyo unavyotafsiri wewe.

ntakupa mfano hapa.

mtu anapokuwa muoga sana wa kuona nge au nyoka through meditation anaweza kuuondoa huo uoga.
au mtu mwenye uoga wa kupanda ndege pia anaweza kuuondoa uoga huo
lkn mtu mwenye uwezo wa kubeba kilo 50 hata afanye meditation siku 100 kamwe hawezi kubeba kilo 100. labda afanye mazoezi pamoja na lishe ya nguvu .

Ingekuwa through meditation unaweza kuona yanayokuja au yaliojificha sidhani km kungekuwa na haja ya serikali Kusomesha watu miaka 20 mpk 30 na kuajiri Wapelelezi wa kesi za mauwaji na kesi mbali mbali. Serikali ingetoa ajira kwa Meditators na Hao wenye macho ya 3D na 4D Tukamaliza matatizo yote ya Hizi kesi.
 
mkuu hakuna sehemu nimekataa kuwa Dunia hii ina mambo ya ajabu. tena ajabu sana.

kuna mambo nimekutana nayo ktk maisha yangu huwezi kuyaingiza kwenye science yakakubalika hata kidogo.

na kuhusu Jicho la tatu nakuhakikishia kwa asilimia 100 kuwa HUWEZI KUONA UHALISIA WWT bali utakachoweza kuona ni Uongo mkubwa na ukweli kidogo mno. na hii ni Kazi ya Majinni.

Watu wengi Duniani wamekuwa wakitumia majinni kutazama mambo yao na ya wengine sehemu mbalimbali Duniani.
Na Haya mambo yanafanyika DUNIA NZIMA.

Lkn kusema ukae peke yako ufanye meditation kisha uone bila kuingiza Ushirikina Hio kitu hakuna kaka.

unless uwe ktk influence of Drugs au mitishamba mikali inayosababisha akili ihame ktk Ulimwengu usiojulikana. na utakachokiona ni ktk yale yale uluokuwa ukitamani kuyaona.

hii wanafanya sana watu wa North America.
nimeona watu wa Peru,Na Pande za Bolivia ati wakitaka kutatua matatizo yao wanakunywa mitishamba flani kisha wanaongea na mizimu. kumbe zile zote ni Hallucination tu zinazotokana na ile mitishamba lkn Hakuna ukweli wwt ndani yake.
Ni sawa na mvuta bangi kavuta bangi kali kuliko zile alizo zoea kisha akaanza kuona maisha yake yoote yametengemaa kumbe bado anapiga debe kwenye daladala.
Haya mambo huyaelewi ndio maana unasema ni uongo

Wengine huku tumeyaxperiece wenyewe kupitia kusoma tu tena humu humu jf mkuu

Achana na maisha kabisa
 
hakuna kitu kama hii Bro. hizi ni ndoto ambazo Holywood wamezipandikiza ktk vichwa vya watu.
asilimia 99 ya maneno ya watabiri wote na waganga wote NI UONGO.
Nimefanya Research miaka chungu mbovu.

Usipoteze muda wako kuzigeuza hizi fictions kuwa Reality. Hizi habari za 4 Dimension ziwache kwenye movie's tu. kinyume cha hapo utapoteza muda wako huenda ukadhurika kwa kulishwa UCHAFU na sumu na waganga wa kienyeji.
Kabla Hollywood haijawepo haya yalikuwepo
 
Back
Top Bottom