Nominee
JF-Expert Member
- Sep 5, 2017
- 459
- 1,240
Nakumbuka Baba yangu mzazi alikuwa anasumbuliwa na saratani ya ngozi.Tulifanya jitihada za kila namna kuokoa maisha ya baba yetu mpendwa,tulizunguka hospitali mbalimbali ila mwisho wa siku tukaelekezwa tuelekee hospitali ya Ocean Road Dar-es-salaam.
Ndugu walipambana kuchangishana hela ili mzee atoke mkoani aende Dar kwa matibabu.Tulifanikiwa kufika Ocean Road na matibabu ya mionzi(Radiotherapy na Chemotherapy) yalianza.Ila mwisho wa siku tuliambiwa kuwa kwa hali aliyonayo mzee hawezi kupona tena.Kwahiyo akawa anapatiwa tu dawa za kutuliza maumivu huku akikisubiri kifo chake.Ni nyakati mbaya sana za maisha ya mzee wangu.Hatimae baada ya miezi takribani nane baadae mzee akaaga Dunia.
Nililia sana,ila hakuna namna zaidi ya kumuachia Mungu.Vijana tujitahidi kufanya check-up za mwili mara kwa mara,magonjwa mengine huwa yanaibuka tu ghafla yakiwa katika terminal stage na hautoweza kujitibu.