Ulaya pamenishinda narudi bongo

Ulaya pamenishinda narudi bongo

Status
Not open for further replies.
Kiongozi kwaio vzr usome lugha yao hata miezi flani km short course ausio? Wkt ume ingia na je hizi permits ina kuaje mkuu hebu tu fungulie kgd Kiongozi
1. Kufahamu lugha yao ni jambo muhimu iwapo unahitaji kweli kuzamia/kuishi. Namna gani utafahamu lugha hilo ni jambo lingine ambalo unaweza kutumia njia mbalimbali ikiwamo njia ya online studies (Youtube n.k)
2.Kupata permit ya kuishi/kuingia nchi nyingine ni issue kubwa kidogo. Kwanza uwe na passport, kisha uanze kuomba VISA/Residence permit ambapo unatakiwa na sababu maalumu; mfano masomo, kutalii, mwaliko wa aina yoyote n.k. masharti mengine utayafahamu ukishaanza mchakato.
 
Huyu Mwehu atakuwa karudi kweli!!! Maana flights zote zipo grounded bcause of corona!! Labda aje na dege la mizigo linalokuja kuchukua mboga mboga pale KIA!!!
 
Pole sana, angalau umethubutu kukiri mapema kuwa ughaibuni hapajakufaa, wazamiaji wengine hawasemi lolote hukomaa kibishi wakati wakiwa na maisha magumu tu. Mkataa kwao ni mtumwa, we rudi tu home ilimradi usije kutuongezea Corona hapa nyumbani.

Kutamani kwako kurudi hakutukatishi tamaa sie wengine wenye ndoto za kuja ughaibuni, tutakuja tu! Maana hapa maisha sio kabisa. Sie hatuamini kama huko ni pagumu, labda ni fikra zako za kupambana zimefikia ukomo. Hao mademu na vibibi ulivyotongoza ndani ya miezi mitatu ni vingapi!? Yaani ilitoka bongo, weapon yako kubwa ikiwa ni mb*o... Na haijakupa matumaini yoyote ndani ya kipindi cha miezi mitatu! Uliamini wanaume walioko huko wote ni vibamia, kwamba umekwenda kuwakomboa kina mama na vibibi kwa kutofikishwa Uhuru peak!? Acha uboya mwana!! Komaa!! Mawazo ya kurudi bongo ni uchuro kabisa, bora hata awamu hii ingekuwa inafika ukingoni. Ukirudi utajuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
hahaaha yani paragraph ya kwanza haihusiani na ya pili....juu ushauri wa hekma chini naona umetumia mbinu za usutaji za kina mama wa uswahilini ..
 
Pole sana, nchi za ulaya zina sheria zake. Kama huko Sweden kwanza ujue lugha yao. Kwa sisi kibongo bongo bora uzamie nchi ambayo first language ni English. Juu ya yote kama huna work permit utasumbuka unless uwe na mwenyeji wa kukulisha . Ila ukiwa na Kibali cha kazi tu ( naongelea UK) unatoka usiwe mvivu anzia na kazi za unskilled ( kulea vizee. Kazi hiyo ina hela) baadae cv yako unai upgrade mengine yanafuata ila mwanzo ni mgumu
 
Mim mwehu ndama kijana wa kitanzania niliwah kuandika uzi kuomba msaada kuhusu jinsi yakupata visa yakuingia nchini Sweden, na nashukuru Kwa maoni ya baadhi ya wadau nilifanikiwa kufuata ushauri nakufanikiwa kutia maguu ndani ya bara la uropa.

Lakini tangu nilipotoka bongo nakufika hapa ughaibuni huku kichwani nikiwa na lengo la kujilipua nakubaki huku moja Kwa moja maisha yamekua tofauti na nilivyo fikiria..
Ukizingatia mwenyeji wangu nayeye anaishi hapa kiujanja ujanja.

Niliomba visa ya wiki 3 na bahati nzuri baada yakufika hapa na nlipokaribia KUMALIZA muda wangu waliniongeza miezi mingine 3.

Lakini sasa sioni kinachobadilika katika maisha yangu zaidi yakupata huduma nzuri ya chakula nakuvuta hewa Safi hapa Uppsala .

Kiukweli maisha ya hapa yanazidi kuwa magumu Kwa upande wangu sababu nimejaribu kuanzisha mahusiano na mabinti, wanawake watu wazima Hadi vikongwe ili kusudi atakae jaa nioe ili niweze kupata makaratasi lakini nawao wamekuwa wagumu.

Sitaki kujivika status za kikimbizi maana nahisi ntaaribu kabisa mpangilio wote wa maisha yangu nakuitendea ubaya elimu yangu niliyoipata Kwa shida bongo land.

Nimekua mzururaji na cha ajabu hata zile KAZI za kubeba box nilizokua nazisikia zikisemwa Sana na wadau humu jf sizipati.

Kwa kifupi uchumi wangu umedidimia mara 100 zaidi ya hata nilivyokua bongo , mpaka najuta Kwa nini nilitumia pesa yangu nlioichanga Kwa shida kama nauli yakuja huku uzunguni pasipo na manufaa ya kiuchumi kwangu.

Hapa navyoongea nimeshawasilisha ombi la msaada wa nauli ya kurudi nyumbani katika kanisa naloSali hapa Uppsala.

Kwa kifupi narudi nyumbani na nikifika hapo Kwa mkuu jiwe naenda moja Kwa moja kijijini kwetu namanditi songea kulima.

Bye bye wabongo mliopo Sweden mim maisha yamenishinda narudi nyumbani.

View attachment 1389715View attachment 1389716

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto mchele mchele wewe... kwenda kwenyewe yondo sister umefunga mkanda! Wenzio hapo tumeingia kwa kupiga mitumbwi ndo tukaingia pande hizo. ila haikuwa mavumba tukarost na kurudishwa bongo kula vitumbua vya moto na mihogo ya kukaanga. Yani ww kiwanja ushaingia tena umepokelewa maji moto maji baridi miezi mitatu tu umembwela😯 inaonekana hata huku bongo maisha yenu mboga saba ugali kitenesi. Kwa hiyo ww ulitegemea ukiingia kiwanja tu kuna miti ya hela? Afu nyie ndo mkirudi mnakuja kuongea udwanzi habari za viwanja. Kibaharia una kesi ya kujibu☹
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom