Siku ya kwanza kuhamia kwangu, nakumbuka nililala chini kwenye tiles, nilikuwa nimeshafanya usafi nikasogea kula bata maeneo ya sinza mpaka saa 8 usiku, nikiwa nnarudi home kwa wazee nikajisemea ngoja nikakague tena kwangu, hapo hamna kitu nikafika nikaangusha sitting room, kuanzia hiyo siku sikuwahi kulala tena home
Kesho yake asubuhi nikazama game nikanunua sofa bed kwa 395,000/= nakumbuka nilikuwa nnalitamani sana afu likawa kwenye ofa nikajilipua, sahani, frying pan, sufuria na glass, nikarudi huome nikang’oa TV yangu, music system + king’amuzi na ki fridge kidogo nilikuwa nnatumia chuo nikabeba na kimeza cha kishkaji cha kuwekea Tv nikamuaga mzee mimi ninasepa nahamia sinza, akasema poa nikapita mwenge nikachukua jiko la gas + mtungi
Hii siku ya pili nikaanza na asset zangu zilikuwa ni sofa bed, kimeza cha kuzushi cha tv, tv, music, jiko la gas, mtungi na vyombo vya jikoni...
Kwa miezi miwili mfululizo nilikuwa nnalala sitting room
Mkuu Wachek wale madalali wa instaWANAGETTO NISAIDIENI NIPATE CHUMBA MAENEO HAYA MAANA MADALALI WANATUKAMUA SANA
-Anayejua chumba maeneo ya Mabibo hostel,sinza,changanyikeni,survey,makongo juu,ubungo external,mwenge na riverside....
Budget yangu ni cha 40k au 50k kwa mwezi...
Tusaidiana na wanaotafuta vyumba maeneo hayo pia...
Nipm nipigie au nitext kwa namba 0759432654
PoaMkuu Wachek wale madalali wa insta
[emoji119][emoji119] mwanangu unapend music system kama mim[emoji16][emoji16]Siku ya kwanza kuhamia kwangu, nakumbuka nililala chini kwenye tiles, nilikuwa nimeshafanya usafi nikasogea kula bata maeneo ya sinza mpaka saa 8 usiku, nikiwa nnarudi home kwa wazee nikajisemea ngoja nikakague tena kwangu, hapo hamna kitu nikafika nikaangusha sitting room, kuanzia hiyo siku sikuwahi kulala tena home
Kesho yake asubuhi nikazama game nikanunua sofa bed kwa 395,000/= nakumbuka nilikuwa nnalitamani sana afu likawa kwenye ofa nikajilipua, sahani, frying pan, sufuria na glass, nikarudi huome nikang’oa TV yangu, music system + king’amuzi na ki fridge kidogo nilikuwa nnatumia chuo nikabeba na kimeza cha kishkaji cha kuwekea Tv nikamuaga mzee mimi ninasepa nahamia sinza, akasema poa nikapita mwenge nikachukua jiko la gas + mtungi
Hii siku ya pili nikaanza na asset zangu zilikuwa ni sofa bed, kimeza cha kuzushi cha tv, tv, music, jiko la gas, mtungi na vyombo vya jikoni...
Kwa miezi miwili mfululizo nilikuwa nnalala sitting room
Ulihama kibingwa sana mkuu..hongera sana..
Wakuu kama nilivoaidi sitwaangusha, ndani ya mwezi mmoja geto ndo lilivyo sasa hiviView attachment 1241489View attachment 1241491View attachment 1241492View attachment 1241493
Mkuu ndo huyu uliyekutana nae baadae akiwa anauza nyanya,kachoka ile mbaya?Dah mi geto nlianza kukaa baada ya kukosa chumba chuo mwaka wa kwanza,basi nikawa sina jinsi zaidi ya kupanga,basi nkaanza na kitanda na feni tu then nkampa mwenye nyumba hela ya miezi sita,but siku nahamia tu nkawaza je ntakaa kujitegemea maisha yangu yote?au ntapanga then mwisho wa siku ntarudi home?kurudi home kiukweli nilikataa hivyo nikaanza hatua ya kwanza ya kujiandikisha masomo ya jioni chuoni(evening class)basi week ya kwanza nikaanza kitabu but huku mchana wakat nipo geto nkawa natoka kutafuta channel za kazi za kufanya,basi nkapata boda boda kwa siku 15 kwa mkaaba wa mwaka,nkawa napiga kila siku then jioni naingia chuo usiku mpka saa 7 ndo nalala huku nikiwa nahakikisha lazima nilale na 30 mpka 20,basi nilifanya hivyo kwa mwaka mzima huku boom likiwa linaingia na huku nikiwa nnaingiza hela hyo mpka zaidi per day,mwaka wa pili nakumbuka ndo nipo na mke wangu maana tulitoka ote high school na tukawa chuo kimoja hivyo mwaka wa 2,hela yake ya hostel akaitoa na mm nikatoa mara mbili ya ile akawa anazungushia kwenye biashara huku akiwa amehamia ninapokaa wakati huo nmehama zangu geto sasa nnachumba na baraza yenye kila kitu ndani.Basi biashara yetu ambayo tulikuwa most tunaifanya online pamoja na maofisini huku yeye akibase kwa vitu vya wanawake huku na mimi nikibase kwa wanaume basi nkawa nawasambaza watu na boda boda mchana wakati huo piki piki ikiwa yangu tayari.basi miezi mi 3 baadae dem akanasa mimba,so alivyoenda kwao likizo kumbka kwao nlikuwa sifahamiki,dah maza wake akashtuka kuwa dogo anamimba aliwaka kichizi na walimtisha mno ,huku wakitaka niende kuchukua mzigo wangu(means)mke wangu
Kweli jamaa ana stories nyingi za uongo na humo hujifanya mwema sana. Anza na story yake na baba mkwe,njoo na story yake ya kuachana na demu wake na baadae kumkuta anauza nyanya.Muongo huyu jamaa
Dohhh.. Hatari mzeeeAisee hatari,soon baada ya kumaliza chuo way back 2014 nikarudi home nikajaribu mishe za maskani ikawa chenga na maneno mengi ya maudhi,nikauza pc nikazama Dar kuna mwana akanipokea ,baada ya mwezi wa kutafuta ramani mshikaji kaniunganisha kazi alipokuwa anafanyia salary 270,000 per month nikapiga kaz by septemba 2015 kibarua kikaota nyasi kampuni ilifilisika mfukoni nina 1,200,000 jamaa akasema saiz kila mtu aangalie namna ya kujisaidia
Nikapiga akili mambo magumu had pesa ikakata hiyo ni may mwaka uliofuata,nikarudisha mpira kwa kipa tena kwa nauli ya kusaidiwa na mdau tuliyefahamiana tuu.Maskani michosho mingi kuna siku nikagoma kufanya ishu fulani fulani wakanitimua nikapanda gari hadi swax,alikuwepo mwana fulani home nilitoka na 60,000 baada ya kulipa nauli nikabakiwa na 40,000 hapo hakuna anayejua nikikokwenda.
Nikamkuta mwana akanipokea nikamwambia nimekuja kusaka life kazi yoyote ntafanya.jamaa akasema utakula ila pia kulala tafuta geto,ndo ikawa mara ya kwanza nimeanza kupanga hiyo ni june 2016 hapo godoro ni mabox mimi na ndoo moja tu ndo kiti hicho.Asubuhi nawahi kwenda kwenye vibarua jioni nakula kwa mshikaji nachagua nikipata.Baridi yote iliniishia maana nilikuwa na shuka tu na sakafu ya baridi,mwezi wa kumi baada ya kudunduliza nikanunua godoro na vyombo vichache vya kuanzia maisha.Ilifika kipindi hali ikawa ngumu sana sometime hakuna kazi unashindia miwa na bumunda tuu huku unawaza kodi na bili za maji na umeme,kodi ilikuwa 12,000 umeme 1000 na maji 2000 jumla 15,000 lakini inasumbua.Piga sana kazi za zege na saidia fundi kutwa 5000 ila ndo hivyo lazima maisha yaende
By Novemba 2016 Mungu saidia kuna mwana akanifanyia connection ya kazi za ukandarasi ambazo ndio fani yangu from there hadi leo hii ndio nilipata nafuu ya maisha japo ni kazi za muda zinaishia zinakuja tena so wanaofanya kazi kwa wakandarasi wanaelewa.Pamoja na kwamba sijatoboa niko kwenye nafuu maana nina familia na nina boma siku yoyote ntahamia kwangu
Ila kitu sitosahau nilipata tabu sana na ishu iliyonisikitisha nilipata demu nikamketa geto baada ya kuona jinsi lilivyochoka hakutaka kukaa na kuanzia hapo akaniblock.Wakati fulani pia nikiwa kwenye ukidampa kuna demu alinielewa but wenzie walimponda eti ntampa pesa gani wakati nashindia ukidampa nae akasepa nikaacha kabisa kutokea mademu,,
Sasa unaogopa niniNna mpango wa kuchomoka home mwakani[emoji848]
Dah ila naogopa kishenzi
Kwa sisi watoto wa mwisho inakua ni mbinde sana kuchomoka home, ila mwakani lazima kieleweke tuAsante kwa uzi huu coz hapa nlipo ndo nipo kwenye process za kuhamia geto from home, sasa tatizo mshua amenigomea kuniruhusu.. kauli aliyonipa ni kuwa "mim kama baba sitakuruhusu ila wewe fanya maamuzi yako ukiamua nenda ukiamua baki. nenda kale kesho unipe majibu.. "
kiukweli home wananitegemea kwa shughuli mbalimbali (mm ni mtoto wa mwisho) ila sema mm ninamishe zangu na naona kama vile sishiriki kikamilifu nyumbani
[emoji16] [emoji16] [emoji16]Daaah!!nimekumbuka mbali Sana,Yani nimeanza gheto na godoro limechoka Yani unalala mbavu zinauma hadi unaamua kuamka usingizini upumzike kidogo halafu unarudi Tena kulala!!
[emoji16] [emoji16] [emoji16]Mambo ya geto bana,,, juzi kuna demu kaja amepika tule geto,, nakuja kugundua kumbe nna kijiko kimoja tu,, vingine vyote nilikua navimwaga tuu wakt naosha vyombo[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hii thread inanihamasisha mpango nnaotaka kuufanya mwezi huu....nimeahirisha kupanga kwa miezi mi3 nikiwa naweka kwanza biashara yangu vizuri
Now nipo fresh...biashara inaenda nna mpango mwezi huu tar 30 nichomoke
Sema napo km nnaanza kuahirisha...nataka pia hela ya mwezi huu niiweke kwenye biashara
Ila kiukweli kabisaa nmeamua mwezi huu kusepa
Sofa lipo tyr
Kitanda tyr
Subwoofer lipo tyr
Vyombo kila kitu tyr
Bado carpet tyuuu
Ukikaa gheto akili inakua
Duu bili za umeme heri ukae na watu wasio na matumizi makubwa buku 3 unatumia mwezi mzmaItakua bill za umeme[emoji16]
Mambo sio mabaya mkuu..nakukumbukaNilihamasika kupanga kupitia thread hii na still bdo nahamasika kuongeza vitu ndan
Japo sijafika nnapotaka lakini kesho yangu naionaView attachment 1255624