Ulichokitokea jasho unakionea uchungu kuliko utajiri wa kuanikiwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
elin_uni.jpg
Pacific-Coast-News.jpg

Jumba alilonunua Ex wife wa Tiger Wood kwa $12 million


Courtesy-of-With-Leather.jpg


Jumba hilo amelibomoa na kusafisha kubaki uwanja mweupe kupisha ujenzi wa jumba analotaka
[h=3]Bofya hapa kupata kinagaubaga zaidi Tiger's ex destroys $12 million mansion[/h]
Twapata funzo gani hapa Wanajamii Forums?

Kwa wengi tunaweza kujifunza katika tukio hili, mali usiyoitokea jasho huna uchungu nayo. Kama angekuwa na akili kidogo kama yangu ambapo wengi wametoa comments za aina ya mtazamo wangu, ingekuwa na manufaa zaidi kama nyumaba hiyo ingebaki na kutafuta kiwanja kingine cha kujenga jumba la kiwango anachotaka. Lakini kwa kuwa ana akili zaidi yangu, hakuona umuhimu wa kuuza jumba hilo na kutafuta kiwanja kingine ili ajenge jumba analotaka kwa kuokoa $12 million.

Kwa uamuzi na utekelezaji aliofanya sijui kwa kushauriwa au kutoshauriwa ni sawa na kwamba ametumbukiza dampo $12 millioni kitu ambacho hata matajiri wakubwa hawathubutu kufanya hivyo.

Pesa aliyopata $100 millioni kutokana na talaka kwa Ex husband Tiger Wood imemchanganya akili kiasi cha mimi kumkumbuka yule tajiri wa Arusha aliyekuwa anauza madini ya Tanzanite alipokuwa anakaa chumba cha juu cha hoteli na kumwaga mapesa nje kupitia dirishani ili watu waokote wakati kuna taratibu ambazo kama ana uchungu na maskini angezifuata na zingefanya kazi vizuri zaidi.
 
Funzo hilo si umeona wengi walipata mali kwa kurithi mambo yanavyo kuwa?jambo sio wote lakini wengi wao huwa ndio hivyo hivyi kama elin wa gävla kommun,
tiger sasa hato chumbia sweden tena hahahah
 
Funzo hilo si umeona wengi walipata mali kwa kurithi mambo yanavyo kuwa?jambo sio wote lakini wengi wao huwa ndio hivyo hivyi kama elin wa gävla kommun,
tiger sasa hato chumbia sweden tena hahahah

Laiti angeomba ushauri walao kuokoa nusu ya hizo, maana akili yake imeishia kujenga tu anachokitaka bila kujali thamani ya pesa aliyonunulia hiyo nyumba.

Nawea kutafsiri kwamba matatizo aliyoyapata Tiger Woods huyu mwanamke alisababisha ili kuzusha songombingo ili ajitajirishe kutokana na talaka.
 
Hamna cha bure, alichanika msamba akamzalia watoto.....

Acha ujinga kwani mtoto ni wa baba pekee au wote wawili wana haki sawa! Mi naona kama huyo mwanamke kajidhalilisha yeye na jumuiya ya wanawake!
 
You view this act from a poor man's/woman's perspective ndio maana umetahayari lakini kwa matajiri hilo ni jambo dogo sana;tajiri mmoja huko India [ Mukesh Ambani] alimnunulia mkewe ndege kubwa [custom built by Boeing] kama zawadi ya kuzaliwa kwake!!
 
Back
Top Bottom