Ulimboka, Mwangosi wamponza Kikwete UN

Ulimboka, Mwangosi wamponza Kikwete UN

Kwa kweli suala la Dr.Ulimboka ni aibu tupu.Maskini my motherland!
 
KUUAWA kikatili kwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi na tukio la kutekwa, kuteswa kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, limechukua sura mpya ambapo sasa limetinga katika Seneti ya Marekani, Tanzania Daima Jumamosi limeelezwa.

Taarifa kutoka Washington nchini Marekani zinasema Rais Jakaya Kikwete amelalamikiwa rasmi katika Seneti na wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu nchini, na kwamba masuala hayo sasa yatafikishwa kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu (UNHRC) kwa hatua zaidi.

Mbali na mauaji ya Mwangosi na tukio la Dk. Ulimboka, Rais Kikwete pia amelalamikiwa kwa kufumbia macho matukio mengi ya kuteswa na kuuawa kwa raia pamoja na kufungiwa kwa gazeti la kila wiki la uchunguzi la MwanaHalisi, kutoroshwa wanyama hai kwa kupelekwa nje ya nchi na hatua ya polisi kutumia silaha za kivita kupambana na raia wasio na silaha wakiwemo wanafunzi wanaoandamana.

Ripoti hiyo ya wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu yenye kurasa 27, inatuhumu utawala wa Rais Kikwete kwa kukandamiza demokrasia kwa kutumia polisi na vyombo vingine vya dola.

Watetezi hao wa haki za binadamu, wamedai kuwa baada ya kufanikiwa kuingiza masuala haya ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika Seneti ya Marekani, sasa wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha suala hili linafikishwa Umoja wa Mataifa kwa kile walichokiita, kuiadabisha serikali.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopatikana, na pia kusambazwa katika baadhi ya taasisi za habari, suala hilo liko mikononi mwa Seneta Kerry, ambaye baada ya majadiliano katika Seneti, ripoti hiyo itapelekwa UNHRC.

Habari zinasema baadhi ya wajumbe wa Seneti waliofanikiwa kuona ripoti hiyo wamemeshitushwa na kile walichokishuhudia katika picha zilizoambatanishwa.

Aidha, ripoti hiyo pia imeeleza jinsi rushwa ilivyoshamiri nchini, ukandamizaji juu ya uhuru wa maoni na matumizi mabaya ya vyombo vya dola kudhibiti vyama vya upinzani na kutumia silaha za kivita kupambana na raia wasio na silaha.

Ripoti hiyo ya kuishitaki Serikali ya Kikwete, pia imelaani vitendo vya polisi kusambaratisha maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, walioandamana Julai 31, mwaka jana kupinga ukosefu wa walimu nchini.

Mgomo wa wanafunzi ulikuja baada ya walimu wa shule za msingi na sekondari kupitia jumuiya yao - Chama cha Walimu Tanzania (CWT) – kuitisha mgomo nchi nzima wa kutaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi zao, nyongeza ya mishahara na malimbikizo ya posho.

Nyaraka zilizowasilishwa na wanaharakati hao, zimeambatanishwa na picha zinazoonesha namna Jeshi la Polisi lilivyohusika kuuawa kwa Mwangosi, picha mbaya ya maiti ya mwanahabari huyo, na namna Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alivyokuwa akishuhudia askari wake wakimsulubu mwanahabari huyo kabla ya kufunga kazi kwa kumaliza uhai wake.

Kadhalika, kumeambatanishwa picha zinazoonesha maiti za watu waliouawa wakati wa maandamano huko Arusha, na ile inayosadikiwa kutokea kule Songea. Picha nyingine za kusikitisha ni zile zinazoonesha askari zaidi ya watano wakimdhibiti mwanaharakati mmoja katika maandamano, na umati wa wanafunzi wa shule za msingi wakiandamana, huku nyingine zikionesha askari mwenye silaha ya kivita akimsindikiza mwanafunzi wa kike mwenye mfuko wa madaftari.

Tangu mwaka 2005 ambapo masuala mazito ya rushwa yamekuwa yakiibuliwa, ikiwamo ununuzi wa rada feki, wizi wa fedha za umma kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mkataba tata wa Richmond, ukusanyaji wa kodi, utoroshwaji wa wanyama hai, wizi wa nyara za serikali, ikiwamo pembe za ndovu, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituhumu serikali kushindwa kuchukua hatua.

Vilevile, wananchi wamekuwa wakituhumu Serikali ya Kikwete, kukumbatia wezi wa fedha za umma katika halmashauri za miji na wilaya, uporaji wa ardhi unaofanywa na makampuni makubwa ya ndani na nje ya nchi.

Jana, Tanzania Daima Jumamosi haikufanikiwa kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu kuzungumzia iwapo serikali ina taarifa juu ya jambo hili kwa kuwa simu yake ilikuwa ikiita muda wote bila kupokelewa.

Kova ajivua

Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova jana ametangaza rasmi kujivua katika sakata zima la kuchunguza kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka.

Aidha, Kova pia amekanusha madai ya kuunda tume kuchunguza suala hilo, akitaka asiulizwe jambo lolote, huku akisukuma tukio hilo kwa wakubwa wake.

Juzi, Kamanda Kova aliliambia Tanzania Daima kwamba, jana angeweka wazi suala hilo ili Watanzania wajue kilichojiri kuhusiana na kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, jambo ambalo limetikisa anga, likiwemo lile la kukamatwa kwa raia wa Kenya, Mulundi anayedaiwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo, kinyume na matarajio ya wengi, jana Kamanda Kova aliruka kimanga na kudai kwamba wenye uwezo wa kulitolea maelezo ni wakuu wake wa kazi, kwa maana ya Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kuhusu kuundwa kwa kamati ya kuchunguza utekaji huo, Kova alisema kilichofanyika wakati huo ni kuundwa kwa jopo la uchunguzi ambalo taarifa zake hazina ulazima wa kutolewa mbele ya jamii zaidi ya kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa kile walichokibaini.

Alisema baada ya kukamilisha kazi yake, alipeleka jukumu la kupeleleza sakata hilo katika ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini (DCI) ambayo ndiyo yenye jukumu la kutoa maelezo

TANZANIA DAIMA
 
UNHCR ndo sh r ka mama la utetez wa hak za k b nadam ambalo l meanz shwa under UN
 
msaada jamani:hivi shirika la kutetea haki za binaadam duniani ni unhcr au amnesty international
utawaweza watu wa chama cha masalia na hilo gazeti lao?!hayo mambo yanatakiwa tuyaone kwenye countries condition report ya un na marekani ndio tutaamini wanachokisema,otherwise ni porojo za kisiasa kama nyingine tu,wamarekani si wana ubalozi hapa na mle ubalozini kuna vitengo kibao ikiwemo kilicho responsible kukusanya taairfa about country condition report pia un hivyo hivyo wako hapa,poa lakini itasaidia wabongo wanaotaka kujilipua kama ikiwork!
 
Naomba Tusikurupuke duh.

Uzi uko wazi zaidi ni UNHRC kwa kirefu United Nations Human Rights Council sio UNHCR ambalo kirefu chake ni United Nations High Commissioner for Refugees na Amnesty Internation ni NGO inayoshirikisha mashirika mengi ya haki za binadamu duniani na wala si sehemu ya UN ni sawa na LHRC hapa TZ. Hivi vitu tulijifunza shule ya Msingi.
 
Jina la mwangosi na ulimboka ni mtaji mkubwa sana saivi kwa wanasiasa na wanaharakati na waandishi wa habari.

Halafu what a coincidence,wote wanyakyusa!ingekua wachagga pangekua hapatoshi hapa jf
 
Daima limeharibika zaidi baada ya absalom kibanda kuondoka
Hivi kahamia wapi yule kilaza nae au ndio kapewa ile kazi na lowassa wake?kile kitabu alichotishia kumtungia mzee samuel sitta kiliishiaga wapi?
 
rais wa kwanza afrika kukutana na obama hapo kazi ni republican vs democratic juu ya masuala ya kimataifa
 
Kama wanadhani watatuua tulishakufa tangu kale na kama wanadhani tumekufa Mawazo yetu yapo na mwishoni kabisa watatekeleza mawazo yetu.
 
Nape na MWIGULU karibuni mchangie. Kweli magamba mmevuliwa na kuachwa uchi. Binafsi nimependa hizi jitihada zinazofanywa na wanaharakati na wapenda haki za binadamu. Natamani siku moja nitakawaona watuhumiwa wote kuanzia kwa rais, IGP, RPC Kamuhanda, Nape, Mwigulu, Kova na wengine wote wanafikishwa The Hague.
 
Duh, hii report ni kiboko. Cant imagine kama kweli imepelekwa bunge la congress. Nafikiri kwa sasa hii report inastahili kupelekwa baraza la usalama la umoja wa mataifa, maana inaonyesha mkakati wa Kikwete wa kuvuruga amani ya nchi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Hili si jambo la kulifumbia macho.
Currently, a number of Tanzania Intelligence agents along with CCM activists are in Iran being trained on how to disrupt elections on the pretext of religious tensions in 2015. All these are paid for by Iran including construction of multiple mosques in Tanzania. Kikwete’s main goal is to keep his party CCM in power to protect his vast financial interests acquired through corruption. Iranians also discussed with Kikwete on how to obtain Uranium which corroborate with Wiki Leaks Uranium Report
 
Hata kama sio leo lakini iko siku yatatimia.Kwani ninaamini hata BABA WA TAIFA HUKO ALIKO ANATULULIA.
 
Miongoni mwa mambo ya kinyama ambayo yatanifanya nikumbuke utawala wa Jk ni KUTEKWA KUTESWA NA KUTUPWA MSITUNI KWA DR ULIMBOKA HALAFU GAZETI LILILOFANYA KAZI NZURI YA KUFICHUA NANI KAMTEKA NA KUTESA KUFUNGIWA BADALA YA KUWA CHANZO CHA KUSAIDIA KUWATIA HATIANI WALIO TENDA UNYAMA HUO.

Na amini kwa kuwa hakuna mtanzania zaidi ya mtanzani mwenzake na hivyo kuamua nani aishi au auwawe mwenyezi Mungu atalipiza hapa hapa duniani, kama sio leo basi kitambo kijacho maana yeye ndio hutufanya tuione leo na ikimpendeza hutuwezesha kuiona kesho na kesho kutwa.

Damu ya DR Ulimboka ina mlilia aliye ifanya itoke wakati mwenyezi Mungu aliiweka kwenye pande lake la nyama kwa mapenzi makubwa bila kuwekea mwili wake matobo au mifereji ya kuitiririsha chini.

​
Mkuu chama,
Naona sarakasi zingine zimeanza huku makandanda wanadanganya ovyo.
Hebu tusaidie tuelewe, sasa hapa uongo uko wapi? au wewe ndiyo wale wale mnaotaka kutuaminisha kuwa nyeusi ni nyeupe?
 
Halafu what a coincidence,wote wanyakyusa!ingekua wachagga pangekua hapatoshi hapa jf
Hivi hamuwezi kujadi mada bila kuweka udini au ukabila...je kwenye yale maandamano ya Arusha hakuna mchaga alie uwawa au wanao uliwa na serikali ya CCM ni makabila mengine tu...
 
UN ipo wapi wakati watoto/wakina mama na watu wasio na hatia wakiuliwa kila kukicha katika nchi yaafghanstan na pakistan na nyinginezo?
Hao UN wapo wapi watu wasio na hatia wakichinjwa myamar?

Miafrica bwana lazima aseme mtu mweupe ndio waone haki imetendeka?
Shame!
 
Sidhani sana kama watatusaidia wakati wenyewe ndo wadau labda watakapoona maslamu yapo wakati hiyohiyo sirikali ndo wanahusika nayo katika mikataba na makampuni ya nchini kwao hata hivyo mi ndo nimeona hivyo
 
Mkuu umenifanya machozi yanilengelenge, hata hivyo tusisahau na damu ya shujaa Daudi Mwangosi iliyomwagwa na mafia hawa nayo hukumu tutaishuhudia hapahapa dunia maana ni kitendo cha kinyama kwelikweli.
Miongoni mwa mambo ya kinyama ambayo yatanifanya nikumbuke utawala wa Jk ni KUTEKWA KUTESWA NA KUTUPWA MSITUNI KWA DR ULIMBOKA HALAFU GAZETI LILILOFANYA KAZI NZURI YA KUFICHUA NANI KAMTEKA NA KUTESA KUFUNGIWA BADALA YA KUWA CHANZO CHA KUSAIDIA KUWATIA HATIANI WALIO TENDA UNYAMA HUO.Na amini kwa kuwa hakuna mtanzania zaidi ya mtanzani mwenzake na hivyo kuamua nani aishi au auwawe mwenyezi Mungu atalipiza hapa hapa duniani, kama sio leo basi kitambo kijacho maana yeye ndio hutufanya tuione leo na ikimpendeza hutuwezesha kuiona kesho na kesho kutwa.Damu ya DR Ulimboka ina mlilia aliye ifanya itoke wakati mwenyezi Mungu aliiweka kwenye pande lake la nyama kwa mapenzi makubwa bila kuwekea mwili wake matobo au mifereji ya kuitiririsha chini.
 
Back
Top Bottom