Ulaya pamenishinda narudi bongo

Ulaya pamenishinda narudi bongo

Status
Not open for further replies.
Kinachomsumbua jamaa na kumfanya atamani kurudi bongo baada ya kufika huko na kukaa kipindi hiki kifupi ni kitu wanaita"home sickness". Ulaya hasa Scandinavia mfumo wao wa maisha ni tofauti sana ukilinganisha na tz. Huko kila mtu yupo busy na mishe zake hakuna muda wa kukaa vijiweni kupiga soga na kubishana nani zaidi kati ya Simba au Yanga ambayo tunaita "socialization". Ulaya hakuna 'socialization" kiasi kikubwa kama nchi zetu za kiafrica.

Kingine ni utofauti wa kitamaduni kwa ujumla wanaita "cultural shock" ikiwa ni pamoja na chakula. Kipindi cha miezi mi 3 hadi mwaka ni kipindi cha "transition" na "realization". Yaani unaniona ulaya halisi sio Ile ya kusadikika ama uisomavyo mitandaoni au uionayo kwenye tv. Hiki ndio kipindi mtoa mada anakabiliana nacho na ndio anahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kutokata tamaa kwani kuna Mambo mengi atayaona tofauti na ambavyo amesikia yakidithiwa kuhusu ulaya. Akitoboa kipindi hiki cha transition atakuja kutuambia habari nyingine kabisa.

Nakubaliana na mchangiaji mmoja kwamba ajichanganye na wa Congo, warundi ama west Africans, hawa wenzetu wapo sharp na risk takers hivyo watamsaidia kumpa ujanja na vichochoro vya kupita japokuwa awe nao makini pia wanaweza muingiza pia chaka. Wa-tz ulaya hawana msaada sana, kuna sababu yake ambayo kuna siku nitashusha Uzi wa hii issue.

Cha mwisho, namshauri kama tayari anapo mahala pa kulala na kula pa uhakika hapo Sweden basi ajichukulie mwenye bahati kubwa sana na kama ni marathon basi yeye tayari yupo Mita 100 mbele ya wenzake atulize ball mambo yatajiseti time after time. Ila kama imejishkiza tu kwa washkaji atafute mchongo ahamie Norway, Denmark au Germany. Huko kuna utofauti kidogo na namna nyingi za kuishi.

Ni hayo machache nikijaribu ku share uzoefu wangu wa miaka takribani mi5 niliyoishi scandavia na ulaya Kwa ujumla..way back 2007-2011.

Nilienda ulaya nikiwa kijana mdogo sana "fresh graduate from UDSM" and very ambitious. Nashukuru nilibeba box za kutosha nikajisomesha Masters na kurudi tz kujenga nchi. Sikuwahi kujuta kwenda na sikuwahi kujuta kurudi baada ya kukamilisha malengo yangu yaliyonipeleka huko.
Ukute hili jamaa limewawaza akina Mwajuma tu! Vijana wa Kibongo kupenda chini kunawaponza!
 
Mim mwehu ndama kijana wa kitanzania niliwah kuandika uzi kuomba msaada kuhusu jinsi yakupata visa yakuingia nchini Sweden, na nashukuru Kwa maoni ya baadhi ya wadau nilifanikiwa kufuata ushauri nakufanikiwa kutia maguu ndani ya bara la uropa.

Lakini tangu nilipotoka bongo nakufika hapa ughaibuni huku kichwani nikiwa na lengo la kujilipua nakubaki huku moja Kwa moja maisha yamekua tofauti na nilivyo fikiria..
Ukizingatia mwenyeji wangu nayeye anaishi hapa kiujanja ujanja.

Niliomba visa ya wiki 3 na bahati nzuri baada yakufika hapa na nlipokaribia KUMALIZA muda wangu waliniongeza miezi mingine 3.

Lakini sasa sioni kinachobadilika katika maisha yangu zaidi yakupata huduma nzuri ya chakula nakuvuta hewa Safi hapa Uppsala .

Kiukweli maisha ya hapa yanazidi kuwa magumu Kwa upande wangu sababu nimejaribu kuanzisha mahusiano na mabinti, wanawake watu wazima Hadi vikongwe ili kusudi atakae jaa nioe ili niweze kupata makaratasi lakini nawao wamekuwa wagumu.

Sitaki kujivika status za kikimbizi maana nahisi ntaaribu kabisa mpangilio wote wa maisha yangu nakuitendea ubaya elimu yangu niliyoipata Kwa shida bongo land.

Nimekua mzururaji na cha ajabu hata zile KAZI za kubeba box nilizokua nazisikia zikisemwa Sana na wadau humu jf sizipati.

Kwa kifupi uchumi wangu umedidimia mara 100 zaidi ya hata nilivyokua bongo , mpaka najuta Kwa nini nilitumia pesa yangu nlioichanga Kwa shida kama nauli yakuja huku uzunguni pasipo na manufaa ya kiuchumi kwangu.

Hapa navyoongea nimeshawasilisha ombi la msaada wa nauli ya kurudi nyumbani katika kanisa naloSali hapa Uppsala.

Kwa kifupi narudi nyumbani na nikifika hapo Kwa mkuu jiwe naenda moja Kwa moja kijijini kwetu namanditi songea kulima.

Bye bye wabongo mliopo Sweden mim maisha yamenishinda narudi nyumbani.

View attachment 1389715View attachment 1389716

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu mtafute huyu hapa chini akakusaida maana yeye anakula matunda ya ulaya kama unashuka kitonga
 
Hebu mtafute huyu hapa chini akakusaida maana yeye anakula matunda ya ulaya kama unashuka kitonga
Ndiyo yule yule mtu mmoja saivi ameshapata kazi😂😂
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom