kahtaan
JF-Expert Member
- Jul 11, 2009
- 19,156
- 11,608
mkuu hakuna sehemu nimekataa kuwa Dunia hii ina mambo ya ajabu. tena ajabu sana.mkuu naona kama aujamuelewa mtoa mada vizuri kutokana na yeye kajichanganya kidogo alivyoanza na mambo ya 3D na 4D za kisayansi zaidi lakini mwisho wa uzii ameenda kwenye point yake mambo ya kumeditate na mjicho wa tatu sijui
Dunia ina mambo mkuu kwa habari ya jicho la tatu alilo lizungumzia mtoa mada ni kweli kabisa inawezekana na ukiwa na nia ya kulifungua ilo jicho litafunguka tu na utaona madudu ya ajabu ajabu
kuna mambo nimekutana nayo ktk maisha yangu huwezi kuyaingiza kwenye science yakakubalika hata kidogo.
na kuhusu Jicho la tatu nakuhakikishia kwa asilimia 100 kuwa HUWEZI KUONA UHALISIA WWT bali utakachoweza kuona ni Uongo mkubwa na ukweli kidogo mno. na hii ni Kazi ya Majinni.
Watu wengi Duniani wamekuwa wakitumia majinni kutazama mambo yao na ya wengine sehemu mbalimbali Duniani.
Na Haya mambo yanafanyika DUNIA NZIMA.
Lkn kusema ukae peke yako ufanye meditation kisha uone bila kuingiza Ushirikina Hio kitu hakuna kaka.
unless uwe ktk influence of Drugs au mitishamba mikali inayosababisha akili ihame ktk Ulimwengu usiojulikana. na utakachokiona ni ktk yale yale uluokuwa ukitamani kuyaona.
hii wanafanya sana watu wa North America.
nimeona watu wa Peru,Na Pande za Bolivia ati wakitaka kutatua matatizo yao wanakunywa mitishamba flani kisha wanaongea na mizimu. kumbe zile zote ni Hallucination tu zinazotokana na ile mitishamba lkn Hakuna ukweli wwt ndani yake.
Ni sawa na mvuta bangi kavuta bangi kali kuliko zile alizo zoea kisha akaanza kuona maisha yake yoote yametengemaa kumbe bado anapiga debe kwenye daladala.