.....Mgomo wa wanafunzi ulikuja baada ya walimu wa shule za msingi na sekondari kupitia jumuiya yao - Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuitisha mgomo nchi nzima wa kutaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi zao said:
Sijui serikali ya kikwete inafikiria nini juu ya madai ya waalimu.Serikali imeendelea kuwapuuza Walimu,mfano;Mwalimu aliyemaliza shahada ya ualimu wa Physics na Mathematics anaanza na mshahara wa TGTS D,lakini mtu aliyemaliza uhandisi (Engineering),akakosa kazi ya uhandisi,akaomba ajishikize kwenye ualimu,afundishe Physics au Mathematics,yeye huanzia daraja la juu yaani TGTS E.Kwanini serikali inawadharau sana walimu? Mishahara yao midogo,madaraja hayapandi kwa wakati,madai yao yanacheleweshwa mno na mengine hayaripwi kabisa. Mwanzo ilionekana kama migomo ya walimu sio tishio,sasa walimu wameerevuka,wamegundua kuwa kumbe wanayo silaha,nao ni wanafunzi.Wakati ule waliandamana wanafunzi walio DSM tu.Wanafunzi wote walio katika shule za walalahoi-shule za serikali wanafundishwa na walimu kuwa,ukitokea mgomo wa walimu,wanafunzi waandamane na waihujumu miundombinu yote ya CCM.Wakati umefika kwa serikali kurudisha usawa katika vipato kwa waajiriwa wake wote,wakiendelea na dharau kwa waalimu,wajiandae kushuhudia maandamano makubwa ya wanafunzi kuanzia chekechea mpaka form six,maandamano yatakayoambatana na vurugu.Kwa uzembe wa polisi,waziri na IGP watafikishwa kwenye mahakama za kimataifa.ACHENI KUWABAGUA WAAJILIWA WA SERIKALI!