Ulianzaje kukaa gheto?

Wakuu mambo vipi,,Leo naomba tufanye kushare kila mtu jinsi alivyo chomoka Nyumbani kwao..Hii itatoa hamasa kwa wale waliokua nyumbani na kuogopa kuhama na kuanza kujitegemea.

Janga hili linawakumba wana vyuo wengi,unakuta mtu anamalza chuo akiwa labda ana 25 then anarud nyumbani ,mbaya zaid anasubir kazi..alaf kazi zenyew haijulkani utapata lini.

Hii inapelekea wana wengi kua na fear ya kuchomoka home...Kiukwel hali ya kukaa hom inakata sana..Mzee unakuta anachomoka anakuachia mikazi flani hivi howcome.

Ukija upande wa MMU ndio mambo yanakua sio mambo...mtoto anataka aje kukusalmia unaona soo kwasababu upo nyumbani..inakata sana hii

Tukija kwenye maisha ya kujituma tu..sometime unakosa hamasa ya kupambana kwasababu ugali wa bure,unalala bure,kila kitu bure..hii inakua ngumu kuwaza kwa mapana ili kuanza kukamilisha dream zako..

Pia inakata sana..pale wanao unakuta wapo na mageto yao..lakin wewe kwako ni tofauti.

Sasa naomba kila mmoja aseme alichomokaje home na kuanza kukomaa na maisha..Achilia changamoto zake kikubwa hapa ni kusepa kwa maza..

##Mimi binafsi geto nilianza kukaa soon nilivyoingia chuo,,,nakumbuka nilipata room ya elf 50 nikaanza nayo kibish,nikanunua bed ya 150, 5 kwa 6,nikatafuta feni tu ya elf 35..si unajua joto la dar..nikaingia k.koo nikavuta subwoofer ya elf 75 tu...geto bila mziki sio geto ni choo,kujichek mfukoni boom likawa lishakata...basi nikaendelea kuishi geto hadi namalza chuo geto likawa limesheheni tu...
sasa baada ya kumalza chuo. Ndio nikarudi hom..ujinga niliofanya ni kurud hom na baadhi ya vitu niliviuza...Kasheshe ndio ipo saiz..wakuu hom akili inalala,,vibe yote hakuna ,hapa ndio najichanga nichomoke tena nirud geto nianze kupambana..hop ndan ya huu mwaka nitakua nishasepa hom kwa mara nyingine.

Sasa share kitu basi nawewe..

#Nini lilikusukuma usepe home?
#Kitu gani kilikupa mzuka wa kuanza kukaa geto?
#Vipi ulianza kukaa geto ukiwa na kazi au kibishi tu?
#Maisha yalkuaje since day one?
#Je ulienjoy uamuzi wako wa kusepa home?
#ulianza kununa vitu gani vya msingi na kuanza kuishi geto
#Una lipi la kuwaambia wana walioko home hadi leo wakiogopa kukaa geto kisa hawana ajira bado?

Karibuni wakuu..

View attachment 878774
Mkuu umenichekesha sana. kuna jamaa nilifikia kwake Dar duh yalikuwa majanga. Jamaa ana kitanda ila hakina godoro katandika shuka juu ya chaga.nilikoma kwa ubahili wangu. palipokucha nilibeba begi nikaelekea lodge kufanya booking ya jioni nikaacha begi nikafuata mishe zilizonileta.
 
Aise nakumbuka mwaka 2009 ,...nilivuoanza kukaa gheto kwangu nikiwa na miaka 21 tu ...nikiwa na kitanda cha 3 kwa 6 na sufuria 3 ...hapo nikiwa nimepanga

Mshua hakufaruhia kabisa uondokaji wangu , alizani nitafeli maisha ...haikuwah kutokea ...mpk leo

pamoja na kastool ka plastic ...mdogo mdogo na jiko la mafuta maisha yaakaanza kusonga na nilikuwa ugenini

Nilikuwa na kishughuli kilikiwa kinaniingizia sh 150,000 kwa mwezi ...

mpk leo namiliki mjengo wangu mkubwa kabisa vyumba 5 master bed room 2 .....yaaani nipo full

Maisha bwana sio mpk kuwa na hela nyingi ni kuamua tu...kwa mlio mwanza karibuni vijana mje mjifunze kwangu

Tafuta marafiki waliofanikiwa acha kukaa na marafiki walioshindwa hawawezi kukupa kabisa future
 
Back
Top Bottom