Dada upo sahihi, mimi siku zote nawaeleza vijana kuwa unapotaka kueleza jambo ambalo linahitaji discussion ni lazime uwe na facts ili wanaojadili watembee humo na great thinkers watajiongeza.
Papara na uzushi zinawafanya washindwe kujenga hoja.
Kikwete, Rais mzima wa nchi aliikataa fedha yetu iliyopigwa na akina Hybinder Singh na shoga yake Rugemalira kwamba si yetu, Magufuli naye kawakataa wazanzibar waliompigia kura chini ya hiyo hiyo ZEC kuwa hawamhusu ila anaona ni halali awapige wakimletea fyoko.
Hizi kauli za viongozi wa nchi kutishia kuwapiga watu wao zimejaa sana huku Afrika, sijawahi kumsikia kiongozi wa Ulaya akiwaambia hivyo raia wake. Hawa wetu sijui wana wazimu gani.
Ngoja Donald Trump aingie madarakani huko marekani asaidie kuwanyoosha maana anasema nchi itakayojiondoa ICC atairudisha kwa nguvu.
Tanganyika ndipo Magufuli anatawala kule Zanzibar hana chake wale wapo huru sasa ni tofauti na enzi ya Nyerere Rais wa Zanzibar alikuwa makamu wa Rais hata sikukuu za mapinduzi Nyerere ndiyo alikagua gwaride siku hizi Tanganyika imekuwa Mkoloni japo Zanzibar ina Serikali yake ni mbinu za kijanja kukwepa lawama endapo yatatokea majanga Tanganyika itajifanya haina mamlaka huko.
Kikwete, Rais mzima wa nchi aliikataa fedha yetu iliyopigwa na akina Hybinder Singh na shoga yake Rugemalira kwamba si yetu, Magufuli naye kawakataa wazanzibar waliompigia kura kuwa hawamhusu ila anaona ni halali awapige wakimletea fyoko.
Hizi kauli za viongozi wa nchi kutishia kuwapiga watu wao zimejaa sana huku Afrika, sijawahi kumsikia kiongozi wa Ulaya akiwaambia hivyo raia wake. Hawa wetu sijui wana wazimu gani.
Ngoja Donald Trump aingie madarakani marekani awanyooshe kabla hamjaporonyoka kutoka ICC.
Nchi hii ina Vioja vingi Rais anasema yeye hana mamlaka na Zanzibar lakini cha Ajabu majeshi yake ndiyo yamejaa Zanzibar kwa Amri zake, sasa Kama hana mamlaka basi ayatoe majeshi Zanzibar aone watajitawala vipi.
Kwa hiyo suluhisho, la mgogoro uliopo ni kwa cuf kugoma ili wafuatwe kubembelezwa na sio kuwa pro-active kusaka haki?
Sijui kama Shein akishaapishwa anaweza kustep down! Sidhani kama vurugu ni suluhu sahihi kwa both sides!
Ila pia mifano yako haina tija, hakimu anachofanya ni kutusaidia kufanya tafsiri ya vifungu ili kuona uko sahihi au umekosea wapi? Kama sheria ya mita 200 ipo ndani ya sheria zako hakimu hawezi kuificha, na ndio maana ya kudai haki mahakamani, si kusikilizwa matakwa yako!
Ugumu mkubwa kwa wanasiasa wa Tanzania ni kuwa tempted na ujanjaujanja wa ccm nanyi kuujaribu! Definitely vyama tawala duniani vinaweza kupindisha mambo, lkn kama alivyochangia mwenzangu hapo juu mechanisms za kufikia hukumu inaweza kuwa appealed kama haiko sawa! Lkn hata unapo appeal kwa wananchi una ground za kutosha kufanya hivyo!
Kwa case ya znz!
Yes Jecha amezuia matokeo na kuitisha uchaguzi mpya! Kinaweza kuwa kosa, lkn pia anaweza kuwa sahihi!
Seif amejitangaza mshindi jambo ambalo ni kosa kwa sheria za uchaguzi Zanzibar, kitendo kinachoweza hata kumpelekea kufungwa! Lkn Seif pia anaweza kuwa sahihi!
Sasa kipi ni sahihi kati ya hivi, hatuwezi kudebate wananchi, uwe ccm, cuf au chama chochote au huna chama! Ni suala linaloweza kuwa argued na our learned brothers!
Kwanza EU au popote bado ni maana sawa tu, tuna appeal hii issue ktk taasisi tunazohisi zinaweza kutoa maamuzi fulani lkn very unfortunately si EU, US, AU au UN zinazoweza kuhukumu zaidi ya mahakama zetu!
Kama tuna doubt our judicial system basi tujue hatuna nchi na kama hatuheshimu sheria tulizojipangia wenyewe hao EU ndio hatutowaogopa kabisa! Hii ni principle ktk utii wa sheria, tunaanza na kuheshimu taratibu tulizojiwekea kabla ya zile zilizokuwa imposed kwetu!
hakuna haja ya story ndefu haitasaidia kitu, kwa mtizamo wangu hakuna haja ya kurudia Uchaguzi Zanzibar ni bora wamtangaze kwa mabavu Shein awe Rais kuliko kupoteza pesa na mda kufanya uchaguzi ambao matokeo wanayo mfukoni Kama JK alivyofanya kule Dodoma. Kila mzanzibar anajua matokeo ya tarehe 20 yalishapangwa Shein awe mshindi kuna haja gani kupoteza pesa? Mtangazeni Shein kisha Dunia itawahukumu kwa Dhambi yenu kubwa.
Uchaguzi Zanzibar ulishafanyika nje yaani mechi imechezwa nje ya uwanja kilichokuwepo ni kupoteza pesa kuchezea akili za watu tu hakuna jipya hapo zaidi ya kusikia Dr Shein apata Ushindi wa kushindo, demokorasia imebakwa kwa 100%
Jecha hawezi kutangaza mpaka aamrishwe na mahakama. CUF wafungue kesi na Jecha ashitakiwe binafsi. Nina hakika atashindwa kwani hana muhtasari wa kikao cha tume kilichofuta uchaguzi.
Tanzania sio nchi iliyowahi kupata uhuru kwenye historia,ni usanii uliyofanywa na mwenyekiti wa tanu kipindi hicho wewe hujazaliwa,nchi yako halisi ni tanganyika ambayo imejipatia uhuru wake 9-12-1961,kwa maelezo zaidi rudi shule utapata kufahamu tanzania ni kitu gn.
Duh wee Mtaalamu utakuwa umetokea Oman maana majibu yako
Kama wale walio watawala kichwani.
Huko Tanganyika hatuta rudi na kama mnataka kuwa wakimbizi Ulaya au Umangani inabidi muende tu.
Msimsahau Tundu bovu Lissu
hakuna haja ya story ndefu haitasaidia kitu, kwa mtizamo wangu hakuna haja ya kurudia Uchaguzi Zanzibar ni bora wamtangaze kwa mabavu Shein awe Rais kuliko kupoteza pesa na mda kufanya uchaguzi ambao matokeo wanayo mfukoni Kama JK alivyofanya kule Dodoma. Kila mzanzibar anajua matokeo ya tarehe 20 yalishapangwa Shein awe mshindi kuna haja gani kupoteza pesa? Mtangazeni Shein kisha Dunia itawahukumu kwa Dhambi yenu kubwa.
hao mahikimu wameteuliwa na serikali ya ccm unafikiri watatenda haki,halafu tume ya uchaguzi haishitakiwa iko huru,serikali ya tz inamifumo mibaya ya utawala halafu wananchi wamenyamaza kimya ukiona hivyo wtz wengi ni mabogas balaa ndo maana hata chupi yanaagiza china!
“Tunamtaka Rais Magufuli kuonyesha uongozi wake kupitia mgogoro huu wa kisiasa kwa kuingilia kati na kutafuta usuluhishi baina ya vyama vikuu kuhakikisha amani pande zote,” MSEMAJI WA EU.JAMAA HAWAOMBI ILA WANAMTAKA.
Umoja wa Ulaya (EU), umemgomea Rais Dk. John Magufuli, kwa kueleza kuwa msimamo wake ni uliotolewa na washirika wa jumuiya ya kimataifa wa kumtaka kushirikiana na vyama vilivyoshiriki uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar kufikia muafaka.
Akijibu swali la Nipashe kutaka kujua walivyopokea ombi la Rais kwa jumuiya za kimataifa kuzungumza na CUF, ili wakubali kushiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu, Msemaji wa EU, Balozi Roeland van de Geer, alisema wanasubiri kuona utekelezaji wa tamko lao.
“Msimamo wa washirika kadhaa wa jumuiya ya kimataifa nchini, Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wakizungumzia kuhusu uchaguzi wa marudio kufanyika, umeelezewa bayana kwenye tamko lilitolewa Januari 29, mwaka huu,” alisema Balozi Roeland na kuongeza:
“Mpaka sasa EU hatuna la kuongeza zaidi ya tamko hilo linaloelezea msimamo wetu kwa ukamili. Hata hivyo, kwa sasa tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo yake na tunatumaini maendeleo hayo yataleta habari njema kwa wote visiwani humo.”
Januari 29, mwaka huu, EU jumuiya ya kimataifa inayojumuisha nchi za Ubelgiji, Canada, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Hispania, Sweden, Uswisi, Marekani na Uingereza zenye ubalozi nchini, zilitoa tamko la pamoja la kumtaka Rais kuingilia katika mgogoro huo.
“Tunamtaka Rais Magufuli kuonyesha uongozi wake kupitia mgogoro huu wa kisiasa kwa kuingilia kati na kutafuta usuluhishi baina ya vyama vikuu kuhakikisha amani pande zote,” ilisema sehemu ya tamko hilo.
Tamko hilo pia lilieleza kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana, ulikuwa na kasoro zilizoelezwa na kwamba waangalizi wa kutoka Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki, EU, Marekani na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliridhika na mwenendo wa uchaguzi huo.
Walisema wakati mazungumzo baina ya CUF na CCM yakiendelea, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, alitangaza uchaguzi wa marudio.
Tamko hilo lilisisitiza kurejewa kwa mazunguzo ya vyama vinavyovutana na kuwa na maridhiano kuliko kurudi kwenye uchaguzi mpya.
Walisema kurudiwa kwa uchaguzi huo kutaongeza hali ya wasiwasi na sitofahamu visiwani humo, hivyo ni vyema pande zote (CUF na CCM) zikakutana na kuwa na makubaliano ya pamoja na ya amani.
“Ili uwe uchaguzi huru na haki ni lazima pande zote zishiriki. Kwa hali iliyopo kwa sasa itakuwa vigumu kwa waangalizi wa kimataifa kushiriki uchaguzi wa marudio,” lilifafanua tamko hilo.
Mwanzoni mwa Desemba, mwaka jana, waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) walitoa wito kwa ukamilishwaji wa haraka wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar kulingana na kanuni za uchaguzi shirikishi, za uwazi, zinazotekelezwa kwa wakati na kuaminika.
Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, Judith Satgentini, alisema: “EU EOM iko tayari kurejea nchini kuangalia mchakato wa uchaguzi Zanzibar pindi makubaliano ya kuendelea yatakapofikiwa.”
Jecha alitoa tamko la kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25, mwaka jana, baada ya kueleza kasoro tisa zilizojitokeza wakati wa uchaguzi huo.
Kumekuwa na mvutano baina ya chama tawala (CCM) na chama kikuu cha upinzani visiwani humo (CUF). Katika mvutano huo, CUF inataka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, ambao mgombea urais wake, Maalim Seif Sharif Hamad, alijitangaza mshindi kwa kupata kura 200,007 dhidi ya 178,363 alizopata mgombea wa CCM, Dk. Ali Mohammed Shein.
Hivi karibuni mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, alisema: “Baadhi ya watu, mashirika, EU, Marekani, Jumuiya ya Madola na wote walioona kwamba tume haikutenda haki (Zec kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar)… kwamba ingemaliza kuhesabu na matangazo yatoke. Lakini tume iliona kabisa kwamba ikifanya hivyo itakuwa imekiuka maadili yake,“ alisema.
“Kwa hiyo kukawa na mvutano. Kwamba kwa upande wa vyama, walivyopewa maamuzi haya ya tume, wakakaa kuona wafanye nini. Na tukadhani katika hivi vyama kuzungumza kule, na sisi bara watatukaribisha, au Serikali ya Muungano watatukaribisha. Lakini wakasema hata, hili mtuachie sisi wenyewe tutalizungumza kuhusu huu uamuzi wa tume,” alisema Balozi Mahiga.
“Wengine wakasema hata misaada tunasimamisha, kama vile Marekani (Fedha za MCC)… tunasimamisha kwa sababu sisi tunaona haya mazungumzo hayatoi majibu na afadhali tu yatangazwe (matokeo ya uchaguzi) kama yalivyokuwa, lakini katika hilo baadaye tume ikasema jamani, afadhali tuite uchaguzi mwingine.
Akijibu baadhi ya hoja za wabunge zilizotolewa wakati wa mjadala wa Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa 2016/17 Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alisema Rais Magufuli hana mamlaka ya kikatiba ya kuingilia masuala ya Zanzibar.
“Kile ambacho baadhi ya wabunge wamekisema hapa ni kama kuitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia mamlaka ya Zanzibar na tafsiri yake ni kama unataka kuleta hoja ya kujenga serikali moja,” alisema Masaju.
“Hoja kwamba Rais Magufuli aingilie haiwezekani. Mambo ya ulinzi na usalama ndio ya muungano na hicho ndicho kinafanyika Zanzibar kuhakikisha amani na usalama,” alisema.
Vikwazo ni useless kwani misaada wanayotupa inatoka basi? ukiambiwa mkopo/msaada wa bilioni 600 utapewa bilioni 140 zingine zinarudi kwao kwa njia ya 'kutoa ushauri'. Wana akili hao wafadhili!
Mkuu hujui usemalo, Muulize Mugambe utam wa vikwazo, tunaweza kusema tuna dhahabu, national parks au hata kukusanya kodi na kutumia kwa uaminifu, haiwez saidia hata kidogo kwani hata kuuza ulicho nacho utazuiwa kuuza kwao, vikwazo ni balaa kwa nchi changa na maskini kama yetu, kama unabisha muulize putini na iran watakwambia ladha yake, kwa ufupi hatuna jeuri kwa sasa lazima tuhakikishe mgogoro wa Zanzibar unamalizika salama
Kwa hiyo suluhisho, la mgogoro uliopo ni kwa cuf kugoma ili wafuatwe kubembelezwa na sio kuwa pro-active kusaka haki?
Sijui kama Shein akishaapishwa anaweza kustep down! Sidhani kama vurugu ni suluhu sahihi kwa both sides!
Ila pia mifano yako haina tija, hakimu anachofanya ni kutusaidia kufanya tafsiri ya vifungu ili kuona uko sahihi au umekosea wapi? Kama sheria ya mita 200 ipo ndani ya sheria zako hakimu hawezi kuificha, na ndio maana ya kudai haki mahakamani, si kusikilizwa matakwa yako!
Ugumu mkubwa kwa wanasiasa wa Tanzania ni kuwa tempted na ujanjaujanja wa ccm nanyi kuujaribu! Definitely vyama tawala duniani vinaweza kupindisha mambo, lkn kama alivyochangia mwenzangu hapo juu mechanisms za kufikia hukumu inaweza kuwa appealed kama haiko sawa! Lkn hata unapo appeal kwa wananchi una ground za kutosha kufanya hivyo!
Kwa case ya znz!
Yes Jecha amezuia matokeo na kuitisha uchaguzi mpya! Kinaweza kuwa kosa, lkn pia anaweza kuwa sahihi!
Seif amejitangaza mshindi jambo ambalo ni kosa kwa sheria za uchaguzi Zanzibar, kitendo kinachoweza hata kumpelekea kufungwa! Lkn Seif pia anaweza kuwa sahihi!
Sasa kipi ni sahihi kati ya hivi, hatuwezi kudebate wananchi, uwe ccm, cuf au chama chochote au huna chama! Ni suala linaloweza kuwa argued na our learned brothers!
Kwanza EU au popote bado ni maana sawa tu, tuna appeal hii issue ktk taasisi tunazohisi zinaweza kutoa maamuzi fulani lkn very unfortunately si EU, US, AU au UN zinazoweza kuhukumu zaidi ya mahakama zetu!
Kama tuna doubt our judicial system basi tujue hatuna nchi na kama hatuheshimu sheria tulizojipangia wenyewe hao EU ndio hatutowaogopa kabisa! Hii ni principle ktk utii wa sheria, tunaanza na kuheshimu taratibu tulizojiwekea kabla ya zile zilizokuwa imposed kwetu!
Huwezi ifuta CUF labda ufute uraia wa zaidi ya nusu ya wazanzibar na watanganyika zaidi ya 20%, It is indispensable!!! Unalona kwa mtazamo finy sana. Serikali ya Majipu inajtahidi sana, lakni hil za Zanzbar, sijui waweza kumwondolea sifa zote Magu.
Mimi naamini kuwa mahakama ina integrity yake. Kuna mechanism ya kufuatilia kuona kama haki inatendeka. Kama hakuna mechanism hiyo, tujue kuna tatizo kubwa linalohitaji ufumbuzi wa haraka, hata kuliko kuangaika na zec au Jecha.
CUF wameshaambiwa kwamba hata wakienda mahakamani haitasidia maana kesi itakuwa TIME Barred.Pole kwetu hapa Hakimu ni mwanaCCM,anafuata Mwenyekiti wake anavyosema ndivyo anatenda.Refer matamshi ya Magufuli
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.