Wayback 2003
Sina life ,Mimi ndiyo mtoto wa kiume ukizingatia bi mkubwa Hana maisha.
Anaishi chumba kimoja.
Ikabidi ni drop kwa bibi ambaye hakuwa ndugu zaidi ya ubibi wa dar haha SI mnaujua ulee wa bibi bibiii.
Nikawa na chill pale ki bishi bishi, siku nyingine nikienda mara mlango umefungwa mara naambiwa nirudi nilipotoka hahaha walikuwa wanalala saa 1. Na Mimi muda huo ndo nakuwa natafuta Dala za kugeukia home .

Siku 1 kama kawaida, nimerudi kwa bibi wa kubatizwa, nikadandia dirisha na kuanza kumuita dogo anifungulie dogo akaropokaa "ahah jamaa unazingua bhna, hapa hakuna mkeo ulitumwa uzaliwe masikini

"
Haha mwamba yale maneno yakanichoma, kesho yake mapema nikaamsha kusiko julikana.
Piga sana kazi za mitaro mixer kubeba vifusi nikawa sichagui kazi. Ndani ya mwezi nikaingia ghetto.
Unyama ukawa mwingi likawa siyo ghetto Bali sehemu ya kuchinjia wanafunzi.
Manzi alipewa mimba,piraa likatimba skani tukasombwa wote..
Ile siku selo niliumia sana!!
Kesi nikawa Sina,maana me niliwapa wadau tu ghetto wawe wanalitumia kuchinjia.
Nikaona hapa msala nikahama mkoa mwengine.
Piga sana saidia fundi. Nikawa fundi njaa.
Jah aka bless nikawa na ghetto langu na Mimi official.
Jina likakuwa nikawa na Kila aina ya material ndani ya ghetto. Hamu ikasogea ya kuwa na chumba nasebu. Nikaona uduwanzi hiyo pesa nikaidundulia nikanunua kiwanja.
Material natolea wapi wakati me fundi maiko bhna.
Ndani ya miezi 4 nikawa nachumba mixer sebu ya kishkaji fundi mwenyewe material nimeokoteza site.

cut story.
Dogo aliyenifukuza kwa bibi yake Ali ni inspire sanaa n Nina mshukuru Hadi kesho namuona kama malaika wangu ambaye alitumwa kuniamsha toka kwenye usingzii wa kubweteka.
Kulipa fadhira dogo nilimsomesha na nikamuingiza kwenye kampuni yangu ya ujenzi.
Hadi leo hajuhi KWANINI namjali na kumpenda Sanaa na hiyo sababu sijawah kumpa zaidi ya wife tu.