Ulaya pamenishinda narudi bongo

Ulaya pamenishinda narudi bongo

Status
Not open for further replies.
Mtoto mchele mchele wewe... kwenda kwenyewe yondo sister umefunga mkanda! Wenzio hapo tumeingia kwa kupiga mitumbwi ndo tukaingia pande hizo. ila haikuwa mavumba tukarost na kurudishwa bongo kula vitumbua vya moto na mihogo ya kukaanga. Yani ww kiwanja ushaingia tena umepokelewa maji moto maji baridi miezi mitatu tu umembwela😯 inaonekana hata huku bongo maisha yenu mboga saba ugali kitenesi. Kwa hiyo ww ulitegemea ukiingia kiwanja tu kuna miti ya hela? Afu nyie ndo mkirudi mnakuja kuongea udwanzi habari za viwanja. Kibaharia una kesi ya kujibu☹

Inaboa kishenzi unaona mwanaume mzima analia nje hakufai..dah hizo bahati sijui kwanini wengie hatupati!.
 
Mim mwehu ndama kijana wa kitanzania niliwah kuandika uzi kuomba msaada kuhusu jinsi yakupata visa yakuingia nchini Sweden, na nashukuru Kwa maoni ya baadhi ya wadau nilifanikiwa kufuata ushauri nakufanikiwa kutia maguu ndani ya bara la uropa.

Lakini tangu nilipotoka bongo nakufika hapa ughaibuni huku kichwani nikiwa na lengo la kujilipua nakubaki huku moja Kwa moja maisha yamekua tofauti na nilivyo fikiria..
Ukizingatia mwenyeji wangu nayeye anaishi hapa kiujanja ujanja.

Niliomba visa ya wiki 3 na bahati nzuri baada yakufika hapa na nlipokaribia KUMALIZA muda wangu waliniongeza miezi mingine 3.

Lakini sasa sioni kinachobadilika katika maisha yangu zaidi yakupata huduma nzuri ya chakula nakuvuta hewa Safi hapa Uppsala .

Kiukweli maisha ya hapa yanazidi kuwa magumu Kwa upande wangu sababu nimejaribu kuanzisha mahusiano na mabinti, wanawake watu wazima Hadi vikongwe ili kusudi atakae jaa nioe ili niweze kupata makaratasi lakini nawao wamekuwa wagumu.

Sitaki kujivika status za kikimbizi maana nahisi ntaaribu kabisa mpangilio wote wa maisha yangu nakuitendea ubaya elimu yangu niliyoipata Kwa shida bongo land.

Nimekua mzururaji na cha ajabu hata zile KAZI za kubeba box nilizokua nazisikia zikisemwa Sana na wadau humu jf sizipati.

Kwa kifupi uchumi wangu umedidimia mara 100 zaidi ya hata nilivyokua bongo , mpaka najuta Kwa nini nilitumia pesa yangu nlioichanga Kwa shida kama nauli yakuja huku uzunguni pasipo na manufaa ya kiuchumi kwangu.

Hapa navyoongea nimeshawasilisha ombi la msaada wa nauli ya kurudi nyumbani katika kanisa naloSali hapa Uppsala.

Kwa kifupi narudi nyumbani na nikifika hapo Kwa mkuu jiwe naenda moja Kwa moja kijijini kwetu namanditi songea kulima.

Bye bye wabongo mliopo Sweden mim maisha yamenishinda narudi nyumbani.

View attachment 1389715View attachment 1389716

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtafute Ngurumo
 
Mleta uzi kachezea za uso mpaka hajarudi tena kuandika chochote kulingana na comments za wadau.😂..au cjui ndo keshafika kijijini mtandao umekata!🤔🤔
 
Karekebisha haraka kabla hakijanuka.

Basi kausha kimya kimya, najua ushanielewa mtu mzima

Mkuu Parabora , upo Bongo? ama Uswisi?
IMG_20200511_125135.jpg

Cc: HARUFU , Guus

-Kaveli-
 
Asirudi ulaya kutokea Sweden?

-Kaveli-
ndugu yangu acha kuwa kichwa ngumu mkuu jamaa anasema anaondoka sweden, mimi nimemjibu asirudi tena tatzo la kuelewa linakujaje mkuu au tuandike kiingereza mbona meseji inaeleweka hiyo au nini haswa point yako, tufupishe mjadala?
 
Title ya uzi pamoja na contents vinareflect hiki: "Ulaya pamenishinda narudi bongo".

Halafu wewe ambaye huwa unajitambulisha kuwa upo Uswisi ukacomment hivi:
IMG_20200511_133131.jpg

Hadi hapo huoni kwamba 'ushamchanganya' msomaji wa threads zako unazosimuliaga kwamba upo Uswisi? Just by common sense, huuoni kabisa huo utatanishi hapo?

Naona ushaanza kupanic 😁.

-Kaveli-
 
Title ya uzi pamoja na contents vinareflect hiki: "Ulaya pamenishinda narudi bongo".

Halafu wewe ambaye huwa unajitambulisha kuwa upo Uswisi ukacomment hivi:
View attachment 1447001

Hadi hapo huoni kwamba 'ushamchanganya' msomaji wa threads zako unazosimuliaga kwamba upo Uswisi? Just by common sense, huuoni kabisa huo utatanishi hapo?

Naona ushaanza kupanic 😁.

-Kaveli-
mimi sijapanick mkuu ila nilikuwa sielewi hasa unataka nini , na kumbe ishu ni hiyo mkuu, basi tufanye niko bongo. tufunge huu mjadala
 
Mim mwehu ndama kijana wa kitanzania niliwah kuandika uzi kuomba msaada kuhusu jinsi yakupata visa yakuingia nchini Sweden, na nashukuru Kwa maoni ya baadhi ya wadau nilifanikiwa kufuata ushauri nakufanikiwa kutia maguu ndani ya bara la uropa.

Lakini tangu nilipotoka bongo nakufika hapa ughaibuni huku kichwani nikiwa na lengo la kujilipua nakubaki huku moja Kwa moja maisha yamekua tofauti na nilivyo fikiria..
Ukizingatia mwenyeji wangu nayeye anaishi hapa kiujanja ujanja.

Niliomba visa ya wiki 3 na bahati nzuri baada yakufika hapa na nlipokaribia KUMALIZA muda wangu waliniongeza miezi mingine 3.

Lakini sasa sioni kinachobadilika katika maisha yangu zaidi yakupata huduma nzuri ya chakula nakuvuta hewa Safi hapa Uppsala .

Kiukweli maisha ya hapa yanazidi kuwa magumu Kwa upande wangu sababu nimejaribu kuanzisha mahusiano na mabinti, wanawake watu wazima Hadi vikongwe ili kusudi atakae jaa nioe ili niweze kupata makaratasi lakini nawao wamekuwa wagumu.

Sitaki kujivika status za kikimbizi maana nahisi ntaaribu kabisa mpangilio wote wa maisha yangu nakuitendea ubaya elimu yangu niliyoipata Kwa shida bongo land.

Nimekua mzururaji na cha ajabu hata zile KAZI za kubeba box nilizokua nazisikia zikisemwa Sana na wadau humu jf sizipati.

Kwa kifupi uchumi wangu umedidimia mara 100 zaidi ya hata nilivyokua bongo , mpaka najuta Kwa nini nilitumia pesa yangu nlioichanga Kwa shida kama nauli yakuja huku uzunguni pasipo na manufaa ya kiuchumi kwangu.

Hapa navyoongea nimeshawasilisha ombi la msaada wa nauli ya kurudi nyumbani katika kanisa naloSali hapa Uppsala.

Kwa kifupi narudi nyumbani na nikifika hapo Kwa mkuu jiwe naenda moja Kwa moja kijijini kwetu namanditi songea kulima.

Bye bye wabongo mliopo Sweden mim maisha yamenishinda narudi nyumbani.

View attachment 1389715View attachment 1389716

Sent using Jamii Forums mobile app
kunahitaji uvumilivu mkuu
 
Kama huna pesa bongo usije bora kuwa illegal migrant tu huko huku ukifanya kazi kwenye mashamba huko

Jitahidi ukitaka kurudi bongo angalau uwe hata na € 15000 za kuanzia hapa bongo otherwise hata papuchi za bongo zitakushunda kununua utakufa na ugumu wako kutoka ulaya

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi tuongee in reality..huko Ulaya kunawshindaje? Au ni mm tu nnayeona umaskini wa chii hii jamani..mideals mikubwa wanapeana wao..arghh
 
Mkuu komaa huko huko ila kama unataka kurudi namanditi, pitia hapa songea mjini tupate kitimoto na bia unipe stori za mbele

aim for the stars
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom