Ulaya wamgomea Magufuli

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,807
34,193
Ulaya Wamgomea Magufuli

Umoja wa Ulaya (EU), umemgomea Rais Dk. John Magufuli, kwa kueleza kuwa msimamo wake ni uliotolewa na washirika wa jumuiya ya kimataifa wa kumtaka kushirikiana na vyama vilivyoshiriki uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar kufikia muafaka.

Akijibu swali la Nipashe kutaka kujua walivyopokea ombi la Rais kwa jumuiya za kimataifa kuzungumza na CUF, ili wakubali kushiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu, Msemaji wa EU, Balozi Roeland van de Geer, alisema wanasubiri kuona utekelezaji wa tamko lao.

“Msimamo wa washirika kadhaa wa jumuiya ya kimataifa nchini, Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wakizungumzia kuhusu uchaguzi wa marudio kufanyika, umeelezewa bayana kwenye tamko lilitolewa Januari 29, mwaka huu,” alisema Balozi Roeland na kuongeza:

“Mpaka sasa EU hatuna la kuongeza zaidi ya tamko hilo linaloelezea msimamo wetu kwa ukamili. Hata hivyo, kwa sasa tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo yake na tunatumaini maendeleo hayo yataleta habari njema kwa wote visiwani humo.”

Januari 29, mwaka huu, EU jumuiya ya kimataifa inayojumuisha nchi za Ubelgiji, Canada, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Hispania, Sweden, Uswisi, Marekani na Uingereza zenye ubalozi nchini, zilitoa tamko la pamoja la kumtaka Rais kuingilia katika mgogoro huo.

“Tunamtaka Rais Magufuli kuonyesha uongozi wake kupitia mgogoro huu wa kisiasa kwa kuingilia kati na kutafuta usuluhishi baina ya vyama vikuu kuhakikisha amani pande zote,” ilisema sehemu ya tamko hilo.

Tamko hilo pia lilieleza kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana, ulikuwa na kasoro zilizoelezwa na kwamba waangalizi wa kutoka Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki, EU, Marekani na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliridhika na mwenendo wa uchaguzi huo.

Walisema wakati mazungumzo baina ya CUF na CCM yakiendelea, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, alitangaza uchaguzi wa marudio.

Tamko hilo lilisisitiza kurejewa kwa mazunguzo ya vyama vinavyovutana na kuwa na maridhiano kuliko kurudi kwenye uchaguzi mpya.

Walisema kurudiwa kwa uchaguzi huo kutaongeza hali ya wasiwasi na sitofahamu visiwani humo, hivyo ni vyema pande zote (CUF na CCM) zikakutana na kuwa na makubaliano ya pamoja na ya amani.

“Ili uwe uchaguzi huru na haki ni lazima pande zote zishiriki. Kwa hali iliyopo kwa sasa itakuwa vigumu kwa waangalizi wa kimataifa kushiriki uchaguzi wa marudio,” lilifafanua tamko hilo.

Mwanzoni mwa Desemba, mwaka jana, waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) walitoa wito kwa ukamilishwaji wa haraka wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar kulingana na kanuni za uchaguzi shirikishi, za uwazi, zinazotekelezwa kwa wakati na kuaminika.

Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, Judith Satgentini, alisema: “EU EOM iko tayari kurejea nchini kuangalia mchakato wa uchaguzi Zanzibar pindi makubaliano ya kuendelea yatakapofikiwa.”

Jecha alitoa tamko la kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25, mwaka jana, baada ya kueleza kasoro tisa zilizojitokeza wakati wa uchaguzi huo.

Kumekuwa na mvutano baina ya chama tawala (CCM) na chama kikuu cha upinzani visiwani humo (CUF). Katika mvutano huo, CUF inataka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, ambao mgombea urais wake, Maalim Seif Sharif Hamad, alijitangaza mshindi kwa kupata kura 200,007 dhidi ya 178,363 alizopata mgombea wa CCM, Dk. Ali Mohammed Shein.

Hivi karibuni mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, alisema: “Baadhi ya watu, mashirika, EU, Marekani, Jumuiya ya Madola na wote walioona kwamba tume haikutenda haki (Zec kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar)… kwamba ingemaliza kuhesabu na matangazo yatoke. Lakini tume iliona kabisa kwamba ikifanya hivyo itakuwa imekiuka maadili yake,“ alisema.

“Kwa hiyo kukawa na mvutano. Kwamba kwa upande wa vyama, walivyopewa maamuzi haya ya tume, wakakaa kuona wafanye nini. Na tukadhani katika hivi vyama kuzungumza kule, na sisi bara watatukaribisha, au Serikali ya Muungano watatukaribisha. Lakini wakasema hata, hili mtuachie sisi wenyewe tutalizungumza kuhusu huu uamuzi wa tume,” alisema Balozi Mahiga.

“Wengine wakasema hata misaada tunasimamisha, kama vile Marekani (Fedha za MCC)… tunasimamisha kwa sababu sisi tunaona haya mazungumzo hayatoi majibu na afadhali tu yatangazwe (matokeo ya uchaguzi) kama yalivyokuwa, lakini katika hilo baadaye tume ikasema jamani, afadhali tuite uchaguzi mwingine.

Akijibu baadhi ya hoja za wabunge zilizotolewa wakati wa mjadala wa Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa 2016/17 Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alisema Rais Magufuli hana mamlaka ya kikatiba ya kuingilia masuala ya Zanzibar.

“Kile ambacho baadhi ya wabunge wamekisema hapa ni kama kuitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia mamlaka ya Zanzibar na tafsiri yake ni kama unataka kuleta hoja ya kujenga serikali moja,” alisema Masaju.

“Hoja kwamba Rais Magufuli aingilie haiwezekani. Mambo ya ulinzi na usalama ndio ya muungano na hicho ndicho kinafanyika Zanzibar kuhakikisha amani na usalama,” alisema.

Chanzo; Nipashe
 
Sielewi kwa nini cuf kama wanaamini kuwa zec imekosea, si waende mahakamani ili haki ipatikane. Wanaogopa nini kwenda mahakamani?
Kwann humshauri jecha amalizie kutangaza matokeo halali ya uchaguzi uliokamilika?cuf waende mahakamani kufanya nn kwa uchaguzi uliokamilika?
 
Kwann humshauri jecha amalizie kutangaza matokeo halali ya uchaguzi uliokamilika!
Mkuu, huwezi kumshauri mtu mzima kubadili kauli aliyoitoa akiwa timamu. Ufumbuzi ni kumshitaki mahakamani. Sijui kama kuna mbadala.
 
Hiyo mahakama unayoizungumzia ni ipi mkuu,? ya mbinguni au hapahapa Tz

Mimi naamini kuwa mahakama ina integrity yake. Kuna mechanism ya kufuatilia kuona kama haki inatendeka. Kama hakuna mechanism hiyo, tujue kuna tatizo kubwa linalohitaji ufumbuzi wa haraka, hata kuliko kuangaika na zec au Jecha.
 
Sielewi kwa nini cuf kama wanaamini kuwa zec imekosea, si waende mahakamani ili haki ipatikane. Wanaogopa nini kwenda mahakamani?
Tanzania serikali ndo mahakama na serikali ndio ccm unategemea nin.
Tusubiri vikwazo zaidi toka wahisani
 
Tanzania serikali ndo mahakama na serikali ndio ccm unategemea nin.
Tusubiri vikwazo zaidi toka wahisani
Vikwazo ni useless kwani misaada wanayotupa inatoka basi? ukiambiwa mkopo/msaada wa bilioni 600 utapewa bilioni 140 zingine zinarudi kwao kwa njia ya 'kutoa ushauri'. Wana akili hao wafadhili!
 
Kwa hili ili watanganyika mpate salama lazima muukabidhi uhuru wa wazanzubar kwa amani na magufuli asimamie jambo hilo,mukilazimisha kuikalia kimabavu zanzibar ndio hasara kwenu watanganyika.
 
Jamani Tanganyika ni wapi?
Mimi nimezaliwa Tanzania nimesikiasikia tu huko Tanganyika
Wataalamu naomba muelewesho.
 
Jamani Tanganyika ni wapi?
Mimi nimezaliwa Tanzania nimesikiasikia tu huko Tanganyika
Wataalamu naomba muelewesho.
Tanzania sio nchi iliyowahi kupata uhuru kwenye historia,ni usanii uliyofanywa na mwenyekiti wa tanu kipindi hicho wewe hujazaliwa,nchi yako halisi ni tanganyika ambayo imejipatia uhuru wake 9-12-1961,kwa maelezo zaidi rudi shule utapata kufahamu tanzania ni kitu gn.
 
Shein kama anapenda madaraka wakubaliane na mwenzake yeye aongoze miaka 2 na nusu na mwenzake anaye aongoze inayobaki! Madaraka matamu jamani yaani Shein amekubali kujivua nguo hadharani kabisa?
 
Mimi naamini kuwa mahakama ina integrity yake. Kuna mechanism ya kufuatilia kuona kama haki inatendeka. Kama hakuna mechanism hiyo, tujue kuna tatizo kubwa linalohitaji ufumbuzi wa haraka, hata kuliko kuangaika na zec au Jecha.
Kwa Mahakama ipi na katiba ipi?
 
Sielewi kwa nini cuf kama wanaamini kuwa zec imekosea, si waende mahakamani ili haki ipatikane. Wanaogopa nini kwenda mahakamani?

Mkubwa jaribu kuweka kumbukumbu zako sawa,katika mambo mazito kama haya yahusuyo hatima ya siasa zetu,Serikali huitumia mahakama kama "nyundo ya kugongelea msumari wa mwisho wa kuharalisha maamuzi yao".CUF wakilipeleka suala hili mahakamani,mahakama itajivuta kutoa maamuzi na watatoa maamuzi zikiwa zimebaki siku chache kabla ya tarehe ya uchaguzi wa marudio huku ZECCCM ikiendelea kuandaa uchaguzi batili.

Unaikumbuka hukumu ya mita 200? Katika shauri la haki ya mpigakura kusimama mita 200,mahakama ilitumika kupindisha sheria ili kuharalisha na kutoa nafasi ya NECCCM na Chama chake cha Majipu kuiba kura za wananchi.

Tuliokuwa Kanda ya Ziwa kipindi cha uchaguzi tunajuwa yaliyofanyika na kamwe hakuna mwanakiwavijeshi yeyote anayeweza kupinga mbinu chafu zilizotumika kulazimisha ushindi wa ccm kanda ya Ziwa.

Ni kweli kura zilipigwa kwa utulivu,lakini zoezi la kuhesabu na kujumlisha matokeo ndilo lililotumika kuipa ccm ushindi.Siku mbili kabla ya uchaguzi,mstaafu mmoja aliyekuwa amepiga kambi Kahama,aliagiza mamlaka zinazohusika kuhakikisha zinampatia namba za simu za mawakala wote wa vyama vya upinzani.Kupitia namba hizo mchezo ukawa umeisha.

Kumbe ni bora kuendelea kuupinga uchaguzi wa marudio Zanzibar kwa matamko kuliko kukimbilia mahakamani.Majipu yanatamani Maalim Seif aende mahakamani ili yakamalize mchezo,lakini kwa uzoefu wa darasa la M.200,UKAWA haina sababu ya kuwapa viwavijeshi waliotapakaa majipu mwili mzima sababu ya kusingizia kuwa mjadara wa uchaguzi tayari umefungwa na mahakama kuu ya serikali ya majipu,na uchaguzi upo palepale.
 
Kwa hiyo suluhisho, la mgogoro uliopo ni kwa cuf kugoma ili wafuatwe kubembelezwa na sio kuwa pro-active kusaka haki?
Sijui kama Shein akishaapishwa anaweza kustep down! Sidhani kama vurugu ni suluhu sahihi kwa both sides!
Ila pia mifano yako haina tija, hakimu anachofanya ni kutusaidia kufanya tafsiri ya vifungu ili kuona uko sahihi au umekosea wapi? Kama sheria ya mita 200 ipo ndani ya sheria zako hakimu hawezi kuificha, na ndio maana ya kudai haki mahakamani, si kusikilizwa matakwa yako!
Ugumu mkubwa kwa wanasiasa wa Tanzania ni kuwa tempted na ujanjaujanja wa ccm nanyi kuujaribu! Definitely vyama tawala duniani vinaweza kupindisha mambo, lkn kama alivyochangia mwenzangu hapo juu mechanisms za kufikia hukumu inaweza kuwa appealed kama haiko sawa! Lkn hata unapo appeal kwa wananchi una ground za kutosha kufanya hivyo!
Kwa case ya znz!
Yes Jecha amezuia matokeo na kuitisha uchaguzi mpya! Kinaweza kuwa kosa, lkn pia anaweza kuwa sahihi!
Seif amejitangaza mshindi jambo ambalo ni kosa kwa sheria za uchaguzi Zanzibar, kitendo kinachoweza hata kumpelekea kufungwa! Lkn Seif pia anaweza kuwa sahihi!
Sasa kipi ni sahihi kati ya hivi, hatuwezi kudebate wananchi, uwe ccm, cuf au chama chochote au huna chama! Ni suala linaloweza kuwa argued na our learned brothers!
Kwanza EU au popote bado ni maana sawa tu, tuna appeal hii issue ktk taasisi tunazohisi zinaweza kutoa maamuzi fulani lkn very unfortunately si EU, US, AU au UN zinazoweza kuhukumu zaidi ya mahakama zetu!
Kama tuna doubt our judicial system basi tujue hatuna nchi na kama hatuheshimu sheria tulizojipangia wenyewe hao EU ndio hatutowaogopa kabisa! Hii ni principle ktk utii wa sheria, tunaanza na kuheshimu taratibu tulizojiwekea kabla ya zile zilizokuwa imposed kwetu!
 
Ahaa kumbe. Asante kwa ufafanuzi, mkuu
Mkubwa jaribu kuweka kumbukumbu zako sawa,katika mambo mazito kama haya yahusuyo hatima ya siasa zetu,Serikali huitumia mahakama kama "nyundo ya kugongelea msumari wa mwisho wa kuharalisha maamuzi yao".CUF wakilipeleka suala hili mahakamani,mahakama itajivuta kutoa maamuzi na watatoa maamuzi zikiwa zimebaki siku chache kabla ya tarehe ya uchaguzi wa marudio huku ZECCCM ikiendelea kuandaa uchaguzi batili.

Unaikumbuka hukumu ya mita 200? Katika shauri la haki ya mpigakura kusimama mita 200,mahakama ilitumika kupindisha sheria ili kuharalisha na kutoa nafasi ya NECCCM na Chama chake cha Majipu kuiba kura za wananchi.

Tuliokuwa Kanda ya Ziwa kipindi cha uchaguzi tunajuwa yaliyofanyika na kamwe hakuna mwanakiwavijeshi yeyote anayeweza kupinga mbinu chafu zilizotumika kulazimisha ushindi wa ccm kanda ya Ziwa.

Ni kweli kura zilipigwa kwa utulivu,lakini zoezi la kuhesabu na kujumlisha matokeo ndilo lililotumika kuipa ccm ushindi.Siku mbili kabla ya uchaguzi,mstaafu mmoja aliyekuwa amepiga kambi Kahama,aliagiza mamlaka zinazohusika kuhakikisha zinampatia namba za simu za mawakala wote wa vyama vya upinzani.Kupitia namba hizo mchezo ukawa umeisha.

Kumbe ni bora kuendelea kuupinga uchaguzi wa marudio Zanzibar kwa matamko kuliko kukimbilia mahakamani.Majipu yanatamani Maalim Seif aende mahakamani ili yakamalize mchezo,lakini kwa uzoefu wa darasa la M.200,UKAWA haina sababu ya kuwapa viwavijeshi waliotapakaa majipu mwili mzima sababu ya kusingizia kuwa mjadara wa uchaguzi tayari umefungwa na mahakama kuu ya serikali ya majipu,na uchaguzi upo palepale.
 
Kila nikiisoma mada iliyopo katika post namba moja, sioni pahala ambapo EU imegoma na wala sijakiona cha kugomea.

Nilichokiona nnaweza kusema kuwa Magufuli ndiyo kawagomea EU.

Kichwa cha habari na utumbo wa habari havirandani kabisa.

Mleta mada unaejiita MziziMkavu hebu onesha ni wapi na kipi walichomgomea Magufuli hao EU.
 
Back
Top Bottom