Ulaya pamenishinda narudi bongo

Status
Not open for further replies.
Pole sana bro, najua jinsi Ulaya palivyo pagumu kuanza bila ya kuwa na connection za kikazi hasa Sweden. Cha kufanya ni kurudi nyumbani mapema au kuanza chini, cleaning jobs zinasaidia kwa kuanzia, ila sasa una visa ya kufanya kazi? Jaribu kuongea na watu wa kanisa lako kama wanafahamu jinsi ya kupata sponsor wa masomo kisha soma chochote hata kiswed, kitambulisho chako cha shule kitakupa kazi na visa ya kusoma pia itakupa kazi. Kila la heri.
 
Unafikir Euro 15,000 ni mchezo mkuu...unajitahidi unaipata tu!!??
 
Watu wanafikir mambo mepesi tu,...Kama huna host wakueleweka,then you're unskilled, nakuambia utanyooka zaidi ya rula...siku utakayotoboa na kuishi kwenye apartment kali basi hadi kizazi chako cha tano kitaikumbuka hiyo siku japo you'd be no more.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kha
 
Hongera kwa kujitambua. Maisha ya mbele ni magumu sana.
 
Europe ukienda mikono mitupu bila professional kama mkimbizi huna cheti huna lolote inategemea ufike utoboe kwa kubeba box elitrea, west africa,Somalia wamejaa wanauza bangi mfano nchi kama uswiss waulaya wenyewe wanaitolea macho Achilia wewe mbongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ughaibuni utapafurahia kama umeenda kwa kujipanga.

1. Umesoma katika nyanja yenye kuhitajika sana kwenye nchi nzuri, sio ilimradi tu ughaibuni.
2. Una vibali vya kuishi na kufanya kazi.
3. Una mipango mizuri ya biashara yenye demand kubwa.
4. Una uvumilivu na subira kutekeleza malengo ya muda mrefu.
5. Unaweza ku focus kwenye malengo yako bila kutetereka na tamaa za starehe, madawa ya kulevya, makundi.

Nimeishi maisha hayo takriban miaka 20 Marekani, na sijajutia maamuzi yangu ya kuhamia Marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulipowaambia mapopoma wengi walibisha na hasa wale wanaodai aheri kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa mwanandamu Bongo,kwa mtu ambaye mwisho wake kusafiri ni Dar ataamini kuwa huko majuu maisha ni rahisi,kiuhalisia Bongo ni peponi,na hata Le mutuz alipoandika humu watu walimkebehi tena hao ni wale ambao hata pasipoti hawajui ni kitu gani.ndugu yangu rudi tu nyumbani afadhali umejionea mwenyewe.Hilo box hakuna labda kwenda kuosha sefuria kwenye migahawa ya Wahindi na kulipwa nusu ujira.
 
Kiongozi.

Umeamua kuharibu.

Kimya kimya ndio ulikuwa mwendo mzuri yaani kama unafukuza Mwizi halafu hutaki watu wajue waje kumuokoa.

Hakuna kilichoharibika.

Usipate tabu kupoteza muda wako.

Mbivu na mbichi ushazijua
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…