Tabia ya wanaume kulelewa na mabinti ikomeshwe

2025DG

JF-Expert Member
Jan 30, 2023
508
1,425
Kijana wa kiume.

Ewe mwanaume.

Nakuita tena wewe mwanaume mwenye sifa zote za uanaume.

Inakuje umeamua kukubali kuudumiwa na mwanamke kwa kila kitu,jamani inasikitisha sana.

Mwanaume leo hii unabadilisha channel kwa tv aliyonunua dada wa watu kwa kubangaiza ,unakaa kwenye sofa na kulala kwa kitanda chenye jasho la mtoto wa kike.

Mjini usumbufu mkubwa wa Ist,nadia ,carina kwa gari alilonunua dada wa watu mara baada ya kuchukua kamkopo kake ka Tsh million 12.

Inakuaje mtoto wa kike inafika hadi hatua unaenda kanisani kufunga ndoa , sherehe ya Harusi michango yote hadi kiwanja cha zawadi unachopewa na wakwe ni nguvu na juhudi za huyo dada.

Mwanaume badilika Acha kulelewa.

Unashindwa kusaidia hata mama yako Elfu 10 kwa kuwa tu umekuwa kama umeolewa na huyo dada maana hauna mamlaka na chochote japo unavimiliki.

Hauna tena sauti iliyobaki kwako ni ndevu na kuvaa suti tu.

Nawasilisha.
 
IMG-20230201-WA0072.jpg
 
Nani wa kuikomesha?
Wanawake wako desperate, vivulana viko nyolonyolo.
Unategemea nini?

Back
Top Bottom