Ulimboka, Mwangosi wamponza Kikwete UN

Bora wapelekwe the Hague kuliko kuja kupatwa na yale laiyomkuta Ghadaffi na wanae. Wakina kova wajanja wameshajivua kwamba hawahusiki. CCM imekwisha
 
93.jpg

Kwani wameanza kuua leo, wale waliofukiwa Shinyanga kwenye machimbo bado hawajasahaulika ... .... .. licha ya watoto walioteketea kwa moto kule Tabora.
 
Sijui serikali ya kikwete inafikiria nini juu ya madai ya waalimu.Serikali imeendelea kuwapuuza Walimu,mfano;Mwalimu aliyemaliza shahada ya ualimu wa Physics na Mathematics anaanza na mshahara wa TGTS D,lakini mtu aliyemaliza uhandisi (Engineering),akakosa kazi ya uhandisi,akaomba ajishikize kwenye ualimu,afundishe Physics au Mathematics,yeye huanzia daraja la juu yaani TGTS E.Kwanini serikali inawadharau sana walimu? Mishahara yao midogo,madaraja hayapandi kwa wakati,madai yao yanacheleweshwa mno na mengine hayaripwi kabisa. Mwanzo ilionekana kama migomo ya walimu sio tishio,sasa walimu wameerevuka,wamegundua kuwa kumbe wanayo silaha,nao ni wanafunzi.Wakati ule waliandamana wanafunzi walio DSM tu.Wanafunzi wote walio katika shule za walalahoi-shule za serikali wanafundishwa na walimu kuwa,ukitokea mgomo wa walimu,wanafunzi waandamane na waihujumu miundombinu yote ya CCM.Wakati umefika kwa serikali kurudisha usawa katika vipato kwa waajiriwa wake wote,wakiendelea na dharau kwa waalimu,wajiandae kushuhudia maandamano makubwa ya wanafunzi kuanzia chekechea mpaka form six,maandamano yatakayoambatana na vurugu.Kwa uzembe wa polisi,waziri na IGP watafikishwa kwenye mahakama za kimataifa.ACHENI KUWABAGUA WAAJILIWA WA SERIKALI!
nini tofauti kati ya TGTS D na TGTS E interms of payment?? wengine hatujawahi kuwa waalim na hatuvijui hivi msaada wako please??
 
Jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao ni la polisi. Polisi naye ni raia, kama polisi akiuwawa bado lawama za kutotimiza wajibu wa kulinda usalama wa raia ni la chombo cha usalama wa raia-POLISI. Utofautishe kati kutetea haki za binadamu na kulinda usalama wa raia. Wanaharakati tayari wametimiza wajibu wao wa kutetea haki za raia hata hivyo hwakutaja wahanga wote. Wametaja baadhi tu kutoa mwanga kwenye uso wa dunia ijue kinachotendeka nchini. Mifano zaidi ikihitajika itatolewa ikiwemo ya polisi kuuwawa.
Mkumbushe mleta uzi kuwa asisahau kuwakumbusha hao anaowaita UNHCR wanapotetea mauaji,wasisahau na polisi wanaouawa kinyama na raia kama kweli wanatetea uhai!
 
Wale waliomwomba BWANA aliwaambia: NYAMAZENI KIMYA. MIMI NITAWAPIGANIA. Kwa muda mrefu, wanyonge wa nchi hii wamekuwa wakimlilia BWANA awaokoe na mateso, kuonewa, kunyanyaswa na walio madarakani. BWANA amesikia kilio chao. Ole wao wale wote wanaotenda maovu, wakiwa ni viongozi wanaoongoza watu wa BWANA. Watatamani ardhi ipasuke ili iwameze. Lakini, ardhi itakaa hivyo vivyo. Mioyo yao itakuwa inalia kwa uchungu. BWANA atatenda. Hasira za BWANA zitawawakia. Watalala kwenye vitanda vyao vya dhahabu, na kula vinono walivyopora kutoka kwa wanyoge. Lakini, hawatapata usingizi kwa vile BWANA atawaadhibu kwa matendo yao maovu wanayowatendea watu wasio na sauti
 
Tofauti ya TGS inategemea muda wa masomo wa kozi husika baada kumaliza high school. Wanaochukua kozi kwa miaka mitatu huanza TGS D. Mfano waalimu, wahasibu au wachumi. Wanaochukua miaka minne na zaidi huanzia TGS E. Mfano wahandisi, madaktari au wanasheria.
nini tofauti kati ya TGTS D na TGTS E interms of payment?? wengine hatujawahi kuwa waalim na hatuvijui hivi msaada wako please??
 
Afadhali umempa jibu huyu Sangu Mnene. Tofauti ya mishahara ya kuanzia Serikalini (TZ) kwa wale wenye degree inategemea masomo ya chuo kikuu yalikuwa ya miaka mingapi. Siyo suala la kudhararu mtu wala taaluma.

Tofauti ya TGS inategemea muda wa masomo wa kozi husika baada kumaliza high school. Wanaochukua kozi kwa miaka mitatu huanza TGS D. Mfano waalimu, wahasibu au wachumi. Wanaochukua miaka minne na zaidi huanzia TGS E. Mfano wahandisi, madaktari au wanasheria.
 
Wachukue hatua kali za kuwashitaki The Hague na si kusitisha misaada, hii haitakuwa sawa. Kwani mara nyingi wanakimbilia kusitisha misaada wakidhani wanaikomoa serikali kumbe wanakomoa wananchi!
 
Wale waliomwomba BWANA aliwaambia: NYAMAZENI KIMYA. MIMI NITAWAPIGANIA. Kwa muda mrefu, wanyonge wa nchi hii wamekuwa wakimlilia BWANA awaokoe na mateso, kuonewa, kunyanyaswa na walio madarakani. BWANA amesikia kilio chao. Ole wao wale wote wanaotenda maovu, wakiwa ni viongozi wanaoongoza watu wa BWANA. Watatamani ardhi ipasuke ili iwameze. Lakini, ardhi itakaa hivyo vivyo. Mioyo yao itakuwa inalia kwa uchungu. BWANA atatenda. Hasira za BWANA zitawawakia. Watalala kwenye vitanda vyao vya dhahabu, na kula vinono walivyopora kutoka kwa wanyoge. Lakini, hawatapata usingizi kwa vile BWANA atawaadhibu kwa matendo yao maovu wanayowatendea watu wasio na sauti

.
Aamen. Bwana Mungu hakika huwapigania watu wake in mysterious way. Mkuu wa nchi ni mjanja kama ahabu. Aliamua kutafuta watu wanaojiita watumishi ili kuwazuga maskini wanaoibiwa kama vile Ahabu alivyolipanga kundi la manabii mia nne ili limtabirie mema. Miongoni mwa watumishi walionaswa na mkulu ni pamoja na kina G. Rwekatare. Habari hizi zimfikie G.L nae ajue kuwa umasikini uliotamalaki nchini kwa sababu ya kundi la watawala wacheche kujigawia rasilimali za nchi yeye ni mmoja wao. Hivyo pia anapaswa ajitathmini.
Bwana Mungu usinyamaze hata umelikata shauri hili la watawala walioamua kuwala watu wako kama vile mtu alavyo mkate.
.
 
Sehemu iliyonifanya nilengwe machozi kwenye hiyo reporti ni story ya watu wa Kisarawe na Kambi ya wakimbizi ya Katumba. Wananchi wanaachwa bila sehemu ya kwenda, ardhi yao wanapewa wawekezaji. Mtanzania anaachwa bila sehemu ya kwenda, matapeli wa serikalini wakiwemo waziri mkuu wanahusika kuwanyayasa wananchi wao. Halafu utakuta mpumbavu mmoja anasimama kulaumu wazungu kwa kila kitu, hivi ni mzungu anayetuambia tudhulimiane kiasi hiki. Hata angetuambia kwanini tusikatae?
Wale wanaopeleka hizi dhuluma kwa wazungu si kwamba hawajithamini lakini hawana pa kwenda zaidi ya kuwakilisha haya kwa bwana mkubwa anayeonekana kujali haki za wanyonge. Wengine ukisema wazungu wanajali haki za wanyonge watabisha mpaka mishipa inataka kukauka lakini hata wao wakibanwa sijawahi kusikia wakipeleka malalamiko yao kwa wachina au wajapan. Hivi itafika Afrika nasi tupate nchi au taasisi ya jumuiya za Afrika zinayojali haki na kuchukua hatua kwa dhuluma kama hizi?
Hata kama impact yake itakuwa ndogo lakini angalau Kikwete aunge kwenye tera la Kagame kama viongozi wanaokiuka haki za watu huku wakijifanya wazuri kwa nchi za magharibi kabla hajaingia M7 humo kwenye chumba cha marais wahuni na wauaji wanaojificha mchana kwa vicheko huku usiku wameshika visu kuwachinja wananchi wao.
 
Kamanda, Marekani haipo hivyo. Naweza kukuthibitishia swala la Richmond halijulikani kabisa kwenye serikali ya Marekani. Richmond walikuwa wa huni tu. Na kama hii ngoma imefika kwenye senetor. Ngoja utaona MOTO.

symbion ni mama crinton na alikuja dom akahakikisha kuwa mambo mazuri na symbion ndio walinunua richmond.Labda sera za amerika zifuatwe!..no permanent enemy no permanent friend!!!!!!!!!!!!
 
Afadhali umempa jibu huyu Sangu Mnene. Tofauti ya mishahara ya kuanzia Serikalini (TZ) kwa wale wenye degree inategemea masomo ya chuo kikuu yalikuwa ya miaka mingapi. Siyo suala la kudhararu mtu wala taaluma.
Sio kweli,wapo walimu waliomaliza chuo kikuu miaka ya 2000,walisoma miaka 4 wakaanza na TGS D,Wahandisi wa St Joseph husoma miaka 3,huanza na TGS E.Wanasheria husoma miaka 3 chuo kikuu cha Tumaini,huanza na TGS G,Madaktari husoma miaka 6 Muhimbili,huanza na TGS F,Kilimo-Utafiti husoma miaka 3 Sokoine,huanza na TGTS H.Kumbuka,kutoka ngazi moja ya mshahara kwenda nyingine unahitajika kuwepo kazini zaidi ya miaka 4.Kama si ubaguzi,kwanini Mhandisi apitwe na mwanasheria? CCM itakuja adhibiwa kwa ubaguzi wake.Subirini mgomo wa walimu unaofuata,wanafunzi wao wataiadhibu serikali kwa ubaguzi wake.
 
Back
Top Bottom