Ulimboka, Mwangosi wamponza Kikwete UN

Ulimboka, Mwangosi wamponza Kikwete UN

..Taarifa kutoka Washington nchini Marekani zinasema Rais Jakaya Kikwete amelalamikiwa rasmi katika Seneti na wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu nchini, na kwamba masuala hayo sasa yatafikishwa kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu (UNHRC) kwa hatua zaidi.

Hapa ndipo unajua vyombo vingine vya habari Tanzania ni makanyanga tupu.

Hizi ni habari za mitaani ambazo haziisadii jamii zaidi ya kuipumbaza na kubweteka ikifikiri kama kuna kitu kinafanyika kuhusu serikali ya Kikwete wakati hakipo.

Hivi watu hawafahamu kama barozi wa Marekani nchini Tanzania ni Rafiki wa karibu wa Rais Kikwete na serikali yake na katika huyo, Marekani haiwezi kutoa tamko lolote bila kupata neno la barozi wake nchini Tanzania.
 
Uzuri ni kuwa Kikwete alikuwa na uchu wa madaraka kiasi kuwa akili yake ndogo ilishindwa kuona mabadiliko ya mawasiliano ya wakati huu. Watanzania wengi mno wameuawa kikatili na polisi. Wengi tu wanatesekea rumande kwa makosa ya mapolisi. Walemavu wengi tu wameuawa bila sababu na hakuna hatua ya msingi imechukuliwa. Pamoja na hao, kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu, "malipo ni hapahapa duniani" Mungu atamwumbua na tamaa zake kiasi kuwa hata aliyojilimbikizia hataweza kuyala. Point yangu ni kuwa Tanzania ina wasomi na watambuzi wengi tu kuliko Kikwete anavyofikiri. Hataweza kukwepa haya kwani picha zinaonyesha licha ya mengi tu ambayo hayajarecordiwa. Wazee hao hao ambao alikuwa anaspend kodi zetu kila siku kwenda kuwachekea watajamfungia mahali ambapo hataona mwanga wa jua maisha yake yote. Kama anataka mfano ajikumbushe tu kina Sadam, Ghadaf, na wenzie. Wako wapi leo? Kikwete you are in for a big trouble!
 
Ulimboka, Mwangosi wamponza Kikwete

• Kova: Sihusiki tena na suala hilo

na Waandishi wetu

KUUAWA kikatili kwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi na tukio la kutekwa, kuteswa kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, limechukua sura mpya ambapo sasa limetinga katika Seneti ya Marekani, Tanzania Daima Jumamosi limeelezwa.

Taarifa kutoka Washington nchini Marekani zinasema Rais Jakaya Kikwete amelalamikiwa rasmi katika Seneti na wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu nchini, na kwamba masuala hayo sasa yatafikishwa kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu (UNHRC) kwa hatua zaidi.

Mbali na mauaji ya Mwangosi na tukio la Dk. Ulimboka, Rais Kikwete pia amelalamikiwa kwa kufumbia macho matukio mengi ya kuteswa na kuuawa kwa raia pamoja na kufungiwa kwa gazeti la kila wiki la uchunguzi la MwanaHalisi, kutoroshwa wanyama hai kwa kupelekwa nje ya nchi na hatua ya polisi kutumia silaha za kivita kupambana na raia wasio na silaha wakiwemo wanafunzi wanaoandamana.

Ripoti hiyo ya wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu yenye kurasa 27, inatuhumu utawala wa Rais Kikwete kwa kukandamiza demokrasia kwa kutumia polisi na vyombo vingine vya dola.

Watetezi hao wa haki za binadamu, wamedai kuwa baada ya kufanikiwa kuingiza masuala haya ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika Seneti ya Marekani, sasa wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha suala hili linafikishwa Umoja wa Mataifa kwa kile walichokiita, kuiadabisha serikali.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopatikana, na pia kusambazwa katika baadhi ya taasisi za habari, suala hilo liko mikononi mwa Seneta Kerry, ambaye baada ya majadiliano katika Seneti, ripoti hiyo itapelekwa UNHRC.

Habari zinasema baadhi ya wajumbe wa Seneti waliofanikiwa kuona ripoti hiyo wamemeshitushwa na kile walichokishuhudia katika picha zilizoambatanishwa.

Aidha, ripoti hiyo pia imeeleza jinsi rushwa ilivyoshamiri nchini, ukandamizaji juu ya uhuru wa maoni na matumizi mabaya ya vyombo vya dola kudhibiti vyama vya upinzani na kutumia silaha za kivita kupambana na raia wasio na silaha.

Ripoti hiyo ya kuishitaki Serikali ya Kikwete, pia imelaani vitendo vya polisi kusambaratisha maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, walioandamana Julai 31, mwaka jana kupinga ukosefu wa walimu nchini.

Mgomo wa wanafunzi ulikuja baada ya walimu wa shule za msingi na sekondari kupitia jumuiya yao - Chama cha Walimu Tanzania (CWT) – kuitisha mgomo nchi nzima wa kutaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi zao, nyongeza ya mishahara na malimbikizo ya posho.

Nyaraka zilizowasilishwa na wanaharakati hao, zimeambatanishwa na picha zinazoonesha namna Jeshi la Polisi lilivyohusika kuuawa kwa Mwangosi, picha mbaya ya maiti ya mwanahabari huyo, na namna Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alivyokuwa akishuhudia askari wake wakimsulubu mwanahabari huyo kabla ya kufunga kazi kwa kumaliza uhai wake.

Kadhalika, kumeambatanishwa picha zinazoonesha maiti za watu waliouawa wakati wa maandamano huko Arusha, na ile inayosadikiwa kutokea kule Songea. Picha nyingine za kusikitisha ni zile zinazoonesha askari zaidi ya watano wakimdhibiti mwanaharakati mmoja katika maandamano, na umati wa wanafunzi wa shule za msingi wakiandamana, huku nyingine zikionesha askari mwenye silaha ya kivita akimsindikiza mwanafunzi wa kike mwenye mfuko wa madaftari.

Tangu mwaka 2005 ambapo masuala mazito ya rushwa yamekuwa yakiibuliwa, ikiwamo ununuzi wa rada feki, wizi wa fedha za umma kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mkataba tata wa Richmond, ukusanyaji wa kodi, utoroshwaji wa wanyama hai, wizi wa nyara za serikali, ikiwamo pembe za ndovu, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituhumu serikali kushindwa kuchukua hatua.

Vilevile, wananchi wamekuwa wakituhumu Serikali ya Kikwete, kukumbatia wezi wa fedha za umma katika halmashauri za miji na wilaya, uporaji wa ardhi unaofanywa na makampuni makubwa ya ndani na nje ya nchi.

Jana, Tanzania Daima Jumamosi haikufanikiwa kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu kuzungumzia iwapo serikali ina taarifa juu ya jambo hili kwa kuwa simu yake ilikuwa ikiita muda wote bila kupokelewa.

Kova ajivua

Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova jana ametangaza rasmi kujivua katika sakata zima la kuchunguza kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka.

Aidha, Kova pia amekanusha madai ya kuunda tume kuchunguza suala hilo, akitaka asiulizwe jambo lolote, huku akisukuma tukio hilo kwa wakubwa wake.

Juzi, Kamanda Kova aliliambia Tanzania Daima kwamba, jana angeweka wazi suala hilo ili Watanzania wajue kilichojiri kuhusiana na kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, jambo ambalo limetikisa anga, likiwemo lile la kukamatwa kwa raia wa Kenya, Mulundi anayedaiwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo, kinyume na matarajio ya wengi, jana Kamanda Kova aliruka kimanga na kudai kwamba wenye uwezo wa kulitolea maelezo ni wakuu wake wa kazi, kwa maana ya Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kuhusu kuundwa kwa kamati ya kuchunguza utekaji huo, Kova alisema kilichofanyika wakati huo ni kuundwa kwa jopo la uchunguzi ambalo taarifa zake hazina ulazima wa kutolewa mbele ya jamii zaidi ya kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa kile walichokibaini.

Alisema baada ya kukamilisha kazi yake, alipeleka jukumu la kupeleleza sakata hilo katika ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini (DCI) ambayo ndiyo yenye jukumu la kutoa maelezo.
dawa ya yote haya,kitu cha kwanza ni kuitoa ccm madarakani,hapo ndipo tutaanza kuona faida ya uhuru,na wezi wote ndio itakuwa mwisho wao,maana ccm ndio inawalinda wezi a mafisadi.
 
Ha, ha haa...mwiteni na chama, idadi ya majuha watatu ikamilike!

Vipi umeishampeleka junior shule?

Mkuu chama,
Mnafiki ni chakula ya mamba huyu jamaa alisema yeye hana chama chochote cha siasa.

Tatizo nyie watu wa kaskazini kila mmoja anajiona ana hisa Chadema.
 
Last edited by a moderator:

- Hamna lolote hizi ni hadithi za Alfu lela ulela, USA wameshindwa China na wao wenyewe kila siku Polisi wao wazungu wanawaua weusi bila sababu leo wana ubavu kuingilia siasa na utawala wetu? I mean huku Bongo ukisema anything watu wanakubali tu hata kama hakina ukweli kama hii habari.

- USA wanahitaji kujipima wenyewe kwanza and waende China ndio waje bongo

le mutuz
 
Binafsi siamini kama Amnest International au UNHCR ndio watakao leta mabadiliko katika nchi ya Tanzania. Kama ndivyo wengi tunavyoamini tuna safari ndefu ya kuyaona mabadiliko ya kila mmoja wetu kutetea na kujua haki zake. Siyo kweli hata kidogo senete ya Marekani ndiyo itakayomfanya Kikwete na Serikali itekeleze wajibu wa kulinda haki na utu wa raia wake.

Suala kubwa ni sisi wenyewe watanzania kila mmoja kwa nafasi yake ambao tunaelewa kila kinachofanyika, tunawajua wote wanaua, wanaosababisha mauaji lakini hata tukiambiwa kutoa ushahidi hawako tayari. Mapinduzi ya kweli ya haki zetu lazima yatokane na sisi wenyewe.

Jiulize, Amnest International, UNHCR, au senete ya Marekani imefanya nini Syria, Sudan, DRC na kwingineko ambao kuna mauaji makubwa ya raia wasiokuwa na hatia. Tuamke watanzania na kuacha projo na usahabiki katika mambo ambayo yanahitaji majibu ya msingi yenye kujenga na kulete matumaini kwa waliokata tamaa ya kudai haki yao. Wakati ndio huu, acheni porojo za Amnest n.k
 
Hili gazeti wanahisi kila habari ni ya kisiasa
 
Kwa hiyo wafuasi wa Chadema mnaamini UN ndiyo wataleta mabadiliko Tanzania.
 
Vipi umeishampeleka junior shule?

Mkuu chama,
Mnafiki ni chakula ya mamba huyu jamaa alisema yeye hana chama chochote cha siasa.

Tatizo nyie watu wa kaskazini kila mmoja anajiona ana hisa Chadema.
Naona asubuhi asubuhi umeamka kuiteetea serikali ya kikwete na ccm yake lakini ujue ni kitanzi tu.....
 
Ona majibu ya KOVA hii maana yake ni kuwa hakuna kitu kesi imeisha, walikuwa wana muunga mkono Dkt. Ulimboka tayari wamesain barua za kutii sheria na kurejea kazini. Unategemea nini kingine hapo? Leo kamanda Mkubwa wa Polisi ambaye alikuwa kifua mbele awali kutangaza jitihada za jeshi la polisi kupata ukweli wa kilichotokea kwa Dkt Ulimboka, leo amekuwa bubu na kudai suala hili liko mikononi mwa wakubwa wake. Je nini hasa Kamada Kova alichomaanisha kwa kusema kuwa sakata hilo lipo kwa wakubwa zake sasa. Ina maana ameambiwa kuwa usiendelelee kuliongelea kwa kuwa ukweli tayari wanao? au ameonekana kuongea tofauti na anavyoagizwa?
Tafakari kwa makini ili kupata majibu ya ukweli.
 
Kwa hiyo wafuasi wa Chadema mnaamini UN ndiyo wataleta mabadiliko Tanzania.
Mabadiliko yataletwa na watanzania wenyewe lakini UN angalau watapunguza safari za Vasco dagama maana zina tuumiza sana watanzania...
 
Naona asubuhi asubuhi umeamka kuiteetea serikali ya kikwete na ccm yake lakini ujue ni kitanzi tu.....

Naona wewe bado umelala na wewe ukiamka utaanza kumtetea Dr Slaa. Nasikia safari hii mtapewa msaada na Nato.
 
Huku ni kufilisika na kukosa cha kuandika, hii taarifa ipo apa tangu jana na tena leo kutwa ilitupiwa hapa tumeijadili sana, mnatuchosha na kubadili heading halafu ndani kitu ni kile kile

Kwani wewe una kazi hii hii ya kujadili?
 
Huku ni kufilisika na kukosa cha kuandika, hii taarifa ipo apa tangu jana na tena leo kutwa ilitupiwa hapa tumeijadili sana, mnatuchosha na kubadili heading halafu ndani kitu ni kile kile
Wewe bwe.ge kweli,kwani lazima u comment? pita kule acha wenye mawazo Chanya wachangie,muone mipovu tu inakutoka.
 
Corruption and other controversiesKikwete's presidency has been marked with wide range of corruption, some of which happened during the presidencies of his predecessors. Some of his supporters claim that to be a sign of transparency that was brought in by Mr Kikwete. Other cases, like deaths, have also been brought up such as Tanzanian police killing people on Tanzanian streets and getting away with it. Some of the leading known corruption scandals are:

  • BAE Security Radar Scandal
The Tanzania government agreed to buy an overpriced radar, which it cannot maintain now. It came to be known later that more than a third of the total purchasing price was paid to a middleman of British citizenship to secure the contract. Also based on an Interpol report, one government minister had siphoned more than £1m to his bank account in Jersey. After many international legal actions, BAE was ordered by court to pay £30m to Tanzanian government.[SUP][2][/SUP]

  • EPA Scandal
The scandal consists of fraudulent payment of about TSh133 billion ($116 million) made by the Bank of Tanzania to 22 companies in the financial year 2005/06 involving the repayment of the country's external debt.[SUP][3][/SUP] After the transactions became wildly known, the President sacked the Central Bank Governor and asked "kindly" those who looted the national treasury to return the money. A few months later, according to a government pronouncement, nearly half of the money (Tsh 60 billion) had "mysteriously" found its way back into state coffers. The Attorney General and the Inspector General of Police have refused to disclose the names, pleading for patience because the investigation is still going on. So far not all of the money has been returned and the government has neither released the culprit's names nor taken any legal action against them.[SUP][4][/SUP]

  • Kiwira, Meremeta and other mining related scandals
Government officials in the previous administrations had taken advantage of the privatization policies and privatized national mines to themselves. A good example is the Kiwira mines, which were privatized to two individuals: the president and his minister for Energy and Natural Resources. The President of that time, Benjamin Mkapa, was rather "smart", registering his shares as AnBen Company; AnBen standing for first names of his wife Ann and himself Benjamin.[SUP][5][/SUP]

  • Richmond, Dowans Electricity Scandal
In 2006, Tanzania faced a serious crisis in electricity supply and, as an emergency measure, Richmond was awarded a contract to supply generators to provide 100 megawatts at a cost of TShs 172 billion. The generators failed to arrive on time and, when they did, they did not work as required. The pipeline was never built and the generators were provided by another company. Under part of the contract, however, the government agreed to pay some $137,000 a day regardless of the amount of electricity provided. Opposition MPs began to smell a rat and the House of Assembly set up a Select Committee to investigate the whole saga under the chairmanship of the ruling CCM Kyela MP, Harrison Mwakyembe. The committee worked diligently and eventually came up with a 165-page report. Parliamentary findings showed the Prime Minister(Edward Lowassa) to be involved in awarding the contract to nonexisting US-based company, and the Prime Minister resigned. However, the Tanzanian government had to keep the contract and keep paying a non-existing company $137,000 US a day without any power being generated. And now Tanzanians are faced with the problem of repaying the debt, with the government increasing the electricity bill by 40% [SUP][6][/SUP]

[TH="bgcolor: #cccccc, colspan: 1"]Issue/ Event[/TH]
[TH="bgcolor: #cccccc, colspan: 1"]Date of Event[/TH]
[TH="bgcolor: #cccccc, colspan: 1"]Cost to the Nation[/TH]
[TH="bgcolor: #cccccc, colspan: 1"]Government Explanation[/TH]

[TD="align: center"]1999[/TD]
[TD="align: center"]£28 million[/TD]

[TD="align: center"]2005–2006[/TD]
[TD="align: center"]US$116 million[/TD]

[TD="align: center"]2000–present[/TD]
[TD="align: center"]Unknown[/TD]

[TD="align: center"]2006[/TD]
[TD="align: center"]US$150 million (TSh172 billion)[/TD]
Also, President Kikwete has been blamed for choosing his friends to the cabinet, a result of which he has no power to condemn them for their irresponsibility. The example of two consecutive bomb blasts at Mbagala and Gongo la Mboto arm base respectively in 2009 and 2011 where General Mwamunyange as well as the defense minister, Mwinyi, were in charge, but they insisted that it was not their fault for the blast and denied to brief the country about the reason for the blasts. The President himself kept praising to the two officials that they are working to secure a country something that raised anger among the victims of blasts.
Although in the past two years of Kikwete's presidency, a remarkable 1,500 new secondary schools have been built and a new 40,000-student science university has started being built in Dodoma, central Tanzania, the quality of these new schools are very poor, (no teachers, no desks, etc.), and there is still a lot that needs to be done. But these successes have led the United States government to grant Tanzania US $698 million under the Millennium Challenge Account assistance program, the UK government US $500 million for education, and the New York based Africa-America Institute (AAI) to award Tanzania the Africa National Achievement Award in September 2007 in New York.
President Kikwete launched a national campaign for voluntary HIV/AIDS testing in Dar es Salaam. He and his wife, First Lady of Tanzania Mama Salma Kikwete, were the first to be tested.[SUP][7][/SUP]
He was elected as Chairman of the African Union on January 31, 2008 at an AU summit in Addis Ababa.[SUP][8][/SUP] His first notable success as AU Chairman was to help bring a two month political crisis in Kenya to an end by brokering a power-sharing deal between Mwai Kibaki and Raila Odinga. He was also one of the first to criticise Robert Mugabe's regime at the most recent summit.
 
Isango ni mganga njaa, anaokoteza habari za kusikia aka umbea aka hear say samahani kwa spelling anatuletea hapa na kujifanya ni uchunguzi
 
Back
Top Bottom